Tafsiri ya ndoto za mapenzi ya jinsia moja na hatima ya maisha yako

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Jun 29, 2023
286
582
Kijana mmoja aliniuliza swali akaniambia alikuwa amekwenda sehemu kikazi akawa amechukua chumba cha kulala

Anasema alipolala aliota Ndoto aliota kuna Mkaka anamwingilia kinyume cha maumbile na anamfahamu na aliposhtuka kwenye Ndoto alijiskia Vibaya Sana akaniuliza maana yake nini?

Mosi
Unapandikizwa roho ya mauti ndani yako, ambayo lengo lake ni kuua kile kitu cha thamani ndani yako, kuua Imani yako ,etc

Mambo ya Walawi 20:13 “Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.”

Pili
Unapandikizwa roho ya kukataliwa Au kutengwa na wenzako, neno chukizo ni Jambo ambalo kwa jamii halikubaliki unatengwa na jamii ya kwako.

Mwanzo 43:32 “Wakamwandalia yeye peke yake, na wao peke yao, na wale Wamisri waliokula pamoja naye peke yao; maana Wamisri hawawezi kula pamoja na Waebrania, kwa kuwa ni chukizo kwa Wamisri.

Tatu
Unayang'anywa nafasi yako yakuwa mrithi wa ufalme wa Mbinguni

1 Wakorintho 6:9 “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti”

Nne
Umechafuliwa kiroho, ili uwepo wa Mungu Ukae mbali na wewe, rejea hapo Law 20:13

Tano
Unajulishwa kuna mbegu za ushoga imepandikizwa kwako ambayo isipoondolewa kwa Damu ya Yesu, itachipuka katika Maisha yako ya baadae

Mathayo 5:27-28 “Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.”
 
Namna ya kuombea Ndoto zenye Uzinzi ndani yake

A. Toba
Omba toba juu ya kile kilichopelekea mlango wa ndoto kufunguka na kupitisha Ndoto kwako.

B. Tumia Damu ya Yesu

Nyunyiza Damu ya Yesu ya Agano kwenye lango la Ndoto kwa toba juu ya kile kilichompa adui uhalili kumiliki lango la Ndoto

C. Vunja

Vunja maagano yote ya kipepo ambayo yamepata uhalali kupitia hicho kitendo cha kwenye Ndoto kwa damu ya Yesu

D. Kemea

Kemea mapepo yote ya ushoga na uasherati kwa Jina la Yesu yapate kukuachia katika nafsi, Moyo na mwili

E. Ondoa
Ondoa kila aina ya mbegu za uharibifu ambazo shetani amepanda kwenye Moyo wako , fikra zako na kwenye sehemu za aja kubwa kwa Damu ya Yesu

F. Ombea uponyaji
Ombea uponyaji WA nafsi roho na mwili kwa Damu ya Yesu na kwa Jina la Yesu

G.Omba neema ya Mungu ikusaidie kutengeneza mahusiano yako Kwa upya na Mungu na wanadamu
 
Binafsi yangu, Ndoto hazina maana yoyote ni mang'amung'amu tu, ntaamini katika ndoto kama ndoto yoyote nitakayokuja kuota pale itakuwa yenye mwanzo na mwisho unaoeleweka, na ikijirudia tena na tena. Sio hizi zinaanzia katikati ghafla mwisho haieleweki

Vinginevyo ni movie tu za kichwani, nishaota nyingi sijawahi kutilia maanani na hakuna kilichotokea.
 
Binafsi yangu, Ndoto hazina maana yoyote ni mang'amung'amu tu, ntaamini katika ndoto kama ndoto yoyote nitakayokuja kuota pale itakuwa yenye mwanzo na mwisho unaoeleweka, na ikijirudia tena na tena. Sio hizi zinaanzia katikati ghafla mwisho haieleweki

Vinginevyo ni movie tu za kichwani, nishaota nyingi sijawahi kutilia maanani na hakuna kilichotokea.
Jambo lolote usilolijua umuhimu wake halina faida yoyote kwako, wazazi wetu hawakujua thamani ya dhahabu walikuwa wanachezea kama mawe lakini walipokuja wanaojua dhahabu ni kitu gani? Ndio tulikuja kutambua dhahabu ni kitu gani ? Ni kawaida kabsa kwa kitu ambacho haujui thamani yake kukidharau
 
Mala nyingi unachokiwaza sanaaa ndicho unachoota...


Haiwezekan from no where
Ujiusishi na maswala ya ufiraji na ufirwaji

Hauangalii x video za gays
Hautaman wanaume wenzako afu zen uote unapigwa pu'mb'u Mi nakataaa


Your the one of them:
 
Jambo lolote usilolijua umuhimu wake halina faida yoyote kwako, wazazi wetu hawakujua thamani ya dhahabu walikuwa wanachezea kama mawe lakini walipokuja wanaojua dhahabu ni kitu gani? Ndio tulikuja kutambua dhahabu ni kitu gani ? Ni kawaida kabsa kwa kitu ambacho haujui thamani yake kukidharau
Nimeipa vigezo vya kuiamini, isipokuwa hivyo basi ni mawazo tu na ndio maana ndoto zangu nyingi ni vitu ambavyo naviishi kwenye maisha yangu ya kila siku, na sijaona maana yoyote ile.
 
Hizo ni porojo tu. Ndoto chache sana zina maana nyingi zinakuja kutokana na mawazo na fikra zako.

Kimjaacho mtu ndicho kimtokacho. Ukiwaza mafanikio muda wote utaota mafanikio pia.
 
Back
Top Bottom