Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 8,787
- 5,536
Abedi Pele enzi zake akaichezea timu ya Taifa ya Ghana aliwika vilivyo. Alicheza 9 na 10 naukumbuka wepesi wake na namna alivyowasumbua mabeki. Jina lake la kuzaliwa ni Abedi Ayew lakini mashabiki wakaona wamfananishe na Mfalme Pele mwenyewe.
Baada ya kustaafu soka watoto wake wawili wakaamua kufuata nyayo za Baba yao. Jordan na Andre wamecheza pale Uingereza kwa misimu kadhaa pia ni sehemu ya kikosi cha Ghana kinachoshiriki afcon mara kwa mara, wameirithi kaka aliyoifanya Baba yao na kila anayewaona anawapigia makofi.
Alikuwepo Profesa mmoja mwenyeji wa Kilimanjaro, aliaga dunia mwaka 2021 inasemekana alisumbuliwa na COVID19, alikuwa ni mtaalam wa magonjwa ya watoto, aliishi Mbezi Beach. Watoto wa profesa yule pia ni wataalam wa afya wameirithi kazi ya Baba yao na wanaziendeleza shughuli alizofanya mzazi wao kwa umahiri.
Sioni dhambi yoyote kwa mtu kuirithi fani ya Baba au Mama yake. Mara nyingi wanakua huku wakiwatazama wazazi wao kwa ukaribu. Wanajikuta wakitamani siku moja kupita njia zile zile za wazazi na ni vigumu wazazi kuwavunja moyo.
Sishangai kuiona Familia ya mstaafu Kikwete ikizama kwenye siasa. Ridhiwani amekua akimuona Baba yake majukwaani akishughulika na siasa za moja kwa moja. Mama Salma pia anao wito wa kisiasa wa moja kwa moja hivyo ni vigumu kwa mtoto wao kutoingiwa na hamu ya kuja kufanana na Baba yake mzazi.
Sioni dhambi yoyote ile kwa mtoto kurithi mapenzi ya kitu fulani kutoka kwa mzazi wake. Inategemea na uwezo wa mzazi kumshawishi mtoto wake kuamua kufanana nae, japo wapo wazazi wengi ambao humuacha mtoto wao awe huru katika kufanya analohisi linamfaa kulifanya maishani mwake.
Zipo familia zinapenda ualimu, Baba mpaka mtoto wa mwisho wanakuwa waalimu, hakuna dhambi yoyote ile maji kufuata mkondo.
Zipo familia zinapenda uanasayansi, Baba mpaka mtoto wa mwisho wote wanavaa majoho meupe wakiwa maabara, hakuna kosa lolote linalofanyika kwa wao kuamua kujikita katika fani hiyo.
Mfano Baba yangu ni mwanasheria mbobezi, kuna ubaya gani na mimi nikawa mwanasheria mbobezi?, ni kosa kufuata nyayo za Mzazi wangu?.
Kibaya ni pale ambapo nafasi ya Baba na Mtoto walio kwenye taaluma moja, inapotumika vibaya kwa maslahi binafsi na kuendekeza zile hulka zilizo kinyume na matarajio ya jamii inayowatazama. Kuiipenda fani ya mzazi mara nyingi ni tabia ambayo mtoto anafanya maamuzi baada ya kuhakikishiwa usalama wa kimaisha na mzazi huyo.
Kosa linakuwa pale Baba, Mama na watoto walio kwenye fani moja wanapokwenda kinyume kabisa na matakwa halisi ya fani hiyo na hivyo kuwakwaza wote wanaowaheshimu. Wanapojirahisisha na kukubali kuchafua majina yao kwa kuendekeza rushwa nyepesi na kuwakwaza wadau wanaotegemea kuona mema yakitoka kwao.
Familia zinakwenda bungeni kwa kasi na hili limekuwa likiwaudhi baadhi ya watu. Lakini hata kingekuwa ni chama kingine zaidi ya CCM kinatawala Tanzania sioni ni kwa namna gani viongozi wangeweza kukwepa ushawishi wa moja kwa moja kutoka kwa watu wenye kuwahusu kwa asilimia mia moja.
Maji hufuata mkondo siku zote.