Faida ya kuwa mkweli na madhara ya udanganyifu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Mfalme alipoona umri umeenda aliamua kutafuta mtu wa kumrithisha Ufalme wake.

Mfalme alikusanya vijana 10 na akawaambia atawapa mtihani yule atakae faulu ndiyo atakuwa mrithi wake.

Mfalme aliwapa vijana hao mbegu za mahindi na akawaambia kila mmoja aende nazo nyumbani akazioteshe, akawapa muda wa wiki 3 warudi na mbegu hizo zikiwa zimeota.

Katika nyumba moja kijana alishangaa kuona mbegu amezipanda na kumwagilia vizuri lakini hazikuota, alirudia tena hata hivyo hazikuota tena.

Familia walihuzunika sana na marafiki wa kijana huyo walimshauri akanunue mbegu zingine ila wazazi wake wakakataa kwa kumuogopa Mungu.

Baada ya wiki 3 kufika vijana wote walirejea nyumbani kwa mfalme wakiwa na mbegu zikiwa zimeota vizuri na walijipanga mstari na mfalme akaanza kupita akikagua mbegu kwa kila kijana, vijana wote 9 walikuwa wameotesha mbegu zao vizuri isipokuwa kijana mmoja ambaye alikuwa amesimama mwisho kwa wasiwasi na uoga.

Mfalme apomfikia akamuuliza kwanini wewe haukufanikiwa kuotesha mbegu zangu?
Kijana, kwa unyonge akajibu: mfalme mimi nijaribu kuzipanda lakini hazikuota.

Mfalme akacheka na kusema wewe ndio unafaa kuwa mrithi wangu.

Mbegu zote nilizowapa zilikuwa zimechemshwa na mbegu ikichemshwa huwa haioti.

Kwa hiyo wote walioziotesha ni wadanganyifu sasa hatupaswi kuwa na mfalme muongo, mfalme anatakiwa kuwa mkweli na mwaninifu.

Kijana alivishwa taji.

Tunaishi kwenye jamii na watu wenye mafanikio makubwa sana. Wengi wao wapata hayo mafanikio kwa njia zisizo halali.

Wangapi wanasomesha watoto wao kwenye shule za gharama, wana majumba na magari ya kifahari waliyoyapata kwa njia za kishetani na kuna wangapi wana vyeo vya juu kwa vyeti feki.

Pongezi kwa wote waliotumia gharama zao halali kujipatia mafanikio walionayo.

Tafadhali tuweni waamifu kwa Mungu wetu na tutafute riziki kwa njia halali vinginevyo tutaotesha mbegu zilizochemshwa.

Kama umeielewa sema amen na like na kushare kwa wingi bila kusahau like page hii kwa post za vicheksho kila siku.


1572406795744.jpeg
 
Hiyo cartoon image ni baada ya kumvisha ufalme au kabla?, naona kama image inatulaghai kutokana na maelezo ya juu yake.

But story nzuri 👏
 
Back
Top Bottom