Familia ya Wema, Diamond wapiga kambi polisi Dar kujua hatima ya watoto wao

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
SAKATA la baadhi ya wasanii wakubwa nchini kuhusishwa na biashara ya dawa za kulevya limezidi kuchukua sura mpya, huku wazazi wa Wema Sepetu na Nassib Abdul ‘Diamond’ wakikutana polisi kujua hatima ya watoto wao.

Wazazi hao wa wasanii hao tangu juzi wamekuwa wakishinda Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaaam baada ya Jeshi la Polisi kuwaita wasanii hao kwa mahojiano na kisha kuwaweka ndani.

Wakizungumza na MTANZANIA jana kituoni hapo wanafamilia hao walisema kwa sasa imekuwa ngumu kukaa kwenye nyumba zao bila kujua hatima ya watoto hao ambao hadi sasa wanashikiliwa na polisi.

Akizungumza huku akiwa kama mtu aliyepatwa na hamaki mama mzazi wa Wema Sepetu, alisema kwa sasa anasubiri kauli ya Polisi ili aweze kujua kama mtoto wake atafikishwa mahakamani au laa.

Alisema kitendo cha kukamatwa mtoto wake na kuwekwa ndani kimemuumiza kama mzazi ingawa kwa sasa hana la kufanya zaidi ya kusubiri uamuzi wa vyombo vya dola.

“Kama mzazi nimeumia sana ila kwa sasa ninawaomba mniache maana siwezi kuongea kitu chochote kuhusu hili, hadi hapo polisi itakapotoa maamuzi yao ya uchunguzi wanaoufanya, ndiyo nitajua nini niseme,” alisema mama Wema

Baada ya kutoa kauli hiyo mama huyo alionekana ni mtu mwenye msongo ambapo muda wote alikuwa amekaa kimya tofauti na ilivyo kawaida yake ambapo huwa ni mtu mwenye ucheshi.

MAMA DIAMOND

Wakati timu ya MTANZANIA inawasili kituoni hapo, mama Diamond, baada ya kuona waandishi wa gazeti hili walikimbilia ndani ya gari na hata alipofuatwa ili kuzungumza naye aligoma kufanya hivyo.

“Jamani kwa sasa sipo tayari kuongea chochote kile,” alisema mama huyo huku akipandisha kioo cha gari.

Baada ya mama Diamond kugoma kuzungumza alijitokeza dada wa mwanamuziki huyo, Esma Kandili ambaye ni mke wa msanii Ahmed Ngahemela maarufu kwa jina la ‘Petit Man’

“Mume wangu amekutwa na balaa hili tangu Februari 2, mwaaka huu ambapo ilikuwa siku ya kumbukumbu yangu ya kuzaliwa ni kitu ambacho sitakisahau katika maisha yangu kimeniumiza sana kuliko ambavyo watu wanadhani.

“Naumia na ninazidi kuumia kuona taarifa za uongo zinasambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikimuhusisha na mdogo wangu Nassib, jamani watu wawe na huruma kwani sisi ni binadamu kama wao kila siku sisi wanatuombea mabaya yatukute kwenye familia yetu,” alisema.

Wazazi wa TID

Nao wazazi wa Khaleed Mohamed ‘TID’, walikuwepo kituoni hapo ambapo walikuwa wameandamana na familia ya Wema na Petit man, wakiwemo kaka zake wawili na mama yake mzazi ambao walionekana wako kwenye huzuni hawakutaka kuongea chochote kile na kusubiri hatima ya ndugu yao.

BABU TALE

Kutokana na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii taarifa za kuitwa polisi mwanamuziki Diamond, MTANZANIA ilimtafuta meneja wa mwanamuziki huyo, Hamis Taletale maarufu kama Babu Tale, ili kupata ufafanuzi wa kwa nini anatajwa na hata kuzushiwa Diamond na dawa za kulevya.

“Taarifa hizo si za kweli hazijakamilika kwa kifupi Kampuni ya Wasafi imeshazoea kuzushiwa habari za uongo. Nawaomba mashabiki wa WCB wawe na amani na sisi, hatuhusiki na biashara hiyo (dawa za kulevya) ila wasiotutakia mema ndiyo kila kukicha wanazusha ili kutupoteza kwenye ramani lakini watashindwa,” alisema Babu Tale.

