Faida za sumu ya nyuki anapokuuma

kufa kupo Bro...
usiogope kufa hata siku moja...maana huwezi kukikimbia

Bali Ugopa baada ya kifo
Ni nini kitakachofuata.....!!!
kufa kupo
ila kama kufa kupo ndio wenzangu wafe na magonjwa makubwa na mimi nife kwa kung'atwa na nyuki kweli?
hapana is not fair distribution
 
Mkuu ni sumu ya nyuki tu au na nge?
 
Sumu ya nyuki ikizidi mwilini unakufa. Nishashihidia mtu alivamiwa na nyuki wengi baada ya kukimbizwa hospitali yule mtu alifariki.
Mleta mada ndugu ndege JOHN unaliongeleaje hili?
 
Niliwahi kung'atwa na nyuki kwenye mkono wa kushoto nilihisi kama napooza mwili au moyo unasimama, nikaja kuambiwa nipake asali na kweli nilivyopaka maumivu yale makali yakaisha, lakini yale maumivu siwezi kuyasahau.
Kweli dawa ya moto ni moto
 
Nenda hospital mara nyingi vyanzo vya Kansa vinakuaga vya ajabu ajabu,
Kimbiaaaaaaaaa.
 
Mkuu. Ungesema kuumwa na nyuki kunaongeza nguvu za kiume au kunaongeza makalio ya kinamama au kurudisha bikra. Bei ya nyuki ingepaa na wengi wangefuga nyuki ili watu waje waumwe kwa kulipia
 
Nimelina sana nyuki kwa maji ya baridi kwa nyuki walio kwenye miti na kwenye nyumba. Na kwa moto wa nyasi kwa walio kwenye vichugu. Kwa nyuki waliooning'ata basi kama ningekuwa na ukimwi kipindi hicho ungeisha.

Maana ilikuwa ni kuvaa sweta la mikono mirefu unachomekea suruali na unafunga rubber band au kamba kwenye miguu ya suruali na mikononi kuzuia nyuki wasiingie ndani ya nguo then unakaza na shingo.

Unamwagia nyuki maji, wanaanguka chini then unaanza kata masega. sasa sio wote wanaoanguka, kuna wanaobaki kwenye masega, hawa wanang'ata mikono mpaka unapata ganzi.
 
I say, wewe mwanaume kweli! Mie niking'atwa na mmoja tu nalia kama mtoto, si kelele hizo majirani wote watajua!
 
Sumu ya nyuki ikizidi mwilini unakufa. Nishashihidia mtu alivamiwa na nyuki wengi baada ya kukimbizwa hospitali yule mtu alifariki.
Mleta mada ndugu ndege JOHN unaliongeleaje hili?
Hapana mkuu huyo alifariki kwa sababu unapong'atwa na nyuiki wengi hutakiwi kutumia dawa ya hospitali wala kuchoma sindano yoyote.
Mimi mwenyewe nlishawah kung'atwa na nyuki wengi adi ubehuwa unabehuwa Kama umekula asali na mpaka ulikua ukiniingalia utadhan mdudu maana sura haijulikan adi makwapani mkuu, nlikua nmenyoa dongo ani ukiniangalia kichwani Kama vile ni mvi kumbe ni sindano za hawa jamaa lkn sikutumia dawa yoyote zaidi ya kupakwa asali mwili mzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ok basi nilifikiria sumu nyingi ya nyuki ndio iliyosababisha kifo chake. Na kwasababu wewe ilikutokea hivyo hivyo na hukufariki basi nakubaliana nawe kuwa mchanganyiko wa sumu + hayo madawa ulisababisha kifo chake.
 
Nimesona andiko hili kwa makini, nimenufaika na ambayo nami nilikuwa siyajui. Ila kwa sababu ya kusaidia wasomaji wengine kunufaika zaidi na maarifa ya sumu ninaweka link hii ya makala yanuvunaji wa sumu ya nyuki ambayo nimeandika hapa jamiiforums kusaidia wasomaji.

Makala hiyo some hapa: Uvunaji wa Sumu ya Nyuki nimeandika mwenyewe nikiwa mfugaji na mmoja wa wavunaji.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…