Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,036
- 20,342
UTAJIRI WA MAKABILA TUKIUTUMIA VIZURI...
Tuna zaidi makabila 120.
Iwapo:
- Tutajikita kuandika vitabu vinavyoelezea historia na tamaduni za kila kabila, tutajikuta tuna zaidi ya vitabu 120 vya kuuzwa ndani na nje ya nchi.
- Tutajikita kuandika kamusi za kila kabila tutajikuta tuna kamusi zaidi ya 120 tunazoweza kuuza ndani na nje ya nchi.
- Tutajikita kuandaa makumbusho za gharama ndogo katika kila eneo linalopatikana kabila husika, tutajikuta tuna zaidi ya makumbusho/maeneo ya maonesho 120.
- Tutajikita kuendeleza sanaa zinazopatikana katika kila kabila(iwapo kila kabila lina sanaa zinazojitegemea), tutajikuta tuna zaidi ya sanaa 120.
- Tutajikita kuendeleza michezo inayopatikana katika kila kabila (iwapo kila kabila lina michezo yake), tutajikuta tuna zaidi ya michezo 120.
- Tutajikita kuendeleza mapishi (iwapo kila kabila lina mapishi yake), tutajikuta tuna zaidi ya mapishi 120.
- Tutajikita kuendeleza methali, hadithi, misemo na vitendawili katika kila kabila, tutakuwa matajiri wa fasihi simulizi.
- Tutachukua mila nzuri katika kila kabila na kuziendeleza, tutakuwa Taifa lenye ustaarabu mkubwa mno.
Iwapo! Iwapo! Iwapo! Iwapo!