...kumbuka, pensheni yako haitokutosheleza kulipia;
1. kodi ya nyumba/chumba
2. ada ya shule kwa mwanao/wanao.
Ugumu wa maisha unaoupata sasa ni 'ishara' ya huko unakoelekea, na huenda yakazidi ugumu, upweke na ukiwa.
Wakati huo ushapoteza kazi, marafiki, na hata ndugu ulowainua kwa pesa zako za ujana. Wahenga walisema, ' mtumai cha ndugu...' Hala hala usijekimbiwa hata na wanao.
Jiwekee 'akiba'...jenga, nunua hisa kama unaamini, nunua pensheni, jiwekee bima ya afya, jipangie maisha...Muda unakuacha mkono.