Faida Za Kuwa Mama Wa Nyumbani

Faida Za Kuwa Mama Wa Nyumbani

Nilitaka kuona michango ya wanawake waliolewa humu ili nijue misimamo yao ikoje, mleta uzi heshima kwako, hata mimi wife nilimbwambia kaa nyumbani, kama unataka shughuli ya ukufanya nenda dukani, huko nako staki uka spend masaa mengi, rudi nyumbani angalia watoto wetu, nilicho kifanya nikumwonesha kote ambako hua nachukua bidhaa ya dukani na namna ninavyo fanya biashara (nimeajiriwa na kufanya biashara kwa pamoja, kazi yangu is time demanding kweli, hata usiku napokea simu za taarifa na kutoa maelekezo ya nini kifanyike). Nafikiri kuna connection fulani ya tabia mbaya za vijana wengi sasa hivi na u busy wa akina mama, think, kwanini pia watoto wa siku hizi wanajua ngono mapema sana kuliko zamani? Utasema utandawazi i.e TV na internet, well kama mama yupo home anaweza kudhibiti hadi baadhi ya vipindi kwao.
 
vizuri siku nyingine leta uzi wa faida za kuwa baba wa nyumani maana watu hawaelew nako kama kuna faida!!!!!
 
It is not necessary kupambana na mafoleni na kukaa ofisini hadi saa 12 ili kuleta money at hm,many alternative ways of earning cash must be considered for a woman to be independent and strong
 
Wababa umetuongezea mzigo wa kutafuta hela. Na pia unaposema tuwafungulie biashara wake zetu, unafikiri ni rahisi namna hiyo? Mitaji tuitoe wapi?
Pia biashara makini yenye kuleta faida inahitaji usimamizi wa hali ya juu. Kwahiyo bado mama atatumia muda mwingi kwenye biashara.
Tunapenda wake zetu wakae nyumbani watunze watoto, lakini hali ya uchumi ni mbaya kiasi kwamba baba peke yako unazidiwa na majukumu.
Lakini option ya mama kukaa nyumbani ndiyo the Best though it's not applicable, kwa zama hizi!
 
.yap umefunguka vyema na ulichokisema ni UKWELI mtupu,katika maisha ya NDOA sehemu kubwa ya malezi, ujenzi wa afya na ufahamu wa watoto hutoka kwa mama nadhani na zaidi ya asilimia 90 dada queeny, sehemu kubwa wanaume twajifanya tunajua kulea na kufanya mambo muhimu kwa watoto wetu, lakini twashindwa kwasababu tu si asili yetu, na ukaribu wa mtoto haswaa uko kwa mama. Najua wanaume wengine mtakataa lakini ndo ukweli, kwani ukipiga hesabu vizuri utagundua kuwa unasema wawapenda wanao kwa kiwango cha juu kwasababu tu mama yuko karibu na watoto, upendo wake mama ulio wa kweli unaangaza maisha yao vyema, then kwasababu wanastawi na kuchanua vyema, afu jamii inakutupia sifa waona unaweza kumbe mama akitoka kidogo tu lazima urudi Maktaba ukaperuzi kidogo namna ya kuishi na watoto.. na naamini fasiri halisi ya mama wa nyumbani ni "mama ambaye mda mwingi yuko karibu na watoto wake kimwili (afya ya mwili), na kiroho (maadili ya jamii/dini) akihakikisha kwamba watoto hawapungukiwi mambo haya muhimu"..na suala la kwamba kuwa mama wa nyumbani ni kama golikipa si kweli kwani wengi wetu tumeishi maisha ya utoshelevu kwa shughuri ndogo ndogo za hawa mama zetu..
 
duh! Like km 800 hiv, natamani niwe nazaa tu na kulea mwnywe,mume anatafuta pesa...mambo ya hg kunilelea watt cpendi lkn huu mfumo mh!
 
Topic nzuri sana.
Mimi naunga mkono hoja. Lkn queeny wanaume wa sikuizi nao wanatuzeveza, unaweza ukasema unakaa nyumbani, mwanaume akaja kukubadikia, keshakuzalisha wtt, mara anakutelekeza na wtt, wewe ndo uanze kuhangaika na wtt. Unaanza alifu kwa ujiti.
Mi kusema kweli natamani sana to be a housewife but to be honest m scared

Mh! Hili nalo neno!
Tatizo kubwa kwa ss
 
Last edited by a moderator:
mwanaume mshenzi ni mshenzi tu, hata ukifanya kazi atakufanyia ushenzi.
Kikubwa kwa mwanamke ni kujitahid uwe na akiba yako na uongee na mumeo uwe na miradi midogomidogo walau 2 ya kukusaidia lakini ambayo haitakubana hata kdg kiasi cha kukunyima mda wa kuhudumia familia.
Miradi ambayo iko flexible kiasi cha mumeo kuweza kukusaidi pindi unapokuwa umebanwa na mambo kama ujauzito, uzazi nk.

