Fani gani itakuwa na soko 2o21? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fani gani itakuwa na soko 2o21?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Tyegelo, Aug 7, 2012.

 1. T

  Tyegelo Member

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi ni kijana wa kidato cha pili. Ninayamudu karibu masomo yote. Mwaka kesho nitalazimika kuyaacha masomo ya biashara au ya sayansi. Ninategemea kuhitimu chuo kikuu mwaka 2021, ninaomba ushauri kutoka kwa waona mbali, nifani gani itakuwa na soko mwaka 2021?
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kilimo kitakuwa kinalipa sana nyakati hizo, tena kilimo hai.
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,404
  Trophy Points: 280
  Ukitaka JF i-shine basi Nyimamadogookumanga eheee,Nyimamadogookumanga!!
   
 4. B

  Babuu Rogger JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 80
  Muombe Mwenyezi Mungu kila uionapo kesho, Hauna mkataba na Mwenyezi Mungu.
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,404
  Trophy Points: 280
  Sasa ni Mwaka 2012 mpaka 2021 ni karibia miaka 9 kutoka sasa,ili nikujibu vizuri ebu turudi miaka 9 nyuma yani mwaka 2003,Je tujiulize mwaka 2003 fani gani ilikua juu? Je kwa sasa hyo fani bado ipo juu? Kipindi hicho yani kila mtu alikua anataka kusoma eng tena ECSE(CIT,TE,ELectrical) lkn sasa je hao wataalamu waliosoma hayo masomo wanafanya nin kwa sasa? Nakushauri Soma kilimo au Maswala ya Ardhi(Archtech/Planing/Env Eng) hayo ndio yatakuwa na soko sana 2021.
   
 6. faabroz

  faabroz JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 291
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mungu akutanguliye kwani yeye ndo aliyekupa uwezo wa kupumua, muombe mungu kama kupata mke ni sawa nahiyo fani yako.
   
 7. Voice of Wisdom

  Voice of Wisdom JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 541
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  kwanza hongera kwa hayo mawazo maana ni wachache wanawazo hivyo. ni shida kumwelekeza mtu anapotaka kwenda kama hujia anaenda wapi? Kitu cha kwanza cha kufahamu toka kwako mtoto(sio kijana wewe kila aliyeko chini ya 18 ni mtoto, na 4m two wa leo wakizidi sana ni 15) kabla ya kukushauri ni
  je ni unataka kuwa na fani gani hapa baadaye?
  Kwa nini unataka kuwa hivyo?
  Baada ya wadau kujua hayo mawili hapo juu, kulingana na uzoefu walio nao hakika utapata ushauri mzuri wa kukusaidia. Hii ni kwa sababu hapa ushauri utakaoupata utakuwa wa jumla na unaweza usikidhi haja yako(your interest) kwa sababu sio kila dawa inatibu ugonjwa wowote, ila dawa maalum kwa ugonjwa maalum.
  Huu ni mtazamo wa VOW na si sheria.
   
 8. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,189
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Sasa hata kama hana uhakika wa maisha ndio asijiwekee malengo?
   
 9. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,189
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Sasa hata kama hana uhakika wa maisha ndio asijiwekee malengo?
   
 10. Bundewe

  Bundewe JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Siasa itaendelea kutesa miaka hiyo. Ila ningekushauri mdogo wangu Soma kozi unayoipenda, achana na mambo ya soko kwa sasa.
   
 11. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Masomo ya sayansi na biashara yanalipa ila ya sayansi yanalipa zaidi kwa sababu zifuatazo:

  - Ukosoma marketing mara nyingi wenye kampuni binafsi wanatafuta masoko wenyewe kwa njia wanazozijua hivyo ajira za marketing na kampuni kubwa na sekta ya umma;

  - Ukisoma uhasibu hawa wanachukuliwa kama "supporting department" ingawaje wanahitajika kwa wingi ujira wao bado siyo mkubwa sana;

  - Ukisoma general management - mahitaji ya soko ni machache ukilinganisha na fani nyingine.

  - Ukisoma course za sayansi huko baada utatambulika na kupata ujira mkubwa ila inahitaji moyo, gharama na kujituma sana. Kama huna "support" unaweza usifike mwisho wa safari yako.

  Ushauri

  - Kama una "financial support" chukua masomo ya sayansi

  - Kama unahisi huna "support" ya kukuwezesha kufika safari yako; chukua masomo ya biashara kwani kuna short -cut nyingi za kujiendeleza mwenyewe hata kama utakosa uwezo wa kujiunga na chuo kikuu
   
 12. c

  chrisnyoni Member

  #12
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nenda mbele rud nyuma dogo kazana na Masomo ya science hasa PCB then utasoma coz yeyote ya afya dogo iyo itakutoa sana tunavozid kwenda watu wanajali afya zao 99% ya watu ote wanaogopa kifo so dogo kaba hapo hapo kwe uoga wao all the best
   
 13. m

  markj JF-Expert Member

  #13
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Mpira wa wanawake!
   
