Faini mahakamani

Andrew Kellei

JF-Expert Member
Sep 11, 2009
348
123
Wakuu,nimekua nikifuatilia kwa muda mrefu hizi adhbu za mahakama,lakini napata tatizo kidogo.Kwa mfano gazeti la leo la mwananchi ukurasa wa 8 wameandika habari ya Raia watatu wa China ambao wamehukumiwa kwenda jela miezi sita kila mmoja kwa kosa la kuajiri watu wasiokua na vibali vya kuishi nchini na kufanya kazi za ujenzi bila kibali cha uhamiaji.
Kinachonitatiza hapo ni kwamba wanatakiwa kwenda jela miezi 6 au kulipa faini ya shilingi elfu hamsini.
Swali langu ni kwamba,jela miezi sita =na shilingi elfu hamsini?
Je hizi faini zinakokotolewaje ili kuwatendea haki?
Kama mtu anaingiza kwa saa zaidi ya elfu 50 iweje hiyo ndiyo iwe faini ya miezi sita?
Kwanini kipato cha mtu kisikokotolewe kwa mwezi then wazidishe kwa idadi ya hiyo miezi?
Je mahakama zetu zinazingatia hali halisi ya maisha au wanatoa faini kulingana na sheria za miaka ya sitini?
Msaada tafadhali.
 
Mkuu tatizo hapa ni kuwa sheria yetu ya kanuni za adhabu imepitwa na wakati.
 
Back
Top Bottom