Thanx,point noted
 
Habari wanajamii wote popote mlipo hapa duniani. natanguliza heshima za dhati kwenu nyote na itifaki imezingatiwa.

Napenda niwashirikishe wanajamii wenzangu kuhusu faida za kuwa mama wa nyumbani na naomba niseme kuwa kwa miaka ya hivi karibuni, jamii imekuwa ikimdharau sana mama wa nyumbani na kumuona mvivu na hana mchango wowote kwenye maendeleo ya familia yake eti kisa haingizi CASH. jamii imeenda mbali hata kudiriki kumtungia maneno ya kashfa na kejeli kwamba ni golikipa yani ni kama kandege kanakosubiria kufumbua mdomo na kupokea chakula kutoka kwa mama yake pasipokuwa na mchango wowote katika kutafuta chakula hicho.

Tukumbuke kwamba wamama zetu walio wengi waliweza kutulea na kutuwezesha kuwa na maadili mema kwa kuwa walikuwa karibu yetu masaa 24. kuanzia tulipozaliwa wamama zetu walio wengi;

1. wametunyonyesha si chini ya miaka 2

2. wametuogesha utoto wetu wote (mama anapokuogesha anahakikisha umetakata na anakukagua mwili mzima kama siku hiyo umeumia au una kidonda basi mama atajua mara moja na kukuhudumia ipasavyo)

3. kukupikia uji/chai na kuhakikisha amekunywesha kila siku. kama unaumwa atajua. ni furaha kubwa sana kwa mtoto kulishwa na mama yake.

4. kukuandaa kwenda shule huku akikusisitiza usome kwa bidii

5. kufuatilia kwa ukaribu masomo yako na kuhakikisha unaishi kwa adabu pale nyumbani maana yupo muda wote kufatilia mwenendo wako (bakora za kutosha).

Wakati huo baba yeye yuko bize kibaruani kuhakikisha analeta mahitaji yote ya familia yake na cha kushangaza maisha yalikuwa mazuri na matamu sana. kulikuwa hakuna dharau. Mama alikuwa anamuheshimu baba maana anajua mchango wake katika familia. Baba naye alikuwa anamuheshimu mkewe maana alikuwa anajua mchango wake katika familia. hivyo kila mtu alikuwa na wajibu wake na familia nyingi (sio zote) silizoishi kwa mfumo huu zimekuwa familia bora.

Je, kulikoni nyakati hizi???

- pesa imekuwa ndo kila kitu. kumekuwa na vita ya pesa kiasi kwamba si baba wala mama anayependa kupitwa na hii kitu

- pesa imekuwa ndio msingi wa familia... hapendwi mtu bali pesa. leo hii mwanamke ukijitolea kuwa mama wa nyumbani ili uwalee watoto wako ipasavyo, uwepo muda wote watoto watakapokuhitaji, unaonekana wa ajabu, jamii na hata mume wako hatokuelewa. lakini ukiondoka nyumbani saa 12 asubuhi na kurudi saa 4 usiku ukitokea kazini (kutafuta pesa), hapo unaonekana mjanja na mpambanaji wa kweli huku nyuma watoto wako wanaharibikiwa.

Hivi kweli hii ni sawa???

Mimi naamini kuwa tumeingia kichwa kichwa katika hii dhana ya usawa na tunakoelekea itatugharimu. Kwa nini?

1. Wanawake siku hizi hawana muda wa kunyonyesha watoto wao kisa wanawahi kazini. kumbuka maziwa ya mama ndio pekee yenye uwezo wa kujenga immunity ya mtoto kwa maisha yake yote. inashauriwa mtoto anyonyeshwe walau miaka miwili (jambo ambalo mama zetu walilijua na kulifanyia kazi japo hawakuwa wamesoma sana). huyu mtoto aliyenyonyeshwa kwa miezi miwili tu atakuwa salama kweli?

2. Dhana hii imewafanya wanaume kuwa wavivu na kukimbia majukumu yao. wanaogopa kubeba mzigo wa familia zao hivyo kutafuta wanawake wenye vipato tayari ili kukwepa majukumu. wake zao wasipokuwa na kazi huwanyanyasa na kuwaona tegemezi (golikipa).