VANESSA, TUNDA POLISI LEO

Mbali na wasanii hao mwishoni mwa wiki iliyopita Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliwataka wasanii Vaness Mdee pamoja na Tunda wajisalimishe polisi leo (Jumatatu) kwa mahojiano kuhusu tuhuma dhidi yao kushiriki biashara ya dawa za kulevya.

MTANZANIA ilimtafuta msaa Vanessa Mdee, ili kuweza kujua kama atakwenda polisi leo au laa simu yake ya kiganjani iliita bila kupokewa.

Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa Vanessa kwa sasa yupo nchini Afrika Kusini akirekodi tamthilia ya Sugar.

NAPE ATAKA BUSARA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amesema busara inatakiwa kutumika wakati wa kuwachukulia hatua wasanii waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kwamba wanajihusisha na matumizi ya dawa za kulevya.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema pamoja na kwamba ni rahisi kuwatambua wasanii maarufu wanaojihusisha na dawa hizo, wasanii hao wasichukuliwe hatua kwa kutumia hisia.

“Kwanza nikiri tu kwamba, tatizo la matumizi ya dawa za kulevya ni kubwa na waathirika wakubwa wanaonekana kuwa ni wenye majina makubwa ingawa inawezekana kuna watumiaji wengi.

“Sisi kama wizara, suala hili tumekuwa tukilijadili na hata Serikali kwa upande wake imekuwa ikilijadili pia kwani hata wasanii kama Ray C tumewahi kuwapa fursa ya kupata matibabu ya kuacha dawa hizo.

“Sisi tunaunga mkono juhudi zozote zinazofanywa na Serikali za kupambana na jambo hilo kwa sababu lengo ni kuokoa wadau wetu. Pamoja na hayo, mjadala uliopo sasa ni namna tunavyoshughulika na waathirika, yaani tutawashitaki kwa sheria ipi wale waliowahi kuathirika na dawa hizo.

“La msingi hapa ni kutumia busara ya kushughulika na suala hili kwa sababu ni rahisi sana kutengeneza brand (alama) yako, lakini brand hiyo inaposhushwa kwa namna yoyote, inakuwa vigumu kuipandisha tena.

“Tusiwahukumu watu kwa hisia, lazima suala hili lishughulikiwe kwa kulinda haki za watuhumiwa ili ikithibitika hawahusiki na matumizi ya dawa hizo, iwe ni rahisi kwao kurejesha heshima yao,” alisema Nape.

NZOWA AMPONGEZA MAKONDA

Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi kitengo cha Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa amesifu jitihada zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda za kupambana na biashara ya dawa za kulevya huku akisisitiza kuwa yupo tayari kutoa ushauri pale utakapohitajika.

Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu jana akiwa wilayani Mbozi mkoani Songwe anakoendelea na shughuli za kilimo baada ya kustaafu, alisema jitihada hizo zinapaswa kuungwa mkono na watu wote wanaowatakia mema vijana wa nchi hii.

Kuhojiwa kwa wasanii hao kunatokana na orodha ya watu 50 iliyotangazwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Katika orodha hiyo alitaja watu wanaouza, kutumia pamoja na kuhusika na biashara ya mihadarati, wakiwamo vigogo wa Jeshi la polisi, wamiliki wa kumbi maarufu za starehe jijini Dar es Salaam na wafanyabishara wa dawa za kulevya.

Kwa upande wa jeshi la polisi, Makonda aliagiza aliyekuwa Kamanda Polisi Mkoa wa Kinondoni, Christopher Fuime, kukamatwa mara moja ili kuhojiwa kwa tuhuma hizo pamoja na askari 12 ambao tayari Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu, amewasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi dhidi yao.

Chanzo: Mtanzania
 
La msingi hapa ni kutumia busara ya kushughulika na suala hili kwa sababu ni rahisi sana kutengeneza brand (alama) yako, lakini brand hiyo inaposhushwa kwa namna yoyote, inakuwa vigumu kuipandisha tena.

“Tusiwahukumu watu kwa hisia, lazima suala hili lishughulikiwe kwa kulinda haki za watuhumiwa ili ikithibitika hawahusiki na matumizi ya dawa hizo, iwe ni rahisi kwao kurejesha heshima yao,
 
Hao ndugu nao ni wapungufu wa akili kweli kweli.....yan mtoto hana kazi yakueleweka lakini anamiliki pesa nyingi then mzazi unashindwa hata kuhoji anazipata vipi then siku anakuja kudakwa ndio unaanza kujiliza.....kama inawezekana na wao wawekwe ndani tu.
 
