Nimekumbuka kisa kimoja: Roza alikutana na rafiki yake Lucy; Mazungumzo yao yalikuwa hivi:
Lucy; Roza umefika Dar es salaam?
Roza: la sijapata kwenda, mjomba ameniambia Ijumaa nitakwenda naye Dar es salaam
Lucy: Basi ngoja nikuelezee. Dar es Salaam ni mji mkubwa sana, hakuna simba wala wanyama wakali kama huku kwetu.
Roza: Kuna nini zaidi
Lucy: Zipo nyumba ndefu na kubwa, magari, meli na magari ya moshi, pia maduka ni mengi.
Roza: Basi usiniambie mengi, nitakwenda kuona mwenyewe.
Lucy: Kwaheri Roza, msalimie kaka yako Juma na Rafiki yake Damasi.