Faida za Windows phones

Faida za Windows phones

Mad Scientist

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2013
Posts
215
Reaction score
77
Baada ya pita pita zangu katika forum yetu ya Tech, Gadgets & Science nimeona kuna jamaa yangu kajaribu kuelezea faida na hasara za Windows phone. Nami naomba nielezee faida nilizoziona kwa haka kalumia kangu.

1. Windows phone zinakaa na charge kwa muda mrefu zaidi kuzidi za android. Kubali au kataa ila muulize mtu yeyote anaetumia windows phone ataitaja hii kama faida ya kwanza. Ukiwa na windows phone hauitaji power bank wala kaobama kwa ajili ya emergence unapokuwa safarini au TANESCO wanapoamua kufanya wanachoweza.

2. Windows phone haziathiriwi na virus. Simu hizi zipo full protected kwahiyo ukiwa nayo hauitaji kudownload any antivirus wa kununua. Na hakuna antivirus unayoweza kuiweka kwa windowa phone.

3. Apps zilizopo kwenye store ni zile ambazo haziwezi zikaidhuru simu yako kwa namna moja ama nyingine. Hapa kwa wale watundu wa kuroot android phone wananielewa. Kuna baadhi ya apps za android ukikosea tu! Simu unaiweka kwenye droo.

4. Windows phones are user friendly. Ama tunaweza kusema ni rahisi kutumia hasa unapoinunua kwa mara ya kwanza inakuelekeza kwa namna ambayo hata kama hujawahi kutumia smartphone basi utajikuta na wewe ni mtaalam.

5. Windows phone ni imara kwenye kurun apps. Hapa naongelea ubora wa RAM. nilikuwa natumia android ya internal 4GB na RAM 512, sasa nina windows phone yenye internal 4 GB na RAM 512. Lakini nilipata wakati mgumu kucheza games na kurun apps nyingi kwa wakati mmoja. Hivi sasa nina game 6 zenye ukubwa zaidi ya MB 45 kwa kila moja unapodownload na ninazicheza muda wowote ninapotaka bila kukwama na charge inatumika kidogo bila simu kuchemka.

6. Kwa wale wasomi na wanaopenda kusearch basi windows phone zinawafaa kwani search option ipo standby muda wote. Pia unaweza kubadili search engine kwa google au bing.

Zipo faida nyingi sana na kama unazo ziongezee hapo ili wadau wazielewe windows phone. Kwa upande wangu android bye bye
 
Kwenye windows phone apps za MS office zipo fresh. Mtu unaweza kuedit/kusoma MS documents kirahisi.
Ila ina limited apps ukicompare na android na updates za most apps zinakuja late sana ukicompare na za android
 
Sina sim ya Adroid wala Windows ila kwa maelezo wanayotoa wadau na mpango wa kununua walau Lumia 630
 
Mimi na androids kama maji na samaki
 
Niliwahi kufikiria kununua Lumia lakini nilipofika dukani muuzaji akanishawishi nikanunua ya Android na pia bei za Lumia ziko juu.
 
Niliwahi kufikiria kununua Lumia lakini nilipofika dukani muuzaji akanishawishi nikanunua ya Android na pia bei za Lumia ziko juu.

Labda aliona hela zako za mawazo sasa ili asikukose bora akuuzie tu Android...
 
Tangu nimeanza kutumia Windows phone sitaki kabisa kusikia kuhusu huo upuuzi sijui Android, hizi simu tamu sana aisee achana kabisa.
 
Mimi hapa ninatumia MICROSOFT LUMIA 535. Ila napata shida ku-save Whatsapp audio files. Mambo mengine yapo poa kabisa
 
Sasa bei ikiwa juu huoni kuwa na ubora upo juu

Unanunua simu kwa sababu unataka ikupatie huduma fulani na uwezo wako. Sasa kama unaweza kupata simu inayokidhi mahitaji yako na kwa uwezo wa mfuko wako kuna haja gani ya gharama kubwa
 
Labda aliona hela zako za mawazo sasa ili asikukose bora akuuzie tu Android...
Acha dharau mkuu. Unaenda ukiwa na budget na sio ukiona kila kilicho kizuri unakinunua ...utanunua vingapi!♣
 
Niliwahi kufikiria kununua Lumia lakini nilipofika dukani muuzaji akanishawishi nikanunua ya Android na pia bei za Lumia ziko juu.

Huwa lumia zinakuwa bei rahisi compare na wenzake wa android.

Mfano hii lumia mpya za 4xx range microsoft anaziuza dola 70 tu na hapa tanzania unazipata chini ya laki 2.

Ina 1gb ram, dual core sd200 processor. Je kuna simu ngap tanzania mpya chini ya laki 2 zenye ram 1gb?
 
Hapa natumia Lumia 1520 window 10 preview sio mchezo na wiki ijayo tutapata update nyengine amabayo itakuwa ina uwezo wa kutumia wireless keyboard na mouse. Na utakuwa na uwezo wa kutumia office Kama una laptop. Duh hawa jamaa ni nouma
 
Hapa natumia Lumia 1520 window 10 preview sio mchezo na wiki ijayo tutapata update nyengine amabayo itakuwa ina uwezo wa kutumia wireless keyboard na mouse. Na utakuwa na uwezo wa kutumia office Kama una laptop. Duh hawa jamaa ni nouma

Ulinunua sh.ngapi mkuu?
 
Winjows phone ni simu zisizo na mashiko kabisaa kwani unadhani wote tupo ofisini
 
Back
Top Bottom