Kwanini CCM imshindwa kufanikisha programme yake ya kujivua gamba mara baada ya kuianzisha,programme iliyoaminiwa na wananchi pamoja na wanachama watiifu kuwa ingeleta heshima ndani ya chama na kutoa dhana kuwa CCM kichaka cha wahuni.Kushindwa kwa falsafa hii ya kujivua gamba kumedhihirisha udhaifu na ombwe la uongozi ndani ya nchi na CCM kwa ujumla.
Ikiwa M/KITI ana kiri kuwa rushwa imekigubika chama chake haitoshi kuishia kutoa kauli,nilitegemea angefanya maamuzi magumu na kufuta uchaguzi na kuivunja taasisi ya kuzuia rushwa kwa kushindwa kuwajibika.Haitaji elimu ya chuo kikuu kubaini rushwa ambayo imetolewa hadharani na kila mtu ana jua kilichofanyika.
Udhaifu wa M/kiti ambaye ndiye Amiri jeshi mkuu wa majeshi yetu kwa kushindwa kufanya maamuzi magumu ndiko kunakopelekea maadili ya uongozi wa umma kushuka na nidhamu ya uwajibikaji kupotea.Serikali itajivunia nini kuhusu kupinga rushwa ilihali viongozi wa chama kinachotawala wana patikana kwa misingi ya rushwa.
Kwa mantiki hii basi hakuna haja ya kuwa na TAKUKURU ikiwa imeonyesha udhaifu wa makusudi kwa kushindwa kuwajibika kama sheria na kanuni ilivyo waongoza.Aibu hii kwa serikali haitoshi kuitwa udhaifu bali ikibidi uwajibikaji wa pamoja wa kisiasa na kiutendaji ufanyike mara moja,hapo ndipo tutakapoamini serikali ya CCM inachukia rushwa kwa vitendo.Kuendele kugharamia uendeshaji wa TAKUKURU ni uhuni na uhujumu uchumi ambao unafanyika kwa misingi ya kuilinda taasisi hiyo kisheria.
Nachukua fursa hii kukaribisha michango mbali mbali tujadili ni kwa nini falsafa hii ya kujivua gamba imeshindwa na kuwafumba midomo wapiga debe wake na kuwaacha mayatima kwa KITENDO CHA M/KITI kuwageuka na kuiona falsafa hiyo kama adui wa kukiua chama,ilihali maamuzi hayo yaliafikiwa kwenye vikao halali vya CCM.NDUGU WAKUU WA BODI YETU NAWASILISHA KWA HESHIMA NA UTIIFU MADA HII ILI KUINUSURU NCHI YETU KUTOKANA NA JANGA HILI LA KITAIFA LA RUSHWA KUITAFUNA NCHI NA WASHEREHESHAJI WAKE KUACHIWA HIVI HIVI WAKIENDELEA KUMWAGILIA MAJI RUSHWA IZIDI KUSHIKA MIZIZI YAKE VIZURI