Faida tutakazopata kama tukitumia vizuri utajiri wa Makabila

Status
Not open for further replies.

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,339
UTAJIRI WA MAKABILA TUKIUTUMIA VIZURI...

Tuna zaidi makabila 120.

Iwapo:
- Tutajikita kuandika vitabu vinavyoelezea historia na tamaduni za kila kabila, tutajikuta tuna zaidi ya vitabu 120 vya kuuzwa ndani na nje ya nchi.

- Tutajikita kuandika kamusi za kila kabila tutajikuta tuna kamusi zaidi ya 120 tunazoweza kuuza ndani na nje ya nchi.

- Tutajikita kuandaa makumbusho za gharama ndogo katika kila eneo linalopatikana kabila husika, tutajikuta tuna zaidi ya makumbusho/maeneo ya maonesho 120.

- Tutajikita kuendeleza sanaa zinazopatikana katika kila kabila(iwapo kila kabila lina sanaa zinazojitegemea), tutajikuta tuna zaidi ya sanaa 120.

- Tutajikita kuendeleza michezo inayopatikana katika kila kabila (iwapo kila kabila lina michezo yake), tutajikuta tuna zaidi ya michezo 120.

- Tutajikita kuendeleza mapishi (iwapo kila kabila lina mapishi yake), tutajikuta tuna zaidi ya mapishi 120.

- Tutajikita kuendeleza methali, hadithi, misemo na vitendawili katika kila kabila, tutakuwa matajiri wa fasihi simulizi.

- Tutachukua mila nzuri katika kila kabila na kuziendeleza, tutakuwa Taifa lenye ustaarabu mkubwa mno.

Iwapo! Iwapo! Iwapo! Iwapo!
 
ndo maana ukajiita kasomi,nimekupata sana.tutatengeneza ajira za kutosha Sana,na kuingiza dolar za kutosha.waziri wa habari,michezo na utamaduni ,MH.bashungwa,najua umo humu,chukua hii kitu.
 
Makabila matajili tz ni haya wanyakyusa, wachaga, wahaya, wakinga wengine wanasindikiza tu, nimechomekea hili ili mjue
 
Hicho kitu hakiwezekani na hata kikiwezekana hakitofika mbali.

Sababu ni dunia kuwekeza kwenye technology na science zaidi na tafiti nyingi ambazo in the future ndio zitakuwa mkombozi kwa human specie survival hence continuity.

For instance global warming kitu ambacho ni inevitable right now due to human activities.
Hivyo watu kama elon wanawekeza kwenye carbon capture technology sababu the consequences of that thing are deadly.
Considering Africa ndio tutakuwa waathirika wakubwa.

I'm not saying that's a bad idea, No.
But what I'm saying ni kwamba hiyo idea haitopata attention itakayopelekea kupata any success or any noble benefits in the country.

Nilikuwa nabishana na mtu mmoja YouTube definitely ni mmarekani or something ila sio mwafrika.
Akasema kwamba in 2100 asilimia kubwa ya africans watakuwa flee to other countries due to climate change sababu our greatest land africa uwezo wake wa kuzalisha chakula utapungua.
Nikamwambia hicho kitu hakitatokea sisi africans tutatafuta njia za kuzalisha chakula in such circumstance and our scientists watatafuta njia za kuneutralise hilo tatizo.

Nilibisha even najua alikuwa sahihi kwa asilimia 50 na africans hawawezi kusolve hilo tatizo kama mpaka leo tumeshindwa kusolve tatizo la maji safi nchi nzima na badala ya kutafuta chanjo africans walikesha kuomba na kujifukiza.
 
Kweli mkuu hii itasaidia sana inatakiwa serikali iliangalie hili
 
Makabila matajili tz ni haya wanyakyusa, wachaga, wahaya, wakinga wengine wanasindikiza tu, nimechomekea hili ili mjue
Upo sahihi kiasi kila kabila lina utajiri wake pengine wewe umeegemea utajiri wa aina moja.
Ila ukiingia ndani kila kabila na utajiri wake.
 
Hicho kitu hakiwezekani na hata kikiwezekana hakitofika mbali.

Sababu ni dunia kuwekeza kwenye technology na science zaidi na tafiti nyingi ambazo in the future ndio zitakuwa mkombozi kwa human specie survival hence continuity.

For instance global warming kitu ambacho ni inevitable right now due to human activities.
Hivyo watu kama elon wanawekeza kwenye carbon capture technology sababu the consequences of that thing are deadly.
Considering Africa ndio tutakuwa waathirika wakubwa.

I'm not saying that's a bad idea, No.
But what I'm saying ni kwamba hiyo idea haitopata attention itakayopelekea kupata any success or any noble benefits in the country.

Nilikuwa nabishana na mtu mmoja YouTube definitely ni mmarekani or something ila sio mwafrika.
Akasema kwamba in 2100 asilimia kubwa ya africans watakuwa flee to other countries due to climate change sababu our greatest land africa uwezo wake wa kuzalisha chakula utapungua.
Nikamwambia hicho kitu hakitatokea sisi africans tutatafuta njia za kuzalisha chakula in such circumstance and our scientists watatafuta njia za kuneutralise hilo tatizo.

Nilibisha even najua alikuwa sahihi kwa asilimia 50 na africans hawawezi kusolve hilo tatizo kama mpaka leo tumeshindwa kusolve tatizo la maji safi nchi nzima na badala ya kutafuta chanjo africans walikesha kuomba na kujifukiza.
Nimekuelewa vizuri sana mkuu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom