Family Photo

hadithi-ya-daudi-na-raza-pic-by-f-macha-e1307496913839.jpg
Inanikumbusha Mbaliiiiiiiiiiiiiiiiiiii! Safi Sana Mr Daudi

Wanaonekana a very happy family... Inapendeza kwa kweli....

Nimekumbuka kisa kimoja: Roza alikutana na rafiki yake Lucy; Mazungumzo yao yalikuwa hivi:

Lucy; Roza umefika Dar es salaam?

Roza: la sijapata kwenda, mjomba ameniambia Ijumaa nitakwenda naye Dar es salaam

Lucy: Basi ngoja nikuelezee. Dar es Salaam ni mji mkubwa sana, hakuna simba wala wanyama wakali kama huku kwetu.

Roza: Kuna nini zaidi

Lucy: Zipo nyumba ndefu na kubwa, magari, meli na magari ya moshi, pia maduka ni mengi.

Roza: Basi usiniambie mengi, nitakwenda kuona mwenyewe.

Lucy: Kwaheri Roza, msalimie kaka yako Juma na Rafiki yake Damasi.
Mkuu wewe ni Mkareeee

Vitabu vya Long Time Baadhi unaweza kwenda pale Dar Es Salaam Book Shop Karibu na Mnara wa Askari Makunganya Street, Utavipata
Maktaba ya Taifa Sijui vipi Sijatia Mguu Miakaz Mingiz

Enzi hizo familia yetu wote walikuwa ni wana ccm tulikuwa tunatoa michango yote.
Nakumbuka nilirudishwa shule ili nikalete sh kumi za jengo la chimwaga.
Najivunia kuchangia udom

Kwa kweli zile zilikuwa enzi za neema na raha...ukienda shule unapewa daftari na mkebe wa bati ule kutoka Tanzania Elimu Supplies (TES). Kuna kitabu cha kiswahili nadhani title yake ilikuwa Lugha Yetu ndani kuna hadithi ya "Sungura Sizitaki mbichi hizi", Hadithi ya yule baba aliyesafiri akatungiwa na shairi maarufu "karudi baba mmoja toka safari ya mbali kavimba yote mapaja na kutetemeka mwili, watoto wake wakaja ili kumtaka hali, wakataka na kauli iwafae maishani......mengine sikumbuki". Pia kitabu cha English nadhani darasa la Sita cha oxford kulikuwa na hadithi ya mjamaa anaitwa Abdul mle na mfalme". I wish ningepata vile vitabu niwaongezee watoto wangu katika maktaba yao....

then Mwalimu jana kwa uzembe tu hakuita majina ..............leo anaita na kama jana ulikuwepo unatakiwa kuitika "jana na leo" na tulikuwa wakweli .......Ndaki Ndaki niliiitika Jana na Leo.

then anaanza kufundisha, tunaimba ukurasa mzima.

"HUYU NI BABA, BABA ANA NG'OMBE WAKE, NG'OMBE WAKE NI MWEUSI, BABA ANASEMA, KIMBIA NG'OMBE, KIMBIA UPESI, KIMBIA NYUMBANI, BABA ANA NJAA" mwisho wa passage.

JUMA NA ROZA, DAMAS NA RUTH, SAFARI YA BURCHEKA NA MKE WAKE LIZABETA ...............................Mzee wewe ni mkali!

Niazimeni kitabu cha juma na roza wandugu, tumetoka mbali wajemeni wacha tu, machumvu tumeyabugiaga!!

Kitabu cha Juma na Roza mii nnacho pamoja na kile Bulicheka alivyokutana na mfalme Huihui wa Wagagagigikoko. Umenihuzunisha kwasababu nimekumbuka jambo baya ambalo ni hili. ZIDUMU FIKRA SAHIHI ZA MWENYEKITI, SHIKAMOO MWAAAALIMU.
na hii hapa ndo nikikumbuka najiona **** xana NAAPA NAAHIDI MBELE YA CHAMA, MAPINDUZI NITAKULINDA MPAKA KUFAA!

nilipoiona nimekumbuka kweli nimetoka mbali ktk safari ya elimu mwalimu wa chekechea mpaka std2 si wakuzarau

daaa! natamani sana turejelee zama zile! nakaribisha hadith zetu zilleeeee za .....karudu baba mmoja........etc

then Mwalimu jana kwa uzembe tu hakuita majina ..............leo anaita na kama jana ulikuwepo unatakiwa kuitika "jana na leo" na tulikuwa wakweli .......Ndaki Ndaki niliiitika Jana na Leo.

then anaanza kufundisha, tunaimba ukurasa mzima.

"HUYU NI BABA, BABA ANA NG'OMBE WAKE, NG'OMBE WAKE NI MWEUSI, BABA ANASEMA, KIMBIA NG'OMBE, KIMBIA UPESI, KIMBIA NYUMBANI, BABA ANA NJAA" mwisho wa passage.

JUMA NA ROZA, DAMAS NA RUTH, SAFARI YA BURCHEKA NA MKE WAKE LIZABETA ...............................Mzee wewe ni mkali!

Aisee umenikumbusha mbali sana. Duuuuu, enzi hizo jamani dunia ilikuwa mahali pazuri pa kuishi. Hakuna ukimwi, kuchakachua wala magamba. Natamani enzi zile zirudi.

Afu darasa la pili kulikuwa na kitabu cha kusoma, hadithi ya Kwanzanza ilikuwa hivi,
Mimi ni Mariam, mwanzo wa mwaka huu nilianza shule.
Na hadithinnyingine ya Chopeko na mnofu, na mpapai na upepo hadi ukavunjika.

Similar Discussions

Back
Top Bottom