Hao wazazi wao ni wafaidika wa hizo hela za madawa ya kulevya.. ulitgemea nn? wasi support watoto wao..? Si wanakula hela hizo pamoja, pumbav kabisa
Tusiwahukumu watu kwa hisia, lazima suala hili lishughulikiwe kwa kulinda haki za watuhumiwa ili ikithibitika hawahusiki na matumizi ya dawa hizo, iwe ni rahisi kwao kurejesha heshima yao,
 
La msingi hapa ni kutumia busara ya kushughulika na suala hili kwa sababu ni rahisi sana kutengeneza brand (alama) yako, lakini brand hiyo inaposhushwa kwa namna yoyote, inakuwa vigumu kuipandisha tena.

“Tusiwahukumu watu kwa hisia, lazima suala hili lishughulikiwe kwa kulinda haki za watuhumiwa ili ikithibitika hawahusiki na matumizi ya dawa hizo, iwe ni rahisi kwao kurejesha heshima yao,

Jua hili vizuri ww uliye lala fofofoo na mdomo wako uko waziii na nzi wanakuingia

1: Hakuna busara ktk kupambana na madawa ya kulevya.. hawa ni watu hatari sana

2: Hakuna Brand inajengwa kwa madawa ya kulevya.. hakuna brand ya hela haramu, hakuna ndio maana uchunguzi unaendelea mkali, jua hakuna aliyehukumiwa.. ila Mh. RC na Polisi, hadi wakuite polisi wana habari zoooooote, kuwa unahusika kwa 100%, mbona wengi tu hawajaitwa..? so hadi uitwe polisi, wana full data unahusikaje na madawa ya kulevya..
 
Tusiwahukumu watu kwa hisia, lazima suala hili lishughulikiwe kwa kulinda haki za watuhumiwa ili ikithibitika hawahusiki na matumizi ya dawa hizo, iwe ni rahisi kwao kurejesha heshima yao,

Makenge yapo mengi humu, nani amehukumiwa..? Those are suspects.. na wako ktk uchunguzi mkali na polisi tayari wana data zao wanahusika vipi, ulifikiri wamewakamata tu..? na walio ndani wako ili wasiharibu uchunguzi..

Nani amehukumiwa, acha ujinga
 
Jua hili vizuri ww uliye lala fofofoo na mdomo wako uko waziii na nzi wanakuingia

1: Hakuna busara ktk kupambana na madawa ya kulevya.. hawa ni watu hatari sana

2: Hakuna Brand inajengwa kwa madawa ya kulevya.. hakuna brand ya hela haramu, hakuna ndio maana uchunguzi unaendelea mkali, jua hakuna aliyehukumiwa.. ila Mh. RC na Polisi, hadi wakuite polisi wana habari zoooooote, kuwa unahusika kwa 100%, mbona wengi tu hawajaitwa..? so hadi uitwe polisi, wana full data unahusikaje na madawa ya kulevya..

Yote yaweza kuwa sawa au yasiwe sawa. Wengine wataitwa ili kuongezea ushahidi. Mfano mtuhumiwa alikuwa mpenzi wako au rafiki yako wa karibu. Ndiyo maana kabla walioenda ijumaa tumeambiwa baadhi wako ndani. Idriss alikuwa mpenzi wa wema na wema wamemzuia ndani,diamond alikuwa pia mpenzi wa wema. Hivyo usijekushangaa wakaitwa hata watu ambao majina yao hayafahamiki
 
Mbona unapaniki ambacho Polisi wanatimiza wajibu wao baada ya kupewa maelekezo na Mkuu wa Mkoa Makonda sitoshangaa watuhumiwa kuachiwa huru kwa kukosekana ushahidi kutokana Makonda kukurupuka .Vita ya madawa ya kulevya hajaanza leo
Makenge yapo mengi humu, nani amehukumiwa..? Those are suspects.. na wako ktk uchunguzi mkali na polisi tayari wana data zao wanahusika vipi, ulifikiri wamewakamata tu..? na walio ndani wako ili wasiharibu uchunguzi..

Nani amehukumiwa, acha ujinga
 
Nimeumia sana kuona yule kada wetu mkuu Wema jamani alivyojitosa kwenye kampeni yetu na kuwavuta wengi, Je Dia wa mondi alivyoizunguka nchi. Halaf leo mmeamua kumdhalilisha?? Haya, tupo. Ukimuweka ndani 2020 tutatoka na nani??
 
