Fahari ya CCM - mgoma ikivuma sana...... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fahari ya CCM - mgoma ikivuma sana......

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Oct 28, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG] [​IMG][​IMG]

  Mficha maradhi mwisho humwumbua. Yalisemwa, yanasemwa na viongozi wa juu wameamua yaendelee kama yalivyo kwani kuyafanyia kazi inawawia vigumu kwa kuwa wahusika ni wao na kila wanakogeukia wanajitazama wao wenyewe, sawa na hadithi ya nyani utamwonea huruma kumpiga atakavyoonyesha huruma wakati akikuibia mahindi yako, lakini kesho utakaporudi kushuhudia mabua tu shambani ndipo utakapojawa na simanzi lisilo kifani.

  Kama kuna wenye malengo ya kukalia Ikulu kwa mwendo huu inatia shaka ushupavu walio nao, maana kuna kila dalili ya mgawanyiko, hawa ni vijana wenye ile motomoto wanaolipuka kwa kasi kama moto wa gas, lakini kuna kundi jingine ambalo halionyeshi hamasa kwa uwazi ile yamebaki moyoni mwao, nini watafanya kwa yanayojilia wao wenyewe ni siri yao wanajua. Bora anayeonyesha kwa uwazi una nafasi ya kumsoma na kutafuta tahadhari, lakini kwa wenye kuficha hisia zao ipo siku itabaki duwazo lisilotabirika.
   
 2. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  Vita ya panzi neema ya kunguru.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Yalipotokea haya wangeweza kusoma ishara za nyakati, lakini wakaona ni upepo unaovuma kwa muda na utatulia wenyewe, lakini sasa upepo huo umegeuka kuwa upepo wa kisulisuli.
   
 4. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  kiukweli makundi ndani ya ccm yanaua chama. Ridhiwani na kundi lake kulia na kundi la malisa kushoto. ritz anataka Lowassa asipite huku malisa akitaka apite, humo humo ndani sitta ana kundi lake, membe nae analo huku kikwete analo yaani ukidadisi ni mkanganyiko unaoishia watu kupigana mchana kweupe.

  but ni aibu sana sana mtu hadi kupigana kisa tu fulan apitishwe ambaye hujui kama akipita atachaguliwa kuwa raisi?????

  ila ukiangalia kwa umakini zaid utagundua ccm imeshikwa na watu wachache wye pesa zao ambao wanataka wasikike tu ila wanyonge hawapewi nafasi kabisa.

  naurudia msemo wangu kwamba mtu wa kuongoza serikali ya tanzania hayuko ndani ya siasa hizi yuko pembeni kabisaaa manake waliopo wameweza kufanya nn hadi sasa?
   
 5. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Chama cha Matajiri hicho, maskini kamwe hawezi kufurukuta.
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Yes, lakini usiguse huko kwa Ridhiwani maana utatonesha kidonda watatwangana zaidi si waona wameshajimilikisha Chama cha kifamilia? Bagamoyo ndo kabisa asiyemwanaukoo haingizi pua.
   
 7. GEMBESON

  GEMBESON JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 256
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hii nyuzi ningefurahi kama Ingetupiwa kwenye jukwaa la Siasa. Japokuwa ngumi jukwaa lake ni hili. Hongereni wana CCM kumbe ngumi nanyi mnaziweza!. Yetu macho tu.
   
 8. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  yaani kiongozi, huyu Ridhiwan hana anachoweza kumtisha mtu makini milele, unless uwe ni mtu mwoga. Namshangaa sana katibu mkuu anayoruhusu mtoto mdogo kama huyu achafue chama to this extent hata kama umri unamruhusu kuwa ndani ya siasa. hapa naona wote wanaoruhusu haya ni kwasabbau tu ya kuomba omba ugali huko kwa kikwete ila mtu makin anayefanya kzi pasi kutegemea mgongo wa mtu lazima asingekubali haya

  tizama wanavyopigana vijana kisa makundi aloyaweka yeye, sisemi uongo Malisa pamoja kijana mmoja aitwae Juma walikuwa marafiki sana wa ridhiwani enzi hizo. lkn ona leo wamebaki kuwa kama maadui kisa siasa chafu za CCM? Juma ashukuru tu ni mtumish wa umma manake nae angeangukia pua kama malisa.

  nani asiyejua nguvu aliyokuwa nayo Lowasa ndani ya ccm? nani asiyejua alivyopigana ili kikwete ashinde? nani asiyejua kwamba ndie mtu akisimamishwa anaweza kuchuana na wapinzani zain yake Lowassa? sasa rizi akileta mambo ya raisi lazima awe mbagamoyo huu sio usultani. anawafanya wanachama makini wa ccm kukichukia chama bureeee.
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Good approach!
  Jambo moja nasema mambo haya yanafikia kwenye ukuta kutoka mbio za sakafuni. Kila jitihada zinashindikana. Yatokeayo ni sawa na ile habari ya kwenye msahafu inayoelezea wairaq nchini Iraq kwa wakati huo walijulikana kama wababilonia. Waliamua kujenga mnara mrefu unaofika mbinguni iliwa wawe wanakwenda mbinguni kusalimia na kurudi duniani. Upeo wao uliifikia hapo bila kukuja mapana na marefu ya Muumba.

  Kwa kuwa walikuwa wanafanya kitu kisicho na akili na kupoteza mali ambayo ingefaa kwa maendeleo ya binadamu wenzao Mungu aliamua kufanya jambo moja dogo sana kuwachafulia lugha wasielewane. Ikawa fundi anapoita udongo wanamletea tofali, anapoita maji wanamletea kamba, basi mambo ni mkorogano tu hadi kufikia kutoelewana wakafarakana. Huo ukawa ndio mwisho wa ndoto za kujenga mnara wa kufirkirika kwa wababilonia.

  Je, yanayoendelea huko CCM yanatofautiana na yale ya wababilonia?
   
 10. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Candid Scope haihitaj mchambuzi kama dr Rwaitama kuja kutudadavulia haya, kiukweli CCM inajikoroga sana tu, na haya yote ni kwasababu ya vyeo ambavyo wanavitaka vya kubebana na kulindana.

  wafikiri hatuji jinsi ambavyo kikwete anahaha kuhusu mali zake alizozipata kwa njia za wizi? wafikiri hatujui jinsi ambavyo ridhiwan anataka abaki kwenye system maisha yake yote? hebu angalia hii familia inavyoitia aibu hadi mkwe anakuwa miongoni mwa wajumbe wa nec?

  binafsi nakipenda sana sana chama cha CCM na daima sio mnafiki katika maslah ya chama. sasa kikwete na familia yake anaua hiki chama na soon ccm itafikia mwisho wake isipokuwa makini.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hii ndio mpya kabisa kwangu eti hata mkwe aingizwe kwenye NEC hapa wamefika pabaya zaidi.
  Wote wanaoonekana kuwa kinyume cha CCM walikuwa wanaCCM wazuri tu, mambo kama hayo ndiyo yaliyowakatisha tamaa. Leo mlala hoi usitegemee kupata nafasi ndani ya CCM, chama kimebaki cha wenye majina kwa kurithishana kama mbio za kupokezana vijiti.

  Imefikia mahala watu wameona maisha yao mafanikio hayako CCM tu, na wengine wameamua kubaki kama walivyozoea miaka nenda rudi kutofungamana na chama fulani ila kuwa tayari kupigia kura chama chenye kuonyesha matumaini kwa maisha ya watanzania ingawa hakuna chama ambacho 100% perfect, lakini kuna kilicho nafuu kuleta matumaini.

  Mbaya zaidi Chama kuhodhiwa na familia na wachache wenye pesa, tumefika pabaya. Hawa wanaopigana kuna machungu ndani ya mioyo yao. Kwa vile upeo wao ni pale CCM tu wanaona ugumu kubandukana nayo, lakini kuna kila dalili kuna walio CCM damudamu haya ndiyo yanayowapata hadi kufikia kuchaniana nguo hadharani.
   
 12. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  lakin Candid Scope hadi ukiona mtu anapigana kisa siasa basi mtu huyu hana njia nyingine ya kumudu maisha zaid ya hizo posho za chama baasi. ila wanachama werevu anakuwa kazi zake chama anakihudumia kama kitu cha ziada tu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  We utashinda nje ya ukumbi wa mikutano ukisubiria wakuu watoke ndipo userebuke nao, huna cha kufanya? Hapo kama ulivyosema bila ubishi hawana njia nyingine za kuendesha maisha na CCM imewapaka kiwi macho na kudumaza ubongo wanashindwa kuwa wabunifu wa kuendesha maisha yao. Hayo ndiyo ninayoyakataa kuwa mtumwa wa vyama vya siasa, inafikia mtu unakuwa shabiki kama wa timu ya mpira vile, na hata goli halali utaona ni makosa kwa sababu ya upenzi wa timu yako. Mambo ya siasa yakendekezwa kwa mtindo huu ndio kufikia kunyofoana pua kama wanyama wa porini wasio na utashi.

  CCM ni sawa na nchi za kibepari ambazo zina mfumo wa kupanga matumizi ya wafanyakazi wake ili waendelee kuwategemea maisha yote hadi wakatakapo staafu kwa manufaa ya wao matajiri. Cha kushangaza hata vijana waliosoma wametumbukia katika mchezo huu mchafu wa CCM pamoja na green lights kuanza kuashiria kugeuka kuwa yellow kwenye traffic lights.
   
 14. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #14
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  tatizo vijana wa kibongo wanapenda maisha mdondo sana tu, kwan hujawah kuskia mtu anatapeliwa kiulaini kisa tu anafikiri anaweza kutajrika kiurahisi?

  mtu anayetapeliwa kisa tamaa ya kupata hela kiulaini hana tofauti na kijana wa ccm anayekaa nje kusubiria mgombea wake atoke ili aserebuk nae akihisi kwamba huyo mgombea wake atamrahisishia maisha. lakin akasahau kwamba huyu mgombea anaweza hata asijerudi kumpa asante.
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Yes, vijana wengi wako kama vile wale wafanyakazi wa restaurant wanaotamani mteja awaachie tip mezani wanapokusanya vyombo vilivyotumika, hii haina uhakika wala kufanya uhesabu sehemu ya pato. Zaidi inamfanya mtu kuwa mtumwa zaidi na kuzidi kupoteza uhuru wake. Mteja asiyeachia tip kutochangamkiwa kwa masilahi binafsi ya mhudumu bila kuangalia dhamana ya restaurant iliyomwajiri itaendeleaje.

  Hizi offer hatari sana, bora kupigania maisha kivyako, ukipatacho tokana na jasho lako unajivunia kulia kivulini, kuliko vya dezo vinavyoleta hata kuhatarisha maisha na kuchapana makonde hadharani bila aibu.

  Utumwa mambo leo tunaosemaga ndio huu
  gfsonwin.
   
 16. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #16
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  ukitaka kujua hawa vijana ni wajinga ona riziwan mungu mtu wao hayupo wala hakupigana, wala hata malisa na nnauye ila wao utafikiri ni askari walinzi wa nchi hii.

  CCM imelea vijana vibaya sana sana, hebu angalia vijana waliochaguliwa kuwa wakuu wa wilaya, kila mmoja anapewa fadhila ama alikifagilia chama alipokuwa mwanahabari ama alijitoa kufanya kampeni.

  kibaya zaid mwenyekiti wa taifa anasemea si jambo zuri kununua kura ili hali anajua watu wamenunua, kwani wasinge ahirisha uchaguzi huo???tena anaongea huku anacheka eti tunakipeleka chama sio kuzuri sana. mnaweza kuchukiana kisa tu huyu kagombea nafasi yako lkn misichukie wale wasiokupa kura??? unapata connection na hii statement?? kwakweli chama hiki kinauliwa na viongozi, manake wanajua kabisa chama kinasemwa kwamba iuongozi unanunuliwa sasa kama wanayasikia kwann wasiache ili wajipange upya?
   
 17. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #17
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tatizo la viongozi ni utumwa wa mali badala ya kutumikia wananchi. Mtu akishatumbukia kwenye utumwa wa mali katu hataona dhamani ya cho chake zaidi ya kupata mali. Nakumbuka niliyosoma kwenye kitabu nikiwa bado darasa la tatu na kusikia kipindi kile kikirudiwa redioni kwamba "zaidi mtu apatavyo ndivyo atamanivyo!"
   
Loading...