Faida Za Kuwa Mama Wa Nyumbani

Faida Za Kuwa Mama Wa Nyumbani

queeny

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
584
Reaction score
421
Habari wanajamii wote popote mlipo hapa duniani. natanguliza heshima za dhati kwenu nyote na itifaki imezingatiwa.

Napenda niwashirikishe wanajamii wenzangu kuhusu faida za kuwa mama wa nyumbani na naomba niseme kuwa kwa miaka ya hivi karibuni, jamii imekuwa ikimdharau sana mama wa nyumbani na kumuona mvivu na hana mchango wowote kwenye maendeleo ya familia yake eti kisa haingizi CASH. jamii imeenda mbali hata kudiriki kumtungia maneno ya kashfa na kejeli kwamba ni golikipa yani ni kama kandege kanakosubiria kufumbua mdomo na kupokea chakula kutoka kwa mama yake pasipokuwa na mchango wowote katika kutafuta chakula hicho.

Tukumbuke kwamba wamama zetu walio wengi waliweza kutulea na kutuwezesha kuwa na maadili mema kwa kuwa walikuwa karibu yetu masaa 24. kuanzia tulipozaliwa wamama zetu walio wengi;

1. wametunyonyesha si chini ya miaka 2

2. wametuogesha utoto wetu wote (mama anapokuogesha anahakikisha umetakata na anakukagua mwili mzima kama siku hiyo umeumia au una kidonda basi mama atajua mara moja na kukuhudumia ipasavyo)

3. kukupikia uji/chai na kuhakikisha amekunywesha kila siku. kama unaumwa atajua. ni furaha kubwa sana kwa mtoto kulishwa na mama yake.

4. kukuandaa kwenda shule huku akikusisitiza usome kwa bidii

5. kufuatilia kwa ukaribu masomo yako na kuhakikisha unaishi kwa adabu pale nyumbani maana yupo muda wote kufatilia mwenendo wako (bakora za kutosha).

Wakati huo baba yeye yuko bize kibaruani kuhakikisha analeta mahitaji yote ya familia yake na cha kushangaza maisha yalikuwa mazuri na matamu sana. kulikuwa hakuna dharau. Mama alikuwa anamuheshimu baba maana anajua mchango wake katika familia. Baba naye alikuwa anamuheshimu mkewe maana alikuwa anajua mchango wake katika familia. hivyo kila mtu alikuwa na wajibu wake na familia nyingi (sio zote) silizoishi kwa mfumo huu zimekuwa familia bora.

Je, kulikoni nyakati hizi???

- pesa imekuwa ndo kila kitu. kumekuwa na vita ya pesa kiasi kwamba si baba wala mama anayependa kupitwa na hii kitu

- pesa imekuwa ndio msingi wa familia... hapendwi mtu bali pesa. leo hii mwanamke ukijitolea kuwa mama wa nyumbani ili uwalee watoto wako ipasavyo, uwepo muda wote watoto watakapokuhitaji, unaonekana wa ajabu, jamii na hata mume wako hatokuelewa. lakini ukiondoka nyumbani saa 12 asubuhi na kurudi saa 4 usiku ukitokea kazini (kutafuta pesa), hapo unaonekana mjanja na mpambanaji wa kweli huku nyuma watoto wako wanaharibikiwa.

Hivi kweli hii ni sawa???

Mimi naamini kuwa tumeingia kichwa kichwa katika hii dhana ya usawa na tunakoelekea itatugharimu. Kwa nini?

1. Wanawake siku hizi hawana muda wa kunyonyesha watoto wao kisa wanawahi kazini. kumbuka maziwa ya mama ndio pekee yenye uwezo wa kujenga immunity ya mtoto kwa maisha yake yote. inashauriwa mtoto anyonyeshwe walau miaka miwili (jambo ambalo mama zetu walilijua na kulifanyia kazi japo hawakuwa wamesoma sana). huyu mtoto aliyenyonyeshwa kwa miezi miwili tu atakuwa salama kweli?

2. Dhana hii imewafanya wanaume kuwa wavivu na kukimbia majukumu yao. wanaogopa kubeba mzigo wa familia zao hivyo kutafuta wanawake wenye vipato tayari ili kukwepa majukumu. wake zao wasipokuwa na kazi huwanyanyasa na kuwaona tegemezi (golikipa).

3. Watoto wetu siku hizi wanaharibikiwa kwani wazazi wote wako bize kutafuta pesa, hakuna mwenye muda na mtoto. hakuna anayejua ameamka vipi, kama amekunywa chai ama la, ameenda shule ama la, huko shule maendeleo yake yapoje, labda kapigwa na mtu shule, au dada au kaka wa kazi kamfanyia kitu kibaya, hakuna anayejali.

