Faida Tano (5) za kusema ukweli

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,700
"Kusema maneno ya UONGO ni kazi rahisi sana ila kuulinda UONGO ni kazi ngumu sana."

"Waweza kudanganya kila kitu kwa kila mtu tena kwa urahisi sana ila kuulinda huo uongo ni kazi ngumu sana."

"Tambua ya kuwa hakuna uongo ambao unadumu milele, bali kila uongo huwa kuna siku unafahamika na hapo ndipo heshima ya mtu ushuka."

"Iko hivi, waweza ukawa unawadanganya watu mambo fulani ambayo hauna kwa kudhani ya kwamba unajijengea heshima kwao, ila tambua ya kuwa siku watakapofahamu UKWELI kukuhusu heshima yako itashuka na utajipotezea uaminifu (kuaminiwa), na hata kama pengine utawaambia jambo la ukweli hawatakuamini tena."

"Usiseme uongo kwa kigezo cha kumtaka binti au mkaka hawe mpenzi wako, maana siku hatakapofahamu ukweli kukuhusu utajiharibia, na tena utajipunguzia uaminifu, hivyo mweleze ukweli wote kuhusu maisha yako arafu yeye mwenyewe ataamua hawe na wewe au akatae."

"Maana mahusiano mengi ya kimapenzi yameishia njiani kwa sababu tu ya wahusika kudanganyana kuhusu maisha yao harisi."

"Lakini pia usiseme uongo kwa kuongozwa na TAMAA ya mali, maana tamaa mbele mauti nyuma, na tamaa ikichukua mimba uzaa DHAMBI, na ile dhambi uzaa MAUTI, kwa hiyo ruhusu watu wakukubari kwa kile ulichonacho yaani kile ulichojariwa na Mwenyezi MUNGU. (Yakobo 1:14-15)."

Ndugu yangu kwa kusema kwako ukweli zipo faida nyingi ambazo utazipata, ambazo ni hizi:-

Moja; Utatambua ni mtu gani ambae ni sahihi kwako, na mwenye UPENDO wa kweli kwako wenda ni mpenzi, ndugu au rafiki. maana yawezekana kuna watu watakuja kujishikisha kwako kwa sababu ya uongo wako, hivyo basi kama utakuwa mkweli utawatambua wapi watu sahihi kwako na wapi ambao si watu sahihi kwako.

Mbili; Utajiepusha na mizinga isiyokuwa na sababu, toka kwa mpenzi wako yaani mfano unadanganya wafanya kazi Airport ni manager wakati hata kazi hauna hivyo utakapopigwa kizinga cha elfu 50 ukasema hauna utaonekana wa ajabu sana maana profile yako haiendani na ulichojibu. Hivyo ili kuepuka mizingia iliyo nje ya uwezo wako jifunze kuwa mkweli.

Tatu; Utailinda HESHIMA yako, yaani kama utasema ukweli basi utakuwa umeilinda heshima yako kuanzia Leo, kesho na siku zote, hivyo hiyo ndio faida ya kusema ukweli maana status yako itazidi kukua ila kama utadanganya basi jiandae kushuhudia status yako ikiporomoka pale watu watakapofahamu maisha yako harisi . Hivyo sema kweli ndugu.

Nne; Utajiepusha na maisha ya maigizo, kwa maana kwamba watu wengi wameishi maisha yasiyokuwa yao yaani maisha ya kuigiza (fake-life) kwa sababu ya uongo wao tu, na maisha hayo yamewafanya waishi kama watumwa, hivyo kama unapenda usiwe na maisha ya maigizo jifunze kusema KWELI.

Tano; Utajiepusha na migogoro kati yako na wanadamu wenzako, naam, pale unapodanganya arafu watu wakafahamu si wote watakuvungia, bali wapo ambao watakuambia ulichofanya si kizuri, na pia wapo ambao watajitenga na wewe, hivyo ili kuyaepuka hayo basi amua kusema ukweli."

Hizo ndizo faida tano (5) nilizokuandalia leo ndugu yangu na imani kwa msaada wa Mungu zitabadirisha maisha yako.

"ACHA UONGO, SEMA UKWELI NDUGU YANGU, MAANA UONGO NI CHANZO CHA MIGOGORO MINGI NDANI YA JAMII."
 
Ukiwa mkweli wala huitaji kuwa na kumbukumbu.

Madhara ya uongo unaweza kuyashuhudia kwa Magufuli, alikuwa bingwa wa uongo na ulaghai lakini sasa hivi ukweli wote uko wazi.
 
Ukweli hukuweka huru,ukiwa muongo wakati mwingine hata kujiamini kunapotea kabisa...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom