Fake election

Fake election

Nina marafiki zangu wanyarwanda huwaambii kitu kwa Kagame, lakini mie nawapa za uso kwamba jamaa anaua wapinzani na pia kuua upinzani ili atawale milele. Huyu nina wasi wasi anaweza kuwa kama Mugabe au Museveni na kuishia kukaa madarakani kwa miongo mitatu au hata zaidi kama afya yake inaruhusu.
Jinsi walivyoibadili katiba jamaa sasahivi anaweza kukaa madarakani kwa miaka 22 kutoka leo
 
KAGAME+PIC.jpg

Ushindi wa kishindo! 98% kavuna!
 
Nina marafiki zangu wanyarwanda huwaambii kitu kwa Kagame, lakini mie nawapa za uso kwamba jamaa anaua wapinzani na pia kuua upinzani ili atawale milele. Huyu nina wasi wasi anaweza kuwa kama Mugabe au Museveni na kuishia kukaa madarakani kwa miongo mitatu au hata zaidi kama afya yake inaruhusu.
BAK ninasikia kile kiti ukishakikalia kukiacha ni vigumu sana
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wakae hata maisha lakini wafanye mazuri kwa wananchi wao na wanapokosea na raia na wapinzani wasikilize na wajirekebishe badala ya kutaka kuwaua. Huyu Kagame kishaua wapinzani wake wengi sana hadi ndani ya jeshi.

BAK ninasikia kile kiti ukishakikalia kukiacha ni vigumu sana
 
yakwetu yanatushinda ya huko nje tunayatakia nini..?
 
Acha ujinga wewe udikteta uchwara na kujirusha kwangu hakuna mahusiano yoyote yale! Na hata kama watu wanajirusha haibadili ukweli kwamba dikteta uchwara na sekta zake MUFILISI kaangusha uchumi wa nchi.

Halafu unalalamika Magufuli kabana huku unawaza kujirusha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha ujinga wewe udikteta uchwara na kujirusha kwangu hakuna mahusiano yoyote yale! Na hata kama watu wanajirusha haibadili ukweli kwamba dikteta uchwara na sekta zake MUFILISI kaangusha uchumi wa nchi.
Ni kawaida za akili za kushikiwa,udikteta unaufahamu kweli?. Kungekua na hata chembe ya udikteta nchi hii usingewaza kujirusha wewe,ungejirushia wapi na saa ngapi?,zaidi ungekuwa mahali unalitumikia taifa. Jaribu kuuliza madikteta walivyo au walivyokua kabla hujamuita mtu dikteta. Na bado,upo uhitaji mkubwa sana kwa taifa hili kumpata dikteta,midomo imezidi mno,kama siyo sasa,awamu yangu nitakuwa full dikteta,watu mfanye kazi,siyo kujirusha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakae hata maisha lakini wafanye mazuri kwa wananchi wao na wanapokosea na raia na wapinzani wasikilize na wajirekebishe badala ya kutaka kuwaua. Huyu Kagame kishaua wapinzani wake wengi sana hadi ndani ya jeshi.
Na alivomwembamba hivo wanashindwaje kumtoa kwa nguvu..
 
  • Thanks
Reactions: Auz
uchaguz gani mshindi anajulikana kama kubet kagame angepewa point ndogo sana 0.5
 
Hakuna aisee ndiyo yale yale ya fake election zinatumika billions chungu nzima wakati matokeo yanajulikana wazi. Nilifurahia sana uchaguzi wa Ghana upinzani kushinda na kupewa nchi bila kumwaga damu. Sijui kama hili litakuja kutokea hapa kwetu.

Hoja mfu hiyo, kwa sababu uliyoitoa kwamba uchaguzi huru na wa haki ni pale tu upinzani unaposhinda!

Kama upinzani una viongozi wenye uchu wa madaraka tu na walalamishi, kila kukicha, unadhani wapiga kura ni wajinga kutokulijua hilo!

Kuongoza nchi siyo sawa na kuongoza chama chochote, hata cha siasa, ambacho wanachama wake ni wa itikadi moja, wafuasi na wanazi tu.

Viongozi wa vyama vya upinzani, kwa mfano hapa nchini, wameonesha, kwa maneno na vitendo, kwamba ni mabingwa wa kutetea maslahi yao. Kwani wakati wapiga kura wao wanatarajia kutetewa bungeni, wao mara kwa mara wabunge wao wamesusia vikao wakidai kutokuoneshwa 'live' au hupeleka 'hayo malalamiko' yao kwa vyombo vya habari, badala ya kwenye vyombo halali vya haki Kikatiba.

Upinzani Kenya umeshindwa tena, sijui viongozi wa upinzani hapa watakuwa na lipi la kusema, baada ya mmoja wao kumpigia debe Rais aliyekuwa madarakani! Tunasubiri kauli yao kwa hamu.
 
Back
Top Bottom