Fanya haya uepuke kuchunwa...

Fanya haya uepuke kuchunwa...

Phlagiey

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2013
Posts
3,499
Reaction score
1,687
Naongea na wale ambao tayari wamesha jitegemea kimaisha, ambao hawaishi na wazazi wao, wanaokumbana na mkono wa Mama/Baba mwenye nyumba kila baada ya miezi sita mitatu au mwaka..

Wanaoishi ki-bachelor lakini wana wapenzi.

Katika hii movie ya ki-bachelor tunakumbana na mengi sana,,kuna wanaogeuza ma girl friend zao kuwafanya kama mke,,tabia ya aina hii imepelekea na wao kugeuzwa kama waume,,hapa unakuta kila kitu girlfriend anakutegemea wewe akipata kashida kidogo ooohh baby nataka hela..

Mazingira ya kuchunwa tunayatengeneza wenyewe usianze kumhisi binti wawatu ni mchwa,,jichunguze kwanza na wewe kinachofanya akunyoshee mkono.

Ukiweza kuyamudu mambo yaha hakika hautayachukia maisha ya ki-bachelor na kumgeuza girl friend kuwa mke, na yeye pia atashindwa kupata ujasiri wa kukutegemea kiasi fulani labda tu kama nitabia yake..

1. Kujipikia
2. Kufua
3. Usafi wa vyombo.
4. Usafi wa chumba.

Ukiweza kukabiliana na hayo pasipo kutegemea msaada kutoka kwa girl wako utayafurahia sana maisha ya ki-bachelor,,na swala la kuoa kwako utaliamua kwa wakati muafaka, ila sio kwa kuwa unahitaji msaidizi.

Ebu fikiria labda girlfriend wako anakuja kukusalimia siku ya mapumziko, anakuta chumba chako umesafisha vizuri vyombo viko katika mpangilio mzuri,,umefua nguo zako na mashuka,,huku na huku haujachoka kuna akiba ya mchele,,unawasha kajiko kako unapikia wali na unaandaa mboga yani kila kitu unaweka sawa kisha unapakua kwenye hotpot yako, basi akija mnakula kama atapenda,,baada ya chakula mnaendelea na mambo yenu,,kusanya vyombo vyako akiondoka unaviosha.

Kumbuka kufanya hivyo hakuondoi uanaume wako,,jifunze kudhamini vitu vyako girlfriend hajawahi kukununua hata kijiko vyote umenunua kwa pesa yako,,ulio itolea jasho kwa kugombania daladala asubuhi uwahi kazini.

Hapo unajaribu kutengeneza mazingira ya kumfanya asijihisi unamtegemea sana zaidi ya kitu kimoja tu nadhani unakijua kwa wale mabachelor ambao mnamiliki kiwanja cha fundi selemara chumbani kwako.

Kama bachelor mwenye akili zako timamu lazima uishi kwa malengo ukijua kesho na wewe utakuwa na familia itaishi vipi kama ukiendekeza kuhonga katika ubachelor wako.

Ishi na mwanamke kwa kanuni kama unavyo fanya hesabu,,baada ya hayo kinachofuatia hakikisha unatumia kiasi kidogo sana cha pesa kumnunulia vitu vidogo vidogo ambavyo havina gharama,,ili mkusahaulisha kiasi fulani auone uwepo wako.

Ila kama wewe sio muoga kama mimi basi unamkazia kabisa,,maana demu nae akishajua unapenda pochi manyoya yake basi atakubabaishia,,,usiwe mtumwa wa pochi manyoya.

Kwa style hiyo binti unasababu ya kumtegemea boy wako???

Na wewe bachelor mwenzangu hapo bado unayo sababu ya kugeuzwa kitega uchumi?????

Haya karibuni kwa michango yenu.........
 
Najipikia, namlipa mtu wa kunifanyia usafi. Senior bachelor raha but dah sometimes I feel like I need one

||"You were too young to understand"||
 
Safi sana mkuu,madem siku hizi ni zaidi ya mchwa!sijui tuweke sumu gani!maana inakera kweli.
 
jembe afrika siungi mkono hoja wengine sie kuchunwa ni hobby nikiwa na mpenzi asiniombe chochote naweza kuugua hadi kulazwa na drip juu
 
mshana jr umenichekesha sana!inaonekana wewe mambo safi,kwamba usipochunwa unaugua.ha ha haaaa,hayo ni maneno tu,nyie ndo wale mkiguswa tu kuchunwa mnaruka futi mia.
 
mpe demu anachotaka apewe na nani si wako we huwajui utachapiwa mchana kweupe wameumbwa kupewa na kuzaa umenieeleewa
 
jembe afrika siungi mkono hoja wengine sie kuchunwa ni hobby nikiwa na mpenzi asiniombe chochote naweza kuugua hadi kulazwa na drip juu

Mshana anasumbuliwa na kutojiamini kuwa bila kuhonga awezi kumiliki kitu......
 
khaaa mi cfanyi hata kimojawapo na anatoa hela vizuru tu
 
jembe afrika siungi mkono hoja wengine sie kuchunwa ni hobby nikiwa na mpenzi asiniombe chochote naweza kuugua hadi kulazwa na drip juu

Mbona mitaa ya kwetu wanaume kama hawa hawapitagi?
 
