Mapema kabisa hakikisha mke na yeyote aliye ndani ya himaya yako anatii na kufuata sheria ulizoweka. Kusiwe na majadiliano yoyote ili mradi humuonei mtu. Mke, mtoto, ndugu au mgeni aliye ndani ya nyumba yako afuate utaratibu. Kimsingi ukiwa BABA KATAA DEMOKRASIA NDANI YA FAMILIA. Udikteta ndo njia pekee ya kulinda kizazi chako kisiangamie.
Saa nyingine wasikilize wanachosema ila iwe kama maoni ambayo sio lazima kuyafanyia kazi. Familia inatakiwa i-fit kwenye mfumo wako. Kwa mfano toto halitaki kufanya kazi za nyumbani kama kudeki, kupiga pasi, nk anatakiwa akutane na hasira zako iwe fundisho kwake.