Faida ya Tanzania kwenye Jumuia baada ya Umoja wa Forodha na Soko la Pamoja kati yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Faida ya Tanzania kwenye Jumuia baada ya Umoja wa Forodha na Soko la Pamoja kati yetu

Discussion in 'International Forum' started by The Quonquerer, Aug 10, 2010.

 1. The Quonquerer

  The Quonquerer JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa wale wataalam, mimi nimekuwa sceptical na hii kitu ya zero rating kwa bidhaa kutoka Kenya na zile za kwetu kwenda kwao. Hivi, kwa kufikia uamuzi huu, si kwamba tume-weaken our potential of domestic industrial growth? Je ulikuwa uamuzi sahihi?Je kuna simulation study iliyofanyika kuonyesha kuwa faida ya kutotoza ushuru itakayopatikana ni kubwa kuliko ule ushuru tuliokuwa tukikusanya (trade off between ‘future' economic growth and revenue loss, i bet in billions). Je hata hizo chache tunazopelekwa kwao, wanapoziwekea NTBs (vikwazo visivyo vya ki-ushuru), maana soko lile lina matatizo, si kwamba tunazidi kuuvaa mkenge? Je uko mkakati upi ulio imara wa kutambua ROOs (Rules of Origin) ili kuwa na uhakika kwamba bidhaa zote zinazo-qualify kweli zinatoka Kenya, TRA na Wizara ya Viwanda na Biashara wana umakini na uwezo kiasi gani kuweza kubaini hili? Na kwenye Soko la Pamoja, je usimamiaji wa utambuzi wa professional qualifications uko makini kiasi gani kuhakiki kuwa hatutaleta vihiyo kwetu hapa kwa kisingizio cha soko la pamoja, hasa iwapo utambuzi wa ndani wenyewe ni tatizo? Na Mutiso , balozi wao anaposema kuwa nchi kubwa zimeendelea kiviwanda hivyo zinataka kutu-weaken as a region kuleta bidhaa zao kwetu na hivyo tufanye biashara kati yetu,maana the Rest of the World tumewawekea CET (Common External Tariff), wao wenyewe kama Kenya, si kwamba nao wanafanya hivyo hivyo kwa nchi wanajumuia wakati wao hawataki kufanyiwa na nchi nyingine. Nina maswali mengi zaidi ya hayo kuliko majibu kuhusu huu ushirikiano, nimeuliza tena kwa sababu kuna member wa JF mmoja na jina nalikumbuka alikuja hapa akaniita ‘myopic nationalist' na mwingine ‘that i live in fear ‘which is OK to me kama sielewi. Sasa, kabla na wengine hawajaniita hivyo, naomba kuelemishwa kwanza kuhusu hayo, maana mimi sielewi mpaka leo! Nadhani JF ni sehemu ya kuelemishana zaidi kuliko kugombana. Naomba kusaidiwa! A thing is that, i don't practice these things, so am not in a picture!
   
 2. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Mkuu hakuna atakayejibu hayo maswali. Si umesikia Mwapachu sasa yeye ndiyo kazi yake kutembeza bakuli kwa donors? Anaomba hata ambacho hakiombeki these guys wanafanyia matumbo yao hizi kazi na kizazi kipya kinakuja kugombea uhuru wa nchi yetu. Economic freedom ambayo Chama Cha Majambazi kimejikabidhi na kuneemesha familia zao na kuwaacha Watanzania solemba. Nyang'au will never change thats a fact kama kweli Kenya wangekuwa na hamu ya kuimarisha collective bargaining power wangekwenda kwenye EGAD lakini kule hawawawezi Sudanese na Ethiopians maana wanawaweka sawa hivyo onea buji kwa Watanzania.

  Wacha waendelee kuwanufaisha wageni lakini time is on our side.
   
 3. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,920
  Likes Received: 1,028
  Trophy Points: 280
  Mkuu hayo maswali tungekuwa tunajiuliza kila mkataba tunaoingia kama vile kwenye madini, kwenye manegement kama RITES, CITY WATER na NetGroup Solution, Nadhani nchi ingekuwa kwenye transional economy tusingekuwa masikini, lkn kwa sababu hatutaki kujiuliza maswali ya msingi ndiyo maana tuko hapa tulipo.

  AKSANTE KWA MASWALI YAKO YA MSINGI.
  BUT REMEMBER. Saa ya ukombozi ni sasa..... VOTE FOR SLAA........ THE CHANGE WE WERE WAITING FOR LONG.
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Aug 10, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,786
  Likes Received: 5,043
  Trophy Points: 280
  ..nchi mwanachama wa EAC ina haki ya kujitoa ktk utekelezaji wa kifungu chochote kile iwapo itaona kina madhara kwa wananchi wake.

  ..kwa mfano, Kenya sasa hivi wameweka mgomo ktk uanzishwaji wa sarafu moja/single currency kwa nchi za Afrika Mashariki.
   
 5. The Quonquerer

  The Quonquerer JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  I hear you:

  1. Kwa kizazi hiki cha nyoka kinachotafuna nchi hii, kujitoa ni ngumu..hivi vizee havijui kusema 'No'. Utadhani ni machangu wa pale Ohio!
  2. Kama Kenya wanalinda maslahi yao, kwa nini sisi ndio tuwe wa kukubali vipengele ambavyo vinatuathiri, na mbaya zaidi tumeshavisaini. Kwa Kenya kufanya mgomo huu, na sisi ndiio ingekuwa sehemu ya kuchomokea na kukataa vipengele ambavyo 'watalaam wameshasaini blindly!
  I believe this EAC cooperation is doomed!
   
Loading...