 14. T

  Tyegelo Member

  #14
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maneno gani sasa hayo? Niache kupanga mambo yajayo kwa kuwa kuna kufa? Je nisipokufa? Ndio maana nchi hii haiendelei watu hawafikirii miaka 20 ijayo, wanawaza leo tu!
   
 15. T

  Tyegelo Member

  #15
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nataka fani itakayolipa na kunifanya niishi vizuri, mi siipendi fani kwa ajili yake, naipenda fani kwa ajili ya kipato itakachonipatia.
   
 16. T

  Tsidekenu Senior Member

  #16
  Aug 8, 2012
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 141
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Kuna shortage kubwa sana ya Forensic Accountants in Tanzania.This is a sub aspect in accounting proffesion which because of a lot of emmbezzlement in Tanzania many international projects and big offices needs accountants specialized in this.Since our government is remotely controlled by these international donors,I am seing this as a requirement in government offices as well. It is unfortunate however that there is no college or university in Tanzania that provide a specific degree in forensic accounting.
   
 17. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #17
  Aug 8, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,169
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  electronics engineering
   
 18. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Tyegelo
  Ukijifunza jinsi ya kutengeneza software mbalimbali za computer including computer games utakuwa tajiri mapema sana. Hii ndio field itakayokuwa inalipa zaidi mwaka 2021.

  Kilimo kinaweza kuwa kinalipa kwa sasa, lakini tambua kuwa mwaka 2021 kupata heka moja tu ya ardhi itakuwa balaa!!! Vilevile kilimo unahitaji kuajiri watu wengi, kakati kwenye software industry huhitaji kununua ardhi wala kuajiri watu.

  Fani nyingine ambayo itakuwa inalipa mwaka 2021 ni sheria. Kadri wananchi wanavyozitambua haki zao, wanakuwa na sababu zaidi ya kuzidai haki hizo mahakamani na umuhimu wa wanasheria unaongezeka. Mfumuko wa wajasiriamali na wawekezaji unaenda sambamba na mahitaji ya wanasheria. Kila kampuni inahitaji mwanasheria na kila inapotokea mzozo baina ya kampuni hizo wanasheria wanahitajika. Ukichagua fani ya sheria somea business law, utatoka.

  Kama una uvumilivu wa kusubiri miaka mingi kabla "hujatoka" somea udaktari. Hii ni fani ambayo kutoka kuko guaranteed, lakini ni lazima uwe mvumilivu. Unahitajika kujifunza vitu kwa muda mrefu na kuwa specialist mzoefu. Baada ya hapo una uhakika wa constant flow of cash mpaka uzeeni. Katika medicine somea upasuaji. Ukiweza kufanya operations vizuri watu watakufuata hata miles 2000 kupata huduma yako kwa gharama utakayotaka wewe.

  Wakati niko form two Mzumbe Sekondari, mwalimu mkuu msaidizi Mr. Kidua aliniambia "nikikuangalia umri wako nakumbuka enzi zangu, nilikuwa na uwezo wa kuchagua chochote ninachotaka lakini sikutambua hilo. Wewe fanya maamuzi sahihi, unaweza kuwa chochote unachotaka sasa hivi, lakini umri unavyozidi kwenda huwezi kurudi nyuma na kuchagua kingine". Kauli yake hii naikumbuka kwa sababu ilinisaidia kufanya maamuzi. Nimechagua field ambayo mpaka sasa nashukuru Mungu kuichagua. Nakutakia kila la heri na wewe katika hatua mbalimbali utakazopitia.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. m

  mkizungo JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 247
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jeshi,,,huon tishio la malawi hiyo ndiyo shule na ajira ya kishujaa,,watapiga domo weeee mwisho ngondo wanaume kazini,,hamna zcha igondi,,,kova ,,msangi wala magwepande,,au,,kujinyonga bila kutapatapa huko morogor,,,kaza buti dogo,,,,,,,
   
 20. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #20
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,738
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hongera mdogo wangu! Kutokana na mabadiliko ya kiuchumi, nakushauri, usome masomo ya sayansi. Ukifika chuo, soma fani zinazohusiana na huduma kama vile kutengeneza software, kutoa huduma za afya, n.k. Uchumi wa sasa unategemea huduma kwa kiasi kikubwa, jaribu kuangalia mapinduzi yaliyoletwa hapa Tanzania; kwa sasa watu wanatumia simu kama benki, pia ukiwa na uwezo mzuri unaweza kufanya kazi popote pale duniani, vile vile kwenye sekta ya huduma hakuhitaji uwe na mtaji, mtaji ni akili yako.
   
Loading...