4. Madhara makubwa ya hii dhana ni kwa wanawake kwani wanajikuta wamejiover-load na shughuli nyingi sana. mfano utakuta mtu ni mjamzito (tumbo kule) hapohapo anahaingaika na kazi kila siku ya Mungu mpaka anajifungua, bosi haelewi una kichefuchefu wala kizunguzungu anachotaka kazi iende.
ukijifungua unanyonyesha miezi 3 tu unakimbia kazini, katoto unakaachia hausigeli ambaye humwamini, unafanya kazi huku presha iko juu. mume naye haelewi. mtoto anakosa bonding na mama yake kitu ambacho ni muhimu sana kwa ustawi wa mwanadamu.

5. Na mengine mengi.....


Sisemi mwanamke asijishugulishe, nachosema mwanamke asiwe bize sana na kusaka pesa, awe na muda wa kulea familia yake (mume na watoto). hata kama ni ujasiriamali usiwe full time ili apate muda wa kulea watoto wake ipasavyo.

Tukubali tukatae, kazi ya kulea watoto na kuhakikiha wanakuwa na maadili mazuri ni ya mama kwa asilimia 90.

HITIMISHO;

-HESHIMA ZANGU ZA DHATI NA ZA KUTOKA MOYONI MWANGU ZIWAENDEE WANAUME WOTE WANAOTAMBUA KUWA JUKUMU LA KULETA MAHITAJI YA NYUMBANI NI LA KWAO NA WANAFANYA HIVYO KWA MOYO WAO WOTE

-WAHESHIMIWE PIA WANAUME WALIO NA WAKE AMBAO NI MAMA WA NYUMBANI NA WANATAMBUA MCHANGO WAO KATIKA FAMILIA NA WALA HAWAWADHARIRISHI WAKE ZAO KWA KUWAITA MAGOLIKIPA AU KUWANYIMA MAHITAJI

-WAHESHIMIWE WANAWAKE WOTE WANAOFANYA DOUBLE JOBS YAANI KUZAA KWA UCHUNGU NA KULA KWA JASHO (wakati wanaume wao wanafanya moja tu ya kula kwa jasho hiyo nyingine hawaielewi). MUNGU AWAFANYIE WEPESI WAMAMA HAO.

Kwa mtazamo wangu USAWA (Beijing) umeletwa kuwakandamiza wanawake na kuharibu familia na si kuwatetea na kuwainua wanawake.

AMANI KWENU WOTE.
 
Safi sana!
Hongera kwa kutoa elimu hii!
...
Laiti ke wa sasa wangekua na tabia kama za Mama zetu, ingekua raha sanaaa!
.
Ke wa sasa wamekua wazungu weusi!
Awe anakazi awe hana! Ni wavivu sana haki ya Mungu!!!
Niwape hongera tu wale wote wanatambua majukumu yao!
 
My wife stays at home and I do provide the necessities plus everything
My babies mama should be at home taking care of my family while me the baba is working for them
 
Although i dont like my wife to stay at home this much but i must say these are the best minds i ever read since knowing JF in 2006! Very concretely analyzed and convincing! Congrats! Thank you.
 
queeny thats a very good post.
Mimi nitafurahi sana mwanamke wangu akiwa a housewife. However kipato changu lazima kiwe juu sana. actually niko tayari kwenda bank na kusema kila mwisho wa mwezi akaunt ya mke wangu iingizwe asilimia 30 ya mshahara wangu ili yy tu akae nyumbani na mimi nitatoa kila kiiiiitu kasoro hela za matatizo ya ndugu zake.
 
My wife stays at home and I do provide the necessities plus everything
My babies mama should be at home taking care of my family while me the baba is working for them

nakusalute.... keep it up na Mungu ataendelea kukubariki.
 
Although i dont like my wife to stay at home this much but i must say these are the best minds i ever read since knowing JF in 2006! Very concretely analyzed and convincing! Congrats! Thank you.

I mean don't stress her with jobs, she already have her own job as a woman. her job should be something like a part time job so that she can get enough time to take care of the family
 
queeny thats a very good post.
Mimi nitafurahi sana mwanamke wangu akiwa a housewife. However kipato changu lazima kiwe juu sana. actually niko tayari kwenda bank na kusema kila mwisho wa mwezi akaunt ya mke wangu iingizwe asilimia 30 ya mshahara wangu ili yy tu akae nyumbani na mimi nitatoa kila kiiiiitu kasoro hela za matatizo ya ndugu zake.

Hahahaaaaaaa.what if umekufa gafla na mke wako alishazoea kukaa nyumbani na kukuta hela bank.Hivi vitu ni rahisi sana kusema lakini kuviweka kwenye vitendo ni ishu.sasa umemkuta mwenzio wazazi wake wamemsomesha gafla unamwambia kaa home uangalie watoto na hela nitakazo kuwekea usiwasaidie ndugu yako.Haingii akilini
 
queeny thats a very good post.
Mimi nitafurahi sana mwanamke wangu akiwa a housewife. However kipato changu lazima kiwe juu sana. actually niko tayari kwenda bank na kusema kila mwisho wa mwezi akaunt ya mke wangu iingizwe asilimia 30 ya mshahara wangu ili yy tu akae nyumbani na mimi nitatoa kila kiiiiitu kasoro hela za matatizo ya ndugu zake.

heshima kwako... wanaume kama ninyi wachache sana. sikatai mwanamke kufanya kazi au biashara, nachosema ni muhimu hiyo kazi au biashara isichukua muda mwingi hata kusahau kwamba familia inamuhitaji mama. jukumu la kuleta mahitaji ya familia ni la mwanaume. Mungu aliweka hivyo, mwanamke asaidie tu kwa kiasi maana yeye ana kibarua chake cha kuzaa na kulea watoto
 
...more theoretical...! Tofautisha zamani na sasa,maisha yamebadilika sana,over my deadbody haitokaa itokee kuwa golikipa hata siku moja hata mume wangu awe na pesa zinazojaa godoro za mtaa mzima!
 
