FAKE NEWS: Chui aonekana jijini Dar es salaam

Status
Not open for further replies.
Jana nilikuwa nasikiliza redio moja maarufu hapa jijini. Walikuwa wakifanya mahojiano na wanawake kadhaa wanaoishi Goba kuhusiana na tukio la kuonekana kwa chui maeneo yale.

Kila mwanamke aliyehojiwa alisikika akishukuru uwepo wa chui kwenye eneo lao kwani eti sasa wanaume au waume zao wanarudi nyumbani mapema.

Ni dhahiri wanawake hawa wangependelea huyo chui aendelee kujivinjari maeneo hayo milele na ikiwezekana waongezeke chui wengine wengi zaidi ili kuwadhibiti "wanaume wa Goba".

Ama kweli Dar kuna mambo!!
 
Ila mawazo ya akina mama huwa yanatafakarisha sana.Ulipokuwa mtoto mama yako alisisitiza hadi kuwa mkali ili urudi nyumbani "kwenu" mapema.Na hata sasa umekuwa mtu mzima mkeo anataka uwe unawahi nyumbani "kwako"!Men,we are the prisoners of our own beloved ones!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom