Fareed wa UAMSHO apingana na dereva wake

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
20,690
20,445
Nilimsikia kwa makini dereva wa sheikh Fareed wa UAMSHO akielezea jinsi walivyoachana na sheikh Faeed. Nimemsikia Fareed mwenyewe akieleza jinsi alivyoachana na dereva wake. Wote wanasema dereva alitumwa na Fareed akanunue umeme, hapo hawajatofautiana.

Tofauti inakuja pale ambapo dereva amesema alimuacha Fareed anaenda kwenye gari (la waliomteka) wakati Fareed anasema gari (la waliomteka) lilikuja wakati dereva ameenda kununua umeme.

Kwa lugha nyingine, dereva anasema aliliacha gari la watekaji likiwa limeshafika na Fareed alilifuata mwenyewe, lakini Fareed amesema wakati gari (la waliomteka) linafika, dereva hakuwepo!

Wachambuzi wa mambo hebu angalieni hapo, inavyoonekana huyu sheikh hakuipanga vizuri hii movie na dili limeshabumbuluka!
 
Hii movie bado haijatulia,wangembuomba kova awasaidia si unakumbuka alivyoicheza ya dr uli
 
Toka mwanzo ilionekana ni movie....dunia sijui inaelekea wapi. Hivi wanahisia kweli kuwa mchezo wao umegharimu maisha ya mtu? Na kwa nini watu wachache waone kuwa wao ndio wanastahili kuishi na sio wengine?
 
Hii sinema imekosewa kwenye utunzi, sterling hakumshirikisha dereva wake kwenye baadhi ya mbinu za kunogesha movie.
Uongo mwingi tutaujua tu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Njia ya muongo fupi, na ukiwa na muongo uwe na kumbukumbu nzuri. Huyo Sheikh Farid na wapambe wake walisahau kipengele kimoja wakati wanasuka namna ya kujificha. Walisahau kumpa tuition dereva ili atoe maelezo yanayofanana nao.

Na kwa bahati (mbaya/nzuri) dereva alitoa maelezo almost immidiately baada ya taarifa za kutekwa, ana anaeleza kuwa Sheikh aliingia kwenye gari nyingine bila bugha. Hayo mambo ya kutekwa ndiyo mimi nayaita mchezo wa kombolela, ni mchezo wa kitoto.
 
Licha ya kupingana na dereva wake, jamaa kuna vitu kijichanganya sana, anasema alipokuwa kwenye nyumba ya watekaji hakula chochote kwani hakuwaamini, SAWA! ila alikuwa anakunywa maji akienda msalani sasa ndugu huko msalani ulikunywaje maji wakti umesema ulikuwa umefungwa pingu na ulikuwa umefungwa kitambaa au ikifika time ya msalani walikuwa wanakufungua,halafu unasema hata sura zao hukuzijua vipi ukijue hiki ndo choo na uweze kujisaidia na kunywa maji,????? damu ya watu mloimwaga itawalilia!
 
Sijui kilichotokea, lakini yule dereva nilivyomuona pale ITV, ni muongo.
 
Sijui kilichotokea, lakini yule dereva nilivyomuona pale ITV, ni muongo.
Inawezekana sheikh ndio muongo, au dereva, au wote wawili. Nimedownload hiyo audio clip kwani nimeona wakishagundua kuwa wamechemka, hawakawii kuiondoa kwenye server
 
halafu mijitu mingine inaingia hapa eti serikali ya zenj ilimteka mtu aliyejifanya katekwa, kaamua kujificha ili kuharibu hali ya hewa. Hawa ni majambazi mimi nashangaa eti mpaka sasa hawajakamatwa. Kubukeni kuna maaskari 2 wamepoteza maisha kwa 7bu za ushinzi wa hawa jamaa, Hivi serikali impaka sasa haijamtia nguvuni?
 
Hii mizoga kwa nini tusiachane nayo tu ili yawe yanakuja Tanganyika kwa visa.
 
Fareed, anadhani watu wote wamepungukiwa kama yeye. Uwazi wa uwongo huo unaothibitishwa na kutofautiana kwa kauli kati ya dereva na gaidi Fareed nami niliuona. Good observation. Uwongo nao unahitaji akili, si kila mtu anaweza kudanganya na watu wakadanganyika.
 
halafu mijitu mingine inaingia hapa eti serikali ya zenj ilimteka mtu aliyejifanya katekwa, kaamua kujificha ili kuharibu hali ya hewa. Hawa ni majambazi mimi nashangaa eti mpaka sasa hawajakamatwa. Kubukeni kuna maaskari 2 wamepoteza maisha kwa 7bu za ushinzi wa hawa jamaa, Hivi serikali impaka sasa haijamtia nguvuni?
Ni kwa nini wakamatwe badala ya kuuwawa kabisa?
 
Huyu ni Gaidi...ndio maana Yule mwenye post isemayo "apatikana" nilim challenge kuwa swala sio kupatikana cause hakutekwa...so angesema tu jamaa karudi nyumbani kwake..
 
Inaonekana kiswahili sio lugha yako. Sheikh farid amesema baada ya jamaa kwenda kununua umeme gari la wateka nyara lilijitokeza, inawezekana dereva aliliona gari lakini sheikh farid hawezi kumsemea dereva, yy anachoelewa dereva dereva aliondoka kwenda kununua umeme, ikumbukwe dereva alijua kama sh farid ana miadi na mtu na sehemu aliokuepo sh farid na dukani sio mbali mmnaweza kuonana btn 2points

Back
Top Bottom