Et wanaharbu Brand hehe brue band yenyewe huwa tunaiharbu sembuse Brand ha ha ha ha nacheka ki dharau kabsa fyeka ndani Wafanyabiashara halamu hao
 
Mbona unapaniki ambacho Polisi wanatimiza wajibu wao baada ya kupewa maelekezo na Mkuu wa Mkoa Makonda sitoshangaa watuhumiwa kuachiwa huru kwa kukosekana ushahidi kutokana Makonda kukurupuka .Vita ya madawa ya kulevya hajaanza leo

Umesema WANAHUKUMIWA.. acha kugeuza maneno hapa, sasa unasema watuhumiwa.. hata hujui unaongea nn, naongea na blind minded kabisa.. kwani ukiwa mtuhumiwa na baadae ukiachiwa huru unashangaa nn..? unashangaa ssbb akili yako ni kilaza.. being a suspect, na kisha baada ya investigation ukikutwa huhusiki, unaachwa huru, sasa unashangaa nn..? ni dead minded & arrogant atashangaa sbb hajui nn kinafanyika ktk utaratibu wa sheria..
 
Jua hili vizuri ww uliye lala fofofoo na mdomo wako uko waziii na nzi wanakuingia

1: Hakuna busara ktk kupambana na madawa ya kulevya.. hawa ni watu hatari sana

2: Hakuna Brand inajengwa kwa madawa ya kulevya.. hakuna brand ya hela haramu, hakuna ndio maana uchunguzi unaendelea mkali, jua hakuna aliyehukumiwa.. ila Mh. RC na Polisi, hadi wakuite polisi wana habari zoooooote, kuwa unahusika kwa 100%, mbona wengi tu hawajaitwa..? so hadi uitwe polisi, wana full data unahusikaje na madawa ya kulevya..
Hayo mawazo yako kutokana na uelewa wako kama ni kweli wangekuwa na ushahidi wangehojiwa na kupelekwa mahakamani .Vita ya madawa ya kulevya siyo rahisi kama Makonda anavyofikiria Jk akiwa raisi mpaka ameondoka alipewa majina wahusika alishindwa kuwakamata wahusika Makonda anatafuta sifa kupitia wasanii akina Chid Benz, TID na Wema Sepetu .tusubiri muda utaongea
 
Mbona unatokwa na povu sana?
Umesema WANAHUKUMIWA.. acha kugeuza maneno hapa, sasa unasema watuhumiwa.. hata hujui unaongea nn, naongea na blind minded kabisa.. kwani ukiwa mtuhumiwa na baadae ukiachiwa huru unashangaa nn..? unashangaa ssbb akili yako ni kilaza.. being a suspect, na kisha baada ya investigation ukikutwa huhusiki, unaachwa huru, sasa unashangaa nn..? ni dead minded & arrogant atashangaa sbb hajui nn kinafanyika ktk utaratibu wa sheria..
 
Mwenye uwezo wa kuthibitisha tuhuma za mwalifu ni mahakama siyo wewe wala Makonda wenu anajitafutia sifa

Wee kweli bado dark headed..!!

Mahakamani unapitia tokea wapi..? njia moja wapo is thru polisi.. ndio maana wako polisi, kama watuhumiwa, polisi wakiona baadhi wana kesi ya kujibu watafikishwa court, wakiona ambao hawana kesi ya kujibu watawaacha huru..

Unashangaa mtuhumiwa kuwa huru, hizo ni akili za mbuya unga.. drug addict ndio atashangaa mtuhumiwa kuachwa huru, ni jambo la kawaida sana
 
NZOWA AMPONGEZA MAKONDA........

SASA HYU NAPE YEYE ANATAKA BISARA GANI ITUMIKE HIVI MUUZAJI WA MADAWA ANAHITAJI BUSARA....HUYU JAMAA NI ZAIDI YA MNAFKI .......
MAKONDA KAZAAA UZIII BABA

OVA
 
Mbona unapaniki ambacho Polisi wanatimiza wajibu wao baada ya kupewa maelekezo na Mkuu wa Mkoa Makonda sitoshangaa watuhumiwa kuachiwa huru kwa kukosekana ushahidi kutokana Makonda kukurupuka .Vita ya madawa ya kulevya hajaanza leo
Na IGP nae kaambiwa na.RC?
 
Back
Top Bottom