Tatizo vijana wa cku hizi niwaoga wa MAISHA wanataka kusaidiwa kutunza Familia na wake zao! mbona cjackia wanawake wanaomba Msaada kwa waume zao wawasaidie kubeba MIMBA! Ishu ya kwamba baba ukifa itakuwaje kwa MKE uliemuacha haina maana yyte! kwani Wazee wetu walikuwa hawafi?! Vijana tambueni wajibu wakutunza Familia zenu! Ndomana dharau hom haziishi kwa7bu ya vijana wakiume kushindwa kutunza MKE na Watt wajanja wakiwasaidia mnarusha ngumi duh!!! Mleta mada hongera kwa kuwashuri PIPO wasiojitambua
 
Ujumbe mzuri ila kwa mimi nionavyo Maisha yamebadilika sana..........

The cost of living is high kuna umuhim wa kufanya kazi ili tuweze kusaidiana wote wawili........
 
Hii ni moja kati ya nyuzi zenye akili sana ambazo nimepata kuziona hapa JF...ama kwa hakika wewe ni GREAT THINKER...big up QUEENY..
 
Mada nzuri na heshima Mama wa Home
huwa wanalea vzr sana.
 
Safi sana queeny wanawake tumejisahau sana kuhusu malezi ya familia yetu badala yake tumewaachia wadada wa kazi majukumu yote.... Uangalizi wa nyumba, watoto na mume ni letu tujaribu kubalance muda wetu angalau tuweze kutimiza hata kidogo wajibu wetu na si kujisahau kabisa.

HUSBAND LOVE YOUR WIFE, WIFE SERVE YOUR HUSBAND!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
katika mada zote nilizowahi kuzisoma humu, hakika hii imenigusa sana.
Tangu nilipokuwa natafuta mchumba moja ya kigezo kilikuwa ni akubali kuwa mama wa nyumbani, kwamba aiweke familia yetu mbele kuliko pesa. Akubali kutumia elimu yake kwa ajili ya familia na sio kutafuta pesa, kwani kutafuta ni jukumu langu.

Ilinichukua mda ila Namshukuru Mwenyezi Mungu hatimae nilimpata.
Hakika kwa sasa naenjoy maisha kupindukia.
 
Topic nzuri sana.
Mimi naunga mkono hoja. Lkn queeny wanaume wa sikuizi nao wanatuzeveza, unaweza ukasema unakaa nyumbani, mwanaume akaja kukubadikia, keshakuzalisha wtt, mara anakutelekeza na wtt, wewe ndo uanze kuhangaika na wtt. Unaanza alifu kwa ujiti.
Mi kusema kweli natamani sana to be a housewife but to be honest m scared
 
Last edited by a moderator:
Ujumbe mzuri ila kwa mimi nionavyo Maisha yamebadilika sana..........

The cost of living is high kuna umuhim wa kufanya kazi ili tuweze kusaidiana wote wawili........

sikatai gharama za maisha zimepanda sama lakini tunasahau hizo pesa tunatafuta kwaajili ya nani?
Kuwasomesha watoto shule nzuri, kuwalisha na kuwavisha vizuri pekee haitoshi.
Zawadi kubwa kuliko zoote kwa mtoto ni malezi.
Kama hatuwalei vzr hata tuwasomeshe angani bado hatutakuwa tumewatendea haki.
 
Topic nzuri sana.
Mimi naunga mkono hoja. Lkn queeny wanaume wa sikuizi nao wanatuzeveza, unaweza ukasema unakaa nyumbani, mwanaume akaja kukubadikia, keshakuzalisha wtt, mara anakutelekeza na wtt, wewe ndo uanze kuhangaika na wtt. Unaanza alifu kwa ujiti.
Mi kusema kweli natamani sana to be a housewife but to be honest m scared

mwanaume mshenzi ni mshenzi tu, hata ukifanya kazi atakufanyia ushenzi.
Kikubwa kwa mwanamke ni kujitahid uwe na akiba yako na uongee na mumeo uwe na miradi midogomidogo walau 2 ya kukusaidia lakini ambayo haitakubana hata kdg kiasi cha kukunyima mda wa kuhudumia familia.
Miradi ambayo iko flexible kiasi cha mumeo kuweza kukusaidi pindi unapokuwa umebanwa na mambo kama ujauzito, uzazi nk.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom