Fally Ipupa vs Ferre Gola.

Fally Ipupa vs Ferre Gola.

Nani mkali?


  • Total voters
    29

ZENITH

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2012
Posts
1,062
Reaction score
987
Kwa wale wenzangu wapenzi wa miziki ya lingala,naomba view zenu.Mimi binafsi ninawakubali sana hawa wasanii wote wawili kiasi ninashindwa kuamua yupi zaidi.Naomba mtazamo wako,nani mkali zaidi kati ya Fally na Ferre.
 
Mkuu hata mimi niemshindwa..................Vijana wote wawili ni wakali sana ila kidogo nimeegemea upande wa Ferre Golla Chalii anangoma Kali mbaya yani rhumba za ukweli.........Wacha kina The Romantic waone huu uzi watoe maoni yao nao ni wadau
Nina collection za kutosha za Ferre toka Wenge mpaka hapo alipofika.The Romantic alinifungua vya kutosha kabisa na kunifanya nimjue zaidi Ferre Golla
 
Kwa mtazamo wangu Fally Ipupa anafanya vizuri zaidi mziki wake uko contemporary na yuko flexible katika kuchanganya aina ya mziki wake na mingine ili kutoa ladha mbalimbali.
 
Mkuu hata mimi niemshindwa..................Vijana wote wawili ni wakali sana ila kidogo nimeegemea upande wa Ferre Golla Chalii anangoma Kali mbaya yani rhumba za ukweli.........Wacha kina The Romantic waone huu uzi watoe maoni yao nao ni wadau
Nina collection za kutosha za Ferre toka Wenge mpaka hapo alipofika.The Romantic alinifungua vya kutosha kabisa na kunifanya nimjue zaidi Ferre Golla
Yaani ni kwamba Ferre Gola katika mahadhi ya RnB anatisha mno lakini Fally katika RnB yupo kimtindo,ukimleta kwenye sebene anampoteza ferre gola ile mbaya.
 
Kwa mtazamo wangu Fally Ipupa anafanya vizuri zaidi mziki wake uko contemporary na yuko flexible katika kuchanganya aina ya mziki wake na mingine ili kutoa ladha mbalimbali.
kweli kabisa,Fally yupo flexible sana.
 
aaaah papa zenith mukulu mutu ya dyamaaa papa na daidaaaa umenifurahishagha sana juu ya hii kituu...aaaaghhh achana naye kabisa Falliii iko juu sana hata ukiskiza makereografa yake ni hatariiiii
 
Yaani ni kwamba Ferre Gola katika mahadhi ya RnB anatisha mno lakini Fally katika RnB yupo kimtindo,ukimleta kwenye sebene anampoteza ferre gola ile mbaya.
Mkuu Jaguar Nakubaliana na wewe Fally kwa Sebene yupo vizuri hilo halina ubishi................ila kwenye rhumba bado ntabaki kumtetea Ferre Golla..............Labda tuwatofautishe kwa aina ya Muzik wanaopigai
 
Fally Ipupa anamaliza...ng'ambo na ng'ambo anapiganisha...kufanya muziki watu waitike.
 
Y a pas match!
Fally is well marketed, he has a good producer and a perfect distribution channel, he is highly professional
Fere is an artist... he can compose, he can sing and he can dance. which is all we expect from an artist. Mengine ni soko tu.
to me they are beyond comparison kabisaaaaaa!
 
Last edited by a moderator:
bado cjamkubali ferre gola...



fally ni hatari.......
find new songs of "nyokalesse", 5me race, tsho tsho tsho, la jungle, french kiss....... ni balaaaaa


napenda mwanamziki anayeimba na kucheza......

FALLY IS MY CHRISS BROWN AND MY NYOSH AL-SADAAT
 
Inachanganya sana,sijui ni kwa sababu hawa ni wanafunzi wa mwalimu mmoja? i.e koffi charles anthony olomide.
 
Hii nitaifanya kama voting,mpaka sasa FALLY (7) VS GOLA(2).
 
Inachanganya sana,sijui ni kwa sababu hawa ni wanafunzi wa mwalimu mmoja? i.e koffi charles anthony olomide.

