Faida ya kitunguu maji katika mwili wa binadamu

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,077
Reaction score
34,848







Kitunguu maji hutibu magonjwa yafuatayo

Kikohozi

Vidonda vya tumbo

Mifupa

Ngozi

Koo

Figo

Tumbo

Mkojo

Matayarisho

Menya vitunguu maji 3 vikubwa, visage au vitwange ili upate maji yake, changanya na maji kidogo yaliyochemka. Chukua punje 3 za Kitunguu Swaumu, mwaga maji ya vitunguu maji juu yake acha mchanganyiko ukae ndani ya bilauri masaa 2, ongeza asali vijiko vikubwa 5.

Tumia kijiko kikubwa kimoja kutwa mara 2 kwa siku 3 au siku 7 inategemea ugonjwa wako jinsi ulivyo na ukubwa wake.

Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili mzizimkavu. Au boonyeza hapa.Mzizi Mkavu


========

 
Wakuu najua labda limeshazunguzwa hili please naomba details.

 
Huoni kwamba kesho atakuja mwingine kudai umuhimu na madhara ya mapera, zambarau, kitunguu saumu, maembe, mapapai, chumvi, asali, majani ya chai, biringanya, pilipili hoho, pilipili kichaa na mengine mengi?
Kuna vitu unaweza google na ukapata maelezo ya kujitosheleza.
Tafakari,chukua hatua.
 


Wiki iliyopita tulianza makala haya kwa kuangalia jinsi kitunguu kinavyoweza kutibu ugonjwa wa kutokwa damu wakati wa kutoa haja kubwa. Katika makala hayo, watu wengi wameonekana kuguswa nayo. Wiki hii, pamoja na mambo mengine, nitakujuza jinsi ya kuitengeneza juisi hiyo.

Halikadhalika katika makala ya leo, utajua magonjwa mengine yanayoweza kutibika kwa kitunguu, iwe kwa kunywa juisi yake au kwa kula kitunguu chenyewe. Kitu kimoja napenda kukuhakikishia kuwa, unayoyasoma hapa kuhusu kitunguu, tayari yalishafanyiwa utatifi na kuthibitishwa na wataalamu waliobobea katika masuala ya vyakula tangu enzi za mababu zetu.

Vile vile, watu wanaoamini lishe kama tiba na kutumia, matokeo yake siku zote huwa dhahiri na wako wengi wanaoweza kuthibitisha jinsi afya zao zilivyo imara leo tofauti na miaka kadhaa iliyopita kabla ya kugundua siri ya chakula kama tiba.

JINSI YA KUTENGENEZA
Kinachotakiwa ni kitunguu maji kimoja cha ukubwa wa wastani ambacho utatengenezea juisi na kupata kiasi cha glasi moja saizi ya kati. Safisha kitunguu chako kwa kuondoa gamba la juu kisha katakata vipande vidogo vidogo ili kurahisisha usagaji.

Kuna njia mbili unazoweza kuzitumia kutengeneza juisi hiyo. Ya kwanza ni ya kisasa ambapo unaweza kutumia blender au juicer, kwa kuweka maji kidogo na kuanza kuisaga hadi kupata juisi. Njia ya pili ni ya kiasili, ambapo utatumia kinu kidogo na maji kidogo kwa kutwangwa hadi kupata juisi.

Ukimaliza kusaga (kwa njia utakayoitumia) kamua na ichuje juisi yako kwa kutumia chujio la kawaida ili kupata juisi pekee ya kitunguu na kuacha masalia ya maganda peke yake. Mara baada ya kuiweka juisi yako kwenye glasi, HAKIKISHA UNAINYWA HAPO HAPO. Hairuhusiwi kuihifadhi au kuinywa baadaye, kwa sababu itapoteza virutubisho vyake muhimu.

Kunywa glasi moja mara moja kwa siku au mara mbili, ukiona tatizo lako ni kubwa. Fanya zoezi hilo la kundaa juisi na kuinywa kwa muda wa siku saba hadi 14.
Kama nilivyoeleza wiki jana, hali ya kuchafuka kwa tumbo na kujisikia vibaya baada ya kunywa, isikuogopeshe, baadaye utaizoea na utajisikia vizuri zaidi.

Mbali ya kutibu tatizo la kusikia maumivu na kutokwa na damu wakati wa kwenda haja kubwa (Hemorrhoids au piles), juisi hiyo pia itatoa ahueni au kinga kubwa dhidi ya matatizo mengine ya kiafya yafuatayo:
Pumu, mafua, magonjwa ya kuambukizwa na bakteria, matatizo ya kupumua kwa shida, kiungulia na kutapika.

