Fanya haya ufurahie maisha ya ndoa

Fanya haya ufurahie maisha ya ndoa

Mazoko

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2009
Posts
674
Reaction score
187
Kunamambo napenda tuyazungumze kwa wale waliondani ya ndoa ili tuimalishe ndoa zetu pia hii itawasaidia hata wale wanaotaka kuingia au kuanza mahusiano wadumu kwenye ndoa zao:

1.Nijinsigani tunaweza kumaliza ugomvi wetu ndani yandoa.

i).Kwanza hakikisha kuwa mda wakuongelea tatizo wote mnakuwa katika hali ya kawaida kwa maana mmetulia.

ii).Hakikisha mnajitahidi kuongea kwa sauti ya kawaida yenyekutafuta kutatua tatizo.

iii)Hakikisha hulali na jambo lililokukwaza.

iv)Usilale nje ya chumba chako kama njia yakumkomoa mwenza wako.

2.Onyesha upendo kwa mwenza wako bila kuchoka ikibidi uwe wakwanza kumfariji panapotokea tatizo,tambua uwepo wake kwako.

3.Usimwite mwenza wako jina lisilostahili mshenzi,malaya,mbwa nk.

4.Tabia za nje usinziamishie nyumbani kwako.

5.Msigombane mbele ya watoto au watu.

6.Fahamu shughuli na kipato cha mwenza wako.

7. Heshimu familia zenu kwa maana wazazi wenu.

8.Jambo lolote baya msilitoe nje.

9.Furahia kutembea na mwenza wako kwenye shughuli inayowahusu na ujisikie fahari kuwa naye eneo hilo.

10.Kubaliana na kila hali inayokukabiri naisiwe chanzo chaugomvi.

Yako mengi tunaweza kufanya ili kudumisha ndoa zetu,tufanye haya ili nyumba zetu ziwe ndiyo sehemu ya mapumziko.
 
Aksante kwa mawazo chanya, shida ni vitendo ni vigumu kuliko nadharia.
 
Umesomeka But Hakuna Mwalimu Wa Ndoa! Labda Mmoja Wa Wanandoa Akubali Kuwa B,w,e,g.e
 
kusema ni rahisi kuliko kutenda. Si rahisi kiivyo unavyoshauri mtoa maada ingawa pia inawezekana maana hakuna lisilowezeka. Asante kwa ushauri mzuri kiongozi
 
Aksante kwa mawazo chanya, shida ni vitendo ni vigumu kuliko nadharia.

kusema ni rahisi kuliko kutenda. Si rahisi kiivyo unavyoshauri mtoa maada ingawa pia inawezekana maana hakuna lisilowezeka. Asante kwa ushauri mzuri kiongozi

Yawezekana ikaonekana ningumu kama mnavyoona hii nadhani kutokana na kuenzi mila na desturi za nyakati hizo.
Pia ieleweke kuwa ninachozungumzia nijinsi tunavyotakiwa kuwa.
Mimi niko kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 10 kutokuelewana kupo ila njia hii ndiyo tunaitumia napenda hata wenzangu waishi katika upendo na wenza wao nahii naizungumza kwa dhati.Ndoa nikufundishana hakuna mwenyeji wa ndoa.
 
Umesomeka But Hakuna Mwalimu Wa Ndoa! Labda Mmoja Wa Wanandoa Akubali Kuwa B,w,e,g.e

Sikubaliani na wewe kuwa hakuna mwalimu, pia sikubaliani na wewe eti mmoja ajifanye ----- Huo niutumwa ndani ya ndoa. Hii ndiyo jambo nataka lifutike kwenye vichwa vya wanandoa wenye kuheshimiana
 
Back
Top Bottom