Ferre si mwanafunzi wa koffi bali alipitia tu kwa koffi tena kwa muda mfupi akiwa tayari maarufu,ferre ni mhitimu wa university of wenge musica bcbg 4x4 Tout Terrain a.k.a.wenge original iliyokamilika ya kina Papaa Cherie Salvatory de la Patria JB MPIANA a.k.a.Papaa na Daida,Le Roi De la Forret WERRASON,BLAIZE BULLA a.k.a.sele bulla,Le Big Tata ADOLPHE DOMINGUEZ,DIDIER MASELA na ALAIN "prince" MAKABA.Hawa kwa pamoja ndio waliompika FERRE GOLA,AIMELIA LYASE DEMIMGONGO,ALAIN MPELA "Afande",TUTU CALUDJI n.k.

Fally Ipupa De Caprio yeye kweli unaweza kusema ni mwanafunzi Le Rambow du Zaire Mopao Mokonzi Quadra Koraman KOFFI OLOMIDE a.k.a.Papaa na Didistone,kwanini basi tunasema fally ni mwanafunzi wa Koffi?Jibu ni kwamba Fally hakuwahi kufanya kazi katika bendi yeyote inayoeleweka zaidi ya QL ya koffi Olomide na toka anakua fally ndoto yake ilikua kuja kufanya kazi kwa koffi olomide na kudhihirisha hilo fally ambae alikua kwenye waiting list ya QL ya koffi olomide kwa muda mrefu kiasi kama angekua na roho ndogo angekata tamaa aliwahi kupata chance ya kufanya majaribio wenge maison mere ya kina WERRASON,ADOLPHE DOMINGUEZ na DIDIER MASELA mwanzoni kabisa wakati wanaisuka bendi hiyo baada ya kutengana na Kina JB MPIANA walioondoka na wanamuziki karibu wote kwenda kuunda wenge bcbg hii ya mpiana,kilichotokea ni kwamba Kina WERRASON na wenge yao maison mere(wenge makao makuu) waliitisha vijana wote wa congo wanaojiamini kuwa na vipaji mbalimbali vya muziki kuja kujaribiwa,miongoni mwa vijana waliojitokeza alikua ni huyu Ipupa Nsimba aka Fally Ipupa aka "DiCaprio" aka "La Merveille,ambaye alifanya vizuri sana kwenye mchujo wa uimbaji uliosimamiwa na majaji watatu FERRE GOLA ambae ndie mwanamuziki wakwanza kujiunga na maison merre kwa kuwa wenge original ilipogawanyika yeye alimfuata WERRASON,majaji wengine ukiacha FERRE walikua WERRASON na ADOLPHE DOMINGUEZ.

Baada ya FALLY kukubalika na majaji wote hao watatu baadae akafuatwa na WILLY BULA(Kaka wa Blaize Bulla wa wenge bcbg)ambae alikua ni kama kaka ya kina FALLY mtaani kwao na ambae alikua ni mwimbaji kwa KOFFI na pia refa muhimu wa FALLY aliekuwa akimpigia debe kwa KOFFI yeye FALLY na mtaalam mwingine BOURO MPELA(mdogo wake Alain Mpela kama mnaikumbuka album ya KOFFI altimutum kuna mtu mwishoni anacheza kwa kujikunja kama nyani).WILLY BULA ndio akamshika masikio Fally kwa kumwambia asiwe na haraka kujiunga na MAISON MERE kwani atapoteza chance kutimiza ndoto yake ya miaka mingi ya kujiunga na koffi,ndioa akampeleka kwa koffi ambae akakubali awe anakuja kufanya mazoezi na kushiriki local concerts za bendi ambapo kipaji chake cha kucheza kwanza ndio kilimkuna koffi kabla ya kuanza kupewa misingi ya uimbaji na koffi akishirikiana na kina SUZUKI 4X4 na wengine...huo ndio ukawa mwanzo wa safari ndefu ya FALLY ambae koffi anamuelezea kama ni kifaa kilichomuumiza sana baada ya kutimka.



 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom