SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,151
- 7,920
Mimi huwa napenda kuja na hoja fikirishi kwa hiyo wale wasiopenda kufikiri wananionaga hamnazo. Muda huwa unadhihirisha kile ninachosemaga.
Kumekuwa na malalamiko ya kutaka CAF ibadili fainali za mechi za Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho kutoka mechi mbili na kubakiwa na moja. Binafsi napendeleza fainali hizo ziwe zinachezwa kwa mtindo wa mechi 3 na siyo 1 kama inavyopendekezwa na baadhi ya watu au 2 kama ilivyo sasa. Huu utaratibu wa mechi 3 unaweza kuanza kutumika hatua ya robo fainali.
Ukiacha changamoto ya Afrika ya mashabiki kusafiri umbali mrefu kwenda nchi ya 3 kwa ajili ya fainali, nitaongelea zaidi hatari ya kutopata bingwa anayestahili endapo fainali itakuwa mechi moja. Tukumbuke tunataka bingwa wa viwango na siyo wa kubahatisha.
Mechi moja ina hatari ya kutoa mshindi asiyestahili kwa sababu inawezekana yule mwenye uwezo labda asiamke vizuri siku hiyo. Hii ni sawa na uende kufanya mtihani ukute kuna swali moja. Kuna mjinga anaweza pasi kuliko wale wenye uelewa mpana zaidi kwa sababu tu jana yake kitu pekee alichopitia ni hilo swali. Ndiyo maana mitihani ina maswali mengi ili kutoa nafasi kwa mwenye uwezo zaidi kuonekana na vilaza pia kuonekana.
Ligi ya mpira wa kikapu ya NBA inalijua hili vizuri sana ndiyo maana "playoffs" zake ni mechi 7. Hii ni kuhakikisha yule mwenye uwezo ndiyo anapita kila hatua hadi anapatikana bingwa.
Kuhusu mechi ya 3 kuchezwa wapi, kuna njia tofauti zinaweza kutumika. Wanaweza kuangalia yule aliye juu ya mwenzake katika rank za CAF kupewa faida ya wenyeji kwa mechi 2, inaweza pia kuwa yule atakayeanza mechi ya kwanza apewe ahueni ya mechi mbili za kwanza kabla ya kumalizia mechi ya 3 kwa timu ya pili. nk.
Binafsi naamini future bora ya mpira wa Afrika ni kufanya mashindano ya AFCON kama ligi rasmi ya Afrika na hizi za vilabu kuwa ya chini yake. Niliwahi kulieleza hili katika uzi huu.