Itaongeza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa nyemelezi, vile vile kwa kutafuna vitunguu vibichi na kukaanavyo mdomoni kwa sekunde kadhaa, kutaua bakteria wote wa kinywani na kutoa kinga dhidi ya kuoza kwa meno na kuondoa harufu mbaya.

Ulaji wa vitunguu maji vibichi mara kwa mara, hulainisha damu na kuzuia kuganda ambako husababisha mishipa kuziba na kusababisha magonjwa ya moyo, ikiwemo presha ya kupanda.

Juisi ya kitunguu ni dawa mara moja ya kuzuia kutapika, mtu anayetapika mfululizo akinywa juisi ya kitunguu, hupata nafuu haraka. Vile vile juisi hii ni dawa ya tumbo linalouma na hutoa kinga dhidi ya magonjwa ya uvimbe tumboni.

Kama unasumbuliwa na chunusi, pakaa juisi ya kitunguu iliyochanganywa na asali sehemu yenye chunusi vitaondoka na kukuacha na ngozi nyororo. Chukua kiasi kidogo cha juisi na kijiko kimoja kidogo cha asali changanya kisha pakaa.

Juisi ya kitunguu pia ni dawa ya kutibu majeraha ya kuumwa na nyuki. Kama unapata maumivu wakati wa haja ndogo au unatoa mkojo mchafu sana, kunywa maji mengi yaliyochanganywa na juisi ya kitunguu kiasi kidogo, tatizo litakwisha.

Juisi ya kitunguu ina virutubisho vyenye uwezo wa kudhibiti chembechembe hai za mwili zenye kansa na hivyo kuwa kinga nzuri dhidi ya ugonjwa wa saratani (cancer).

Ulaji wa vitunguu au juisi pia hutoa ahueni kwa mgonjwa wa kifua kikuu. Juisi iliyopashwa moto pia ni dawa ya sikio linalouma. Weka matone mawili tu kwa kila sikio linalouma.

Juisi ya kitunguu pia ni dawa ya majeraha yatokanayo na moto. Ukiungua, pakaa juisi hiyo sehemu zilozoungua kwa nafuu ya haraka. Pia kitunguu ni dawa ya mbu, pondaponda vitunguu, kisha jipakae sehemu za miguu na mikono - mbu hawatakugusa.

Faida za kitunguu na juisi yake ziko nyingi na zote ni muhimu kwa ustawi wa afya zetu. Nakushauri kuanzia leo, kunywa juisi hiyo au kula kitunguu katika kila mlo kwa jili ya kutibu maradhi uliyonayo au kwa kuupa mwili wako kinga imara, na kamwe hutajuta!
 
Wiki iliyopita tulianza makala haya kwa kuangalia jinsi kitunguu kinavyoweza kutibu ugonjwa wa kutokwa damu wakati wa kutoa haja kubwa. Katika makala hayo, watu wengi wameonekana kuguswa nayo. Wiki hii, pamoja na mambo mengine, nitakujuza jinsi ya kuitengeneza juisi hiyo.
 
Hii nimeona sehemu moja nilikuwa na raia wa Misri walikuwa wanakula sasa vitunguu sana vibichi..

Na mimi nikawa najaribu mpaka nimezoea saizi kila mlo wangu lazima vitunguu viwepo..tunakuombea dua MziziMkavu
 
Swadacta.... Hakuna shaka hata kidogo. Ukienda India (South India.....Madras, Mysore, Bangalore nk) kila mlo utakuta wanakuwekea na vitunguu kibao wee utafuneee ili upate japo faida hata moja.

Big up!
 
Mzizi mkavu big up,sijui kama ulisha wahi kutaja tiba ya presha ya kupanda kama ulishawahi mimi ilinipita.

mimi nilikuwa nataka ya kupunguza unene....mzizi ulishaleta hiyo...?.....kama bado hebu nitupie......
 
Mzizi mkavu big up,sijui kama ulisha wahi kutaja tiba ya presha ya kupanda kama ulishawahi mimi ilinipita.

Dawa ya pressure kwa jumla (imewafaa watu wengi), ni majani ya mbaazi

>yaliokua bado machanga. Chukua kiasi majani 4 mpaka matano hivi na

>utafune tafune huku unameza mate, kisha majani yatupe baadae, usimeze.

>Tumia kwa muda wa

> siku mbili au tatu hivi na baadae ukapime. Inshaallah utahisi

>upungufu mkubwa.

>Usiendelee kutafuna kwa muda wa masiku mengi bila ya kupima, kwani

>huenda pressure ikashuka sana.

>Mwenye ugonjwa huu jaribu kutumia, kwani haina madhara yoyote yale.

>Kuna watu wa karibu sana na mie wametumia na imewafaa sana. Walikua

>vidonge haviwatoki na baadae wakaacha kabisa, mpaka madakitari

>walistaajabu ni dawa gani wametumia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…