3. Watoto wetu siku hizi wanaharibikiwa kwani wazazi wote wako bize kutafuta pesa, hakuna mwenye muda na mtoto. hakuna anayejua ameamka vipi, kama amekunywa chai ama la, ameenda shule ama la, huko shule maendeleo yake yapoje, labda kapigwa na mtu shule, au dada au kaka wa kazi kamfanyia kitu kibaya, hakuna anayejali.

4. Madhara makubwa ya hii dhana ni kwa wanawake kwani wanajikuta wamejiover-load na shughuli nyingi sana. mfano utakuta mtu ni mjamzito (tumbo kule) hapohapo anahaingaika na kazi kila siku ya Mungu mpaka anajifungua, bosi haelewi una kichefuchefu wala kizunguzungu anachotaka kazi iende.
ukijifungua unanyonyesha miezi 3 tu unakimbia kazini, katoto unakaachia hausigeli ambaye humwamini, unafanya kazi huku presha iko juu. mume naye haelewi. mtoto anakosa bonding na mama yake kitu ambacho ni muhimu sana kwa ustawi wa mwanadamu.

5. Na mengine mengi.....


Sisemi mwanamke asijishugulishe, nachosema mwanamke asiwe bize sana na kusaka pesa, awe na muda wa kulea familia yake (mume na watoto). hata kama ni ujasiriamali usiwe full time ili apate muda wa kulea watoto wake ipasavyo.

Tukubali tukatae, kazi ya kulea watoto na kuhakikiha wanakuwa na maadili mazuri ni ya mama kwa asilimia 90.

HITIMISHO;

-HESHIMA ZANGU ZA DHATI NA ZA KUTOKA MOYONI MWANGU ZIWAENDEE WANAUME WOTE WANAOTAMBUA KUWA JUKUMU LA KULETA MAHITAJI YA NYUMBANI NI LA KWAO NA WANAFANYA HIVYO KWA MOYO WAO WOTE

-WAHESHIMIWE PIA WANAUME WALIO NA WAKE AMBAO NI MAMA WA NYUMBANI NA WANATAMBUA MCHANGO WAO KATIKA FAMILIA NA WALA HAWAWADHARIRISHI WAKE ZAO KWA KUWAITA MAGOLIKIPA AU KUWANYIMA MAHITAJI

-WAHESHIMIWE WANAWAKE WOTE WANAOFANYA DOUBLE JOBS YAANI KUZAA KWA UCHUNGU NA KULA KWA JASHO (wakati wanaume wao wanafanya moja tu ya kula kwa jasho hiyo nyingine hawaielewi). MUNGU AWAFANYIE WEPESI WAMAMA HAO.

Kwa mtazamo wangu USAWA (Beijing) umeletwa kuwakandamiza wanawake na kuharibu familia na si kuwatetea na kuwainua wanawake.

AMANI KWENU WOTE.
ujumbe mzuri sana nafarijika coz nilimwachisha kaz mke wangu hata ndugu hawakunielewa yani anaenjoy kuwa mama wa nyumbani yuko huru
 
queeny thats a very good post.
Mimi nitafurahi sana mwanamke wangu akiwa a housewife. However kipato changu lazima kiwe juu sana. actually niko tayari kwenda bank na kusema kila mwisho wa mwezi akaunt ya mke wangu iingizwe asilimia 30 ya mshahara wangu ili yy tu akae nyumbani na mimi nitatoa kila kiiiiitu kasoro hela za matatizo ya ndugu zake.

Umeniacha hoi hapo kwenye matatizo ya nduguze...
 
Mada nzuri kwa sisi wamama wa nyumbani mana nami ni mmoja wapo, watoto ukikaa nao nyumbani raha sana kwa jinc wanavyokuzoea, hata wakirudi kutoka shule, wa kwanza kuuliziwa ni mama, baba mida yake ni usiku, ikifika mida ya kwenda kulala, kama baba yao hajarudi ndio wanaanza kumuulizia, kama nikitoka kidogo, halafu niwaache nyumbani, nitaharakisha kilichonitoa ili niwawahi watoto, ndio maana wanangu wananipenda sana, kama ulivyosema mtoa mada, kuwaogesha, kuwapikia, kuwafulia, kuwasaidia wafanye h/w, na hata kucheza nao, wanafurahi sana vitu hivi niwafanyie mimi, kuliko dada wa kazi.

big up mama Kijino
mama yangu mama wa nyumban alijitahid kunilea hasaaaa
 
Last edited by a moderator:
wazo hili nilikuanalo lakini umeziD nipa mashik0 ya kwann ni bora wife abaki kulea... dats is BEING A WIFE ni kazi ya KWANZA ya mwanamke.. 18
 
Sorry to say this, but the post is kinda loaded with male chauvinism ideas. And for the era we livin it's utopia.
Nice writing though
 
Back
Top Bottom