Faida 5 za kuwa na muda wa peke yako wa kutafakari

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,910
6,706
I.
Tangu enzi na enzi, binadamu wamekuwa wakipata maono makubwa na ya tofauti, kupata suluhisho la matatizo yao makubwa na hata kujitambua wao wenyewe baada ya kupata muda wa kuwa peke yao.

Kuanzia wanafalsafa, wanasayansi, watu wa Imani na hata viongozi, waliweza kufanya makubwa waliyofanya baada ya kupata muda wa kuwa peke yao wa kutafakari mawazo yao, kwa kuondokana kabisa na usumbufu wa makelele kutoka kwa watu wengine.

Tukianzia kwa watu wa Imani, soma historia za viongozi wote wa kiimani, kuanzia YESU KRISTO, MOHAMED, BUDHA na wengineo, walibadilika kutoka katika maisha yao ya kawaida na kuwa watu wa Imani kubwa baada ya kupata muda wa kuwa peke yao katika kutafakari.

Imeandikwa katika vitabu vya Dini YESU KRISTO alienda milimani kufunga na kuwa peke yake, kadhalika MUHAMMAD na hata BUDHA pamoja na kukulia kwenye maisha ya kifahari, hakupata uamsho mpaka pale alipoenda porini na kupata muda wa kukaa peke yake kwa kutafakari ndio alipata uamsho mkubwa.

Tukija kwa wanasayansi, wanafalsafa na waandishi wakubwa waliweza kuja na mawazo yao bora kuhusu maisha baada ya kupata muda wa kukaa peke yao na kutafakari. Wanafalsafa na waandishi wengi waliweza kuja na njia bora za kuishi na suluhisho la matatizo mbalimbali baada yakujifungia wenyewe kwa kipindi fulani katika mazingira ya utulivu.

Mfano mwanasayansi Newton aligundua sheria ya mvutano akiwa amekaa peke yake chini ya mti kwa kuangalia tunda likianguka. Kadhalika mwanasayansi Albert Einstein aliweza kuja na kanuni bora kabisa za kisayansi kwa kuwa na muda wa kukaa peke yake na kutafakari.

Na hata viongozi bora wa kisiasa kuwahi kutokea duniani, ambao waliweza kuendesha nchi zao na kuvuka magumu na changamoto mbalimbali, walihakikisha wanakuwa na muda wa kukaa peke yao huku wakitafakari.

Zifuatazo ni faida ambazo kila mtu anaweza kuzipata kwa kutenga muda wa kuwa peke yake akizungumza na mawazo yake.

Inakusaidia Kupata mawazo mapya.

Unapokaa peke yako, hakuna usumbufu au kelele zozote zinazoingia kwenye akili yako, hivyo akili yako inaweza kufikiri na kuja na mawazo mapya. Hivi ndivyo watu wamekuwa
wakigundua vitu vipya, kwa sababu akili zao zinakuwa hazijatingwa na usumbufu wa mambo mengi.

Inakusaidia kujitambua wewe
mwenyewe.

Huwezi kujitambua wewe mwenyewe bila ya kupata muda wa kuwa peke yako wa kutafakari. Unapopata muda wa kuwa peke yako ni rahisi kujihoji na kujitathimini kwa kila unalofanya na kuona matokeo unayopata, madhaifu yako na uimara wako.

Inakusaidia kuwa na mahusiano bora na watu wengine.

Huwezi kujua umuhimu wa wengine kwenye maisha yako kama hupati muda
wa kuwa peke yako. Ni kupitia muda wa upweke ndiyo unajua umuhimu wa wengine kwenye maisha yako. Pia unapojitambua wewe mwenyewe, mahusiano yako na wengine yanakuwa bora zaidi.

Inakusaidia Kutatua matatizo yako magumu.

Matatizo magumu katika maisha yako yanahitaji utulivu mkubwa katika kuyatatua, hivyo unapokuwa na muda wa peke yako wa kutafakari inakusaidia kuyaelewa matatizo yako na njia za kuyatatua matatizo yako magumu yanayokukabili.

Inakusaidia Kudhibiti hisia zako.

Hisia zimekuwa changamoto kwa watu wengi, matatizo mengi ambayo watu wanakutana nayo kwenye maisha yao yanaanza na hisia zao wenyewe, hasa pale ambapo zinashindwa kudhibitiwa. Unapopata muda wa kuwa peke yako wa kutafakari unaweza kuzikagua hisia zako na kujua kichocheo chake na jinsi ya kuzidhibiti zisikuletee madhara katika maisha yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SOURCE...?
 
Kuna faida sana ya kukaa peke yako ili uweze kufikiri vitu vingi ila baadhi ya wabongo utashangaa wanakuita mbinafsi mara mchoyo bila kujua faida unayopata ukiwa peke yako
 
Ni kwel,mfano mimi kukaa peke yangu kumeshanifanya nipangilie vitu vyangu vizuri na kutatua changamoto mbalimbali za kiufundi kwenye kitu kinachotakiwa kuwekwa kwenye ubora,
 
Back
Top Bottom