Faini za Trafiki bila elimu tutaendelea na ajali mpaka kiama

clasi

JF-Expert Member
May 5, 2013
379
709
Faini zimetamalaki kuanzia NEMC, TRA na Trafiki, wacha leo nizungumzie za Trafiki kila kosa 30,000/= ukishatozwa (maana yake ni ruksa kuendelea na kosa ulilotozwa faini, hakuna namna ya kurekebisha kosa zaidi ya Faini? ikiwemo kupunguzwa points za kwenye leseni? JELA? KUFANYA KAZI ZA JAMII mfano, usafi.
 
Mkuu hicho ni chanzo kipya cha mapato nchini,ndio mana wanavizia na kukamata tu ili mladi ipatikane 30,000/=, ndio mana hawaishi kutangaza mapato kila mwenzi kuwa wamevuka lengo,mi nadhani furaha yetu ingekuwa kuona mapato hayo yakipungua ili kujua kwamba watu watu wameanza kufata sheria barabarani, lakini imekuwa kinyume chake
 
Juzi rafiki yangu kakamatwa kakaguliwa hakupatikana na kosa. Akaambiwa afungue dashboard. Akaulizwa: Mbona hatuoni Notification? Twende kituoni. Akaambiwa lazima alipe tu. Haiwezekani tangu mwanzo wa mwaka hajapewa notification. Akaambiwa kama hataki kulipa aache gari hapo mpaka kesho yake. Ikabidi alipe tu maana ukiacha gari hapo chochote kikipotea huna wa kimuuliza
 
Kama umepewa reseni na hujui lipi ni kosa barabarani,utasaidiwaje!!!!
 
Back
Top Bottom