Falsafa ya kiti; Siri ya mchezo

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,343
Reaction score
859,902


unapoalikwa kwenye sherehe kaa kiti cha nyuma ili ukumbi ukishafurika waalikwa utafutwe kule uliko ufuatwe ushikwe mkono na kupelekwa siti ya mbele! Hii ni heshima pia ni sifa njema na ni hitaji muhimu la mwanadamu katika kudhihirisha thamani yako kwao

Ila kama ukialikwa kwenye karamu ukakuta viti havijajaa usikimbilie kukaa viti vya mbele, waepuke wanaokuhimiza kwenda kukaa huko, hawakutakii mema kwakuwa ukumbi utakapofurika waalikwa na ukafuatwa na kuambiwa hiki si kiti chako, twende kule nyuma tumeluandalia kule! Hii ni aibu, hii ni dhihaka na sifa hasi, wenye tafakuri wengi huliepuka hili

Habari za wiki hii zinasikitisha, zinakatisha tamaa hakuna msisimko ni habari mbaya kila kona...huu ni mwendelezo wa miezi na miezi wa kutibua na kuharibu kila kitu

Ni kilio kila kona kuwa uchumi unaporomoka, si kutoka kwetu sisi tuliopewa jina la wachochezi bali kwa washika dau na nguli wa biashara na uchumi
Biashara zinakufa, vitega uchumi vingi vinadorora, mali za pesa mingi zinauzwa kwa bei ya kutupa...nchi imeanza kuchechema na kuchechemea



hatuna habari njema tena za kujenga Taifa bali kila kinachosikika ni msiba wa kiuchumi biashara na kipato mahali fulani, ni habari za watu kutumbuliwa na kuswekwa ndani, ukiangalia kwa jicho la kiroho ni kama msiba mmoja mkubwa sana....tunapita katika bonde la uvuli wa mauti



kama ulikimbilia kukaa mbele wakakusifia ulikosea sana kuwaamini, kitambo si kirefu utashikwa mkono uonyeshwe kiti chako halisi....ni falsafa ya kiti usikarike ukatuharibia karamu
Tunachanja kuelekea mbugani....kamwe na kamwe milele na milele mchimba kaburi huingia mwenyewe

jifunze falsafa ya kiti, hii ndio siri ya mchezo
 
Uchumi wa Tanzania uko tete miaka yote.

Sasa la ajabu nini hapo?

Hata huo uchumi feki wa kifisadi nao ulikuwa ni tete vilevile.

Hakuna jipya hapo. Ndo uhalisia wenyewe.
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji115] [emoji115] [emoji115] [emoji115] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji144] [emoji144] [emoji144]
 
Hii picha imepigwa tawi gani na imepigwa lini/ saa ngapi?

Manake haya mambo ya mitandao bana...isije kuwa picha imepigwa kabla tawi halijafunguliwa au baada ya saa za kazi halafu watu mnataka kuaminisha watu mambo ambayo siyo.

Mi leo nimeenda CRDB pale Shamo Tower na watu walikuwa wengi tu kama ilivyo kawaida.

 
Hi je
 
Kwa hiyo watu walio wengi huenda benki kukopeshwa na kwa sababu hali ni tete ndo maana umeleta picha ya lobby iliyo tupu inayothibitisha utete wa uchumi?
Huu ni mtazamo kutokana na picha nilizoweka kama kiwakilishi kinachochagiza kile nilichoandika, nimeweka hizo na nyingine ila interest yako ikawa kwenye hizo
 
Yaani wewe kila jambo unakataa,jaribu kwenda na ualisia mambo yanavokwenda,utajificha kwenye kichaka cha tunanyoosha nchi mpaka lini?
 
Mbona niko mhalisia siku zote humu.

Uchumi wa Tanzania umekuwa tete siku zote.

Unabisha?
Watu walipenda kudai xana Rasilimali za tanzania sikuzote,lakini sasa hivi kilakona uchumi,uchumi,uchumiiiii,wakiulizwa wanajificha kwenye kichaka cha tunanyoosha nchi,tuambieni basi na siku ya mwisho kunyoosha tuwe na subira.
 
Mbona niko mhalisia siku zote humu.

Uchumi wa Tanzania umekuwa tete siku zote.

Unabisha?
Acha uongo ivi we ukidanganya unapata nn unataka sema hela ya ufisadi ile iliyokua kule uswiss imerudi toka lini ebu kua mkwel bana ata kama unalipwa nenda na we bank kapige yako uweke iwe ya mchana mda wa kazi ndo ubishe
 
tarehe kama hizi hiyo ndio hali halisi, japo najua ndugu zangu hawashindwi kusema ni photoshop [emoji144] [emoji144] [emoji144]
Hapo CRDB ni uchumi wa Kilimanjaro tu ndiyo utaathirika na si vinginevyo. Maana hata wakipunguza wafanyajazi ni watu wa Kilimanjaro ndiyo watapunguzwa kwa wingi maana ndiyo wengi. Ni zaidi ya asilimia 80 ya wafanyakazi wa CRDB. Acha wapunguzwe.
 
Hapo CRDB ni uchumi wa Kilimanjaro tu ndiyo utaathirika na si vinginevyo. Maana hata wakipunguza wafanyajazi ni watu wa Kilimanjaro ndiyo watapunguzwa kwa wingi maana ndiyo wengi. Ni zaidi ya asilimia 80 ya wafanyakazi wa CRDB. Acha wapunguzwe.
[emoji15] [emoji15] [emoji115] [emoji115] [emoji115] [emoji144] [emoji144] [emoji144] hapa ndipo tulipofikia kweli?![emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…