Fahari wawili hawakai zizi moja

Fahari wawili hawakai zizi moja

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,805
Reaction score
43,230
Habari ya mchana MMU,

Its a true story, it happens to me, Kasie mie.... anyways iko hivi:

Wakati nasoma Sekondari, O-level, moja ya masomo niliyokuwa nasoma ni Physics na Chemistry, na kwa wakati ule wa Mwinyi ukiwa unasoma hayo masomo tuition inahusika ili kuyakazia mkazo masomo ukimbie C,D na F kwenye mitihani, tuition ya physics nilikuwa nafanya kwa mwalimu Mkichwe Jumamosi. Sasa pale tuition tukawa tunakutana vijana kibao wa shule mbali mbali wasichana kwa wavulana kila mtu akitaka kupata elimu akapasue shuleni kwao.

Tuition, haikuwa tuition tuu na kijiwe cha umbea pia, hivi na vile na hivi viliongelewa kila Jumamosi watu tukikutana
Sasa kuna kijana mmoja alikuwa anasoma shaban robert, yaani hapo tuition tulikuwa tunamuita wa mnato coz alikuwa anajiskia na hakuwa na story sana na watu, most of time he was alone alone.

Maisha yakaenda yakarudi kila mtu alisambaraika kivyake, huku na huku bana, nikakutana na huyu jamaa kwenye harusi moja hivi tukashangaana nini na nini kila mtu akishangaa mwenzie amebadilika, kosa lililofanyika kwenye hiyo harusi kila mtu alikuja mwenyewe mwenyewe tukajikuta tumekaa meza moja tumestorisha mziki tukacheza pamoja na baada ya harusi kuisha tukakubaliana kwenda club tuongee na kucheza, na ilikuwa hivyo.

Baada hapo kila mtu alirudi kwake na tukaanza kuwasiliana through wasap na phone calls, it was a date, we ended up kissing but we didnt reach the intercourse. Na nashukuru mungu kwa hilo, kumbe alikuwa mambo ya mnato na kujiskia hajaacha, hakujua Kasinde nae ni kiburi mwisho wa reli, mhehe haoni ndani. Siku moja akaniambia naomba tukutane lunch nikatoka akaniambia amepata kazi nchi za uarabuni so anaondoka soonest coz document zilichelewa kumfikia na akatakiwa kuondoka immediately. Hapo ndo tulipo kiss na siku anaondoka sikwenda airport kumsindikiza was a bit tight na ilikuwa muda wa kazi. Kumbe jamaa ali mind why sikuenda msindikiza, mie sikuona sissue was busy na nilimwambia nikajua kanielewa kumbe kaweka rohoni.

Kufika Dubai kijana mnato tukaendelea na mawasiliano ila yakawa yanalega sasa mie nikawa naendeleza converation siku moja nikaamua kumlia cobis, yeye ana text dry nami natext dry huwezi amini, ndo vimeishi hivyoo till todate hatujawasiliana tena hadi leo, nikajisemea moyoni, UKINIONA WA NINI NAMI NAKUONA WA KAZI GANI.

Yeye fahari anataka kubembelezwa, kakutana