Na huyo mwanamke atakaye kubali nioshe na nipakue chakula mbele yake huyo hafai kuwa MKE.....

umeona eeeeh bila kuambiwa atasema bby acha nitakusaidia
lakini ukiona unapika na girl wako kakutumbulia mimacho anasubiri kiive jiulize mara mbili
 
naongea na wale ambao tayari wamesha jitegemea kimaisha, ambao hawaishi na wazazi wao, wanaokumbana na mkono wa mama/baba mwenye nyumba kila baada ya miezi sita mitatu au mwaka..

Wanaoishi ki-bachelor lakini wana wapenzi.

Katika hii movie ya ki-bachelor tunakumbana na mengi sana,,kuna wanaogeuza ma girl friend zao kuwafanya kama mke,,tabia ya aina hii imepelekea na wao kugeuzwa kama waume,,hapa unakuta kila kitu girlfriend anakutegemea wewe akipata kashida kidogo ooohh baby nataka hela..

Mazingira ya kuchunwa tunayatengeneza wenyewe usianze kumhisi binti wawatu ni mchwa,,jichunguze kwanza na wewe kinachofanya akunyoshee mkono.

Ukiweza kuyamudu mambo yaha hakika hautayachukia maisha ya ki-bachelor na kumgeuza girl friend kuwa mke, na yeye pia atashindwa kupata ujasiri wa kukutegemea kiasi fulani labda tu kama nitabia yake..

1. Kujipikia
2. Kufua
3. Usafi wa vyombo.
4. Usafi wa chumba.

Ukiweza kukabiliana na hayo pasipo kutegemea msaada kutoka kwa girl wako utayafurahia sana maisha ya ki-bachelor,,na swala la kuoa kwako utaliamua kwa wakati muafaka, ila sio kwa kuwa unahitaji msaidizi.

Ebu fikiria labda girlfriend wako anakuja kukusalimia siku ya mapumziko, anakuta chumba chako umesafisha vizuri vyombo viko katika mpangilio mzuri,,umefua nguo zako na mashuka,,huku na huku haujachoka kuna akiba ya mchele,,unawasha kajiko kako unapikia wali na unaandaa mboga yani kila kitu unaweka sawa kisha unapakua kwenye hotpot yako, basi akija mnakula kama atapenda,,baada ya chakula mnaendelea na mambo yenu,,kusanya vyombo vyako akiondoka unaviosha.

Kumbuka kufanya hivyo hakuondoi uanaume wako,,jifunze kudhamini vitu vyako girlfriend hajawahi kukununua hata kijiko vyote umenunua kwa pesa yako,,ulio itolea jasho kwa kugombania daladala asubuhi uwahi kazini.

Hapo unajaribu kutengeneza mazingira ya kumfanya asijihisi unamtegemea sana zaidi ya kitu kimoja tu nadhani unakijua kwa wale mabachelor ambao mnamiliki kiwanja cha fundi selemara chumbani kwako.

Kama bachelor mwenye akili zako timamu lazima uishi kwa malengo ukijua kesho na wewe utakuwa na familia itaishi vipi kama ukiendekeza kuhonga katika ubachelor wako.

Ishi na mwanamke kwa kanuni kama unavyo fanya hesabu,,baada ya hayo kinachofuatia hakikisha unatumia kiasi kidogo sana cha pesa kumnunulia vitu vidogo vidogo ambavyo havina gharama,,ili mkusahaulisha kiasi fulani auone uwepo wako.

Ila kama wewe sio muoga kama mimi basi unamkazia kabisa,,maana demu nae akishajua unapenda pochi manyoya yake basi atakubabaishia,,,usiwe mtumwa wa pochi manyoya.

Kwa style hiyo binti unasababu ya kumtegemea boy wako???

Na wewe bachelor mwenzangu hapo bado unayo sababu ya kugeuzwa kitega uchumi?????

Haya karibuni kwa michango yenu.........

kaka ahsante sana
 
jembe afrika siungi mkono hoja wengine sie kuchunwa ni hobby nikiwa na mpenzi asiniombe chochote naweza kuugua hadi kulazwa na drip juu

hahahaha umeona eeeeh uwe na mpenzi hata vocha hakuombi jua unachapiwa
 
Hapa nakaa pembeni nasoma comments

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom