Faida za sumu ya nyuki anapokuuma

Ukimaliza za nyuki, uje na faida za kugonhwa na nyoka halafu umalizie za kung'atwa na simba
Sent from kekonuuuwanjawamchanga

Sent using Galaxy S10+
 
Ukimaliza za nyuki, uje na faida za kugonhwa na nyoka halafu umalizie za kung'atwa na simba
Sent from kekonuuuwanjawamchanga

Sent using Galaxy S10+
Ninachotambua sumu ya nyuki pia inavunwa na kuuzwa Kwa matumizi ya kutengeneza dawa, lakini sumu ya nyoka ni kali zaidi ya sumu ya nyuki hivyo kila inapoingia mwilini ni hatari. Ila ngoja tungoje wenye uelewa zaidi waje?
 
inabidi ukamatwe upelekwe maabara uchunguzwe
tukikugundua ni mzima wa akili kabisa tunakuweka kwenye mzinga wa nyuki
ukipona utarudi jf kuendeleza thread yako
watu wanadai kung'atwa na nyuki accident wewe unatuambia ni neema
Hapo anamaanisha : Kosa lenye Bahati.
Ila ujue: Mzinga wa nyuki haukumbatiwi.
Kuna ukweli fulani kwenye mada hii - kwa mfano ni mara chache sana kumkuta Mrina asali wa muda mrefu anasumbuliwa na tatizo la maumivu ya viungo (Arthritis) eg. mabega kuuma, magoti kuuma n.k.(maumivu yasiyokuwa gaut).
Kwa mantiki hiyo, naomba msimkamate na kumpeleka maabara ila fanyeni uchunguzi wa hayo aliyosema ili nanyi mjifunze kitu.
 
Ninachotambua sumu ya nyuki pia inavunwa na kuuzwa Kwa matumizi ya kutengeneza dawa, lakini sumu ya nyoka ni kali zaidi ya sumu ya nyuki hivyo kila inapoingia mwilini ni hatari. Ila ngoja tungoje wenye uelewa zaidi waje?
Sumu ya nyoka ni dili kubwa. Huuzwa na hutumika kutengeneza dawa za Local anaesthesia. Wapo watu wajasiriamali hufuga nyoka kwa ajili ya kukamua sumu yao na kuiuza nchi za nje.Yupo jamaa hapa Jf aliwahi kuleta uzi unaouhusiana na biashara hii.
 
Iweje basi watu wanakufa kwa kung'atwa na nyuki japo hawana allergy?
Inategemea kiasi (uwingi) cha sumu kilichoingia mwilini mwako, Uwezo wa mwili wako kuhimili madhara au kishindo cha sumu mwilini. Hii inaitwa Lethal Dose (LD). Sumu ikiwa kiwango cha juu ya LD utaathirika vibaya lakini ikiwa chini ya LD, utaendelea kudunda. Wapo watu hata nyuki mmoja tu akimng'ata inakuwa ni shughuli pevu kwake lakini wakati huo-huo wapo watu wanahimili kung'atwa hata na nyuki zaidi ya 10.
 
Sumu ya nyoka ni dili kubwa. Huuzwa na hutumika kutengeneza dawa za Local anaesthesia. Wapo watu wajasiriamali hufuga nyoka kwa ajili ya kukamua sumu yao na kuiuza nchi za nje.Yupo jamaa hapa Jf aliwahi kuleta uzi unaouhusiana na biashara hii.
Kuna vitu ni risk sana
 
Kuna vitu ni risk sana
Ni kweli mkuu. Kwa mfano yule jamaa aliyeleta uzi hapa Jf. alikuwa anaomba msaada afanyeje na nyoka hao maana Tajiri wake kutoka Kenya aliishia mitini na nyoka wanazidi kuzaliana/kuongezeka. - Ni hatari hata kwake mwenyewe.
 
Binadamu aking’atwa na nyuki hupata faida nyingi ikiwamo kusaidia kuondoa sumu mwilini.

Sumu ya nyuki Ina uwezo wa kupambana na seli za saratani pia hupunguza maumivu katika viungo.

Inayo component inayoitwa mallitini inayopambana na virusi vya ukimwi Bila kuua seli gai za Kinga ya mwili.

Kuna mpaka huduma ya kung'atwa na nyuki au kudungwa Kama sindano.

Inashauriwa kuumwa na nyuki mmoja au wawili ndani ya mwezi.

Angalizo usiwe tu na allergy ili usivimbe. Pia sumu ya nyuki huongeza usambaaji msukumo wa damu yapo maziwa ya nyuki ambayo ni maalumu kwa ajili ya kulishwa malkia wa nyuki na maziwa hayo mtu akitumia huongeza akili.

Maziwa ya nyuki yana protini nyingi na kwa mwenye kuyatumia anakuwa na akili nyingi sana na kama ni mwanafunzi atakuwa anafanya vizuri kwenye masomo kwa kushika nafasi za juu.

View attachment 1641475





Nyuki wa kike,yaani vibarua na malkia wana mwiba mwishoni mwa
tumbo ambao wanaweza kuuchomoa na kuufutika tena.Malkia kwa
kawaida anatumia mwiba huu kutaga mayai,lakini anaweza pia
kuutumia kudunga maadui.Tone ambalo ndiyo sumu ya nyuki,huvuja
kutokea kwenye mwiba unapochomolewa.Mwiba huu pia una miiba
midogomidogo inayojitokeza kuzunguka mwiba mkuu.
Sumu ya nyukii natengenezwa ndani ya tezi ya sumu,na inahifadhiwa
ndani ya kifuko kidogo mwishoni mwa mwiba mkuu.Nyuki
wachanga wanasumu kidogo.Vifuko vyao vya sumu huwa havijazwi
hadi siku ya15 hadi 20 toka kuzaliwa ambapo huwa na sumu kiasi
chamilligramu3/10(tatuyakumi).Nyuki wanaokua wakati wa majira
ya maua mengi huwa na sumu nyingi na yenye nguvu zaidi.
Sumu ya nyuki huyeyuka katika maji lakini sikatika mafuta.Spiriti
inadhuru sumu ya nyuki.

Nyuki anapokudunga mwiba wake,anasukumiza maji ya sumu kupitia
katika mwiba huo,nakuingiza sumu mwilini mwa adui.Nyuki
vibarua hawatagi mayai bali huutumia kudunga.Kama nyuki
akimdunga mwiba nyuki mwenzake,au nyigu,mjusi au nyoka,
anaweza kuuchomoa mwiba.Lakini kutoka na namiiba midogo
midogo inayozunguka mwiba mkuu,mwiba hubaki mwilini mwa
binadamu au wanyama wenye damu ya joto.Mwiba huendelea kuvuja
sumu kwa dakika 10 hadi 20,ambapo 1/3ya sumu huwa imevuja tayari
kutoka kwenye kifuko cha sumu.Kiasi kikubwa cha sumu huvuja
katika dakika ya kwanza.Nyuki au mdudu mwingine anaweza
kuuawa kwa kudungwa mara moja;kuku,farasi au punda,huweza
kuuawaa kwa kudungwa mara kadha,lakini binadamu anaweza kustahimili
sana hata anapodungwa mara nyingi.

Mtu ambaye amevamiwa na kundi la nyuki anaweza kuwa na mamia
ya miiba mwilini mwake.Hii miiba inaweza kuhesabiwa hospitalin iili
kujua vizuri idadi ya miiba inayoweza kufanya watu mbalimbali
kupoteza fahamu au kufa.Kwenye mwili wa binadamu,duara nyeupe
ya kipenyo cha sentimita moja(1sm) hujitokeza kuzunguka sehemu
iliyodungwa,halafu sehemu kubwa zaidi huvimba.Mara baada ya
kudungwa mwiba wa kwanza,mtu atajisikia dalili mbaya kwa mfano
kuumwa kichwa,kuvimba pale palipoumwa,na mwasho.Watu wengi
zaidi hujenga ustahimilivu,lakini wengine hupata mzio baada ya
kudungwa na miiba ya nyuki hata iwe mara nyingi.
Sumu ya nyuki inadhuru hata ikiwa ni kwa kiwango cha chini sana,na
baadhi ya watu wanapata mzio,hasa inapopitia ndani ya mwiba wa
nyuki mwenyewe.Ndani ya saa moja baada ya kudungwa,mtu
mwenye mzio huathirika msukumo wa damu ambao hushuka kwa
kiwango kikubwa mno kinachosababisha figo kuzorota na
kusababisha kifo kwa mtu huyo.Damu hupitapita katika mwili wa
mtu,nakusababisha upungufu wa uteute ndani ya viungo vyote
vyenye kazi maalum mwilini,hasa figo.Kutapika na kunywa maji
huweza kurekebisha tatizo hili,kwa vile damu sasa hurudishwa katika
mfumo wa uyeyushaji chakula mwilini na kwenye viungo vingine vya
mwili.Tahadhari na njia za kujilinda ni ya muhimu sana wakati wa
kujihusisha na nyuki,unapovuna au kusindika sumu ya nyuki.

Kwa watu wasio na mzio,sumu ya nyuki huongeza usambazaji damu
ndani ya mwili,nakuruhusu damu ipite kwa urahisi katika mipaka ya
kila chembechembe hai za mwili.Mshipa inayosafirisha damu
mwilini hupanuliwa,na msukumo wa damu huteremka.Sumu ya
nyuki vilevile hulegeza misuli,na huweza kupunguza maumivu ya
misuli kwa kuyeyusha kemikali ziitwazo“lacticacid”kwa
kiingereza,zinapokuwa mwilini.Kiasi kidogo cha sumu ya nyuki,
huburudisha mwili,lakini kiasi kingi husababisha kuongezeka kwa
mapigo ya moyo,kukosa usingizi,sawa na matokeo ya kunywa
kahawa nyingi mno.Inaweza pia kusababisha ongezeko au upungufu
wa mkojo.
Kwamujibu wa takwimu zilizopo,wafugaji nyuki wanaepushwa
kuugua maradhi kadhaa kutokana na kudungwa miiba ya nyuki hivyo kuingiziwa mwilini sumu ya nyuki,
mfululizo.
Maradhi
wanayoepushwa nayo ni kwa mfano baridiyabisi,maumivu ya viungo
na saratani/kansa.
Zipo kumbukumbu zinazoeleza mafanikio ya wagonjwa waliokuwa na
maradhi sugu yakuganda viungo ambao waliweza kutembea tena
baada ya kudungwa sana miiba ya nyuki.Sumu ya nyuki inaamsha
utengenezaji wa kemikali iitwayo“cortisone”kwa kiingereza,ambayo
ni dawa itengenezwayo na tezi za figo katika sehemu iitwayo
“adrenalcortex”ndani ya figo.Hii kemikali huchangamsha mfumo
wa fahamu,hasa usambazaji hisia ndani ya fundo la neva liitwalo,
“myelin”.Sumu ya nyukii nasemekana kuweza kutibu uharibifu
katika fundo la“myelin”.
Sumu ya nyuki hutumika kwa njia mbalimbali.Inavutwa kupitia
puani,inamezwa ikichanganyika na asali,inadungwa mwilini kwa
kutumia sindano,au kufungwa juu ya mwili kama madawa
yaliyolowa.Sumu ya nyuki inafika mwilini kwa kudungwa miiba ya
nyuki kwa makusudi,kama tiba peke yake au kwa kuchanganya
utaalamu wa tiba ya nishati ya umeme(electrotherapy,kwa
kiingereza),au utaalam wa tiba ya Kichina iitwayo kwa kiingereza
“acupuncture”,na“acupressure”..Nchini China na Japani hutumika mwiba tuulionyofolewa unaofanywa sindano ya kudunga katika sehemu
zinazotibiwa kwa“acupuncture”.Maumivu yanatokea,lakini siyo
makali sana.

Uzalishaji na utayarishaji
Sumu ya nyuki ni sumu halisi na inaweza kuua wanyama na
binadamu.Kwa ukusanyaji wake,uvunaji na uzalishaji,tahadhali
maalum zinahitajika,kama vile mipira ya kuvaa mikononi(glovu),
mpira wa kufunika mdomo,na kadhalika.Usivute hewa au kumeza
sumu ya nyuki kwa njia yoyote bila kufuata kwa uangalifu maagizo ya
daktari,na kiasi cha dawa.
Sumu ya nyuki huvunwa kwa kutumia kikusanyio maalum.Hiki
chombo kina umbo la sahani ya kioo,ambacho waya zimewambwa
juu yake na kuunganishwa na chanzo cha umeme kwa mfano beteri
moja kubwa au ndogondogo kadhaa.Hapo nyuki watakapogusa
nyaya zenye umeme,watamwaga kwa hasira sumu kutoka vifuko
vyao vya sumu.Baada ya nyuki wachache kumwaga sumu yao,kundi
zima lanyuki litavamia sahani yote kwa maelfu na nyuki watamwaga
sumu kwenye sahani hiyo.
moja ya kitu ghali duniani ni sumu ya hawa jamaa
 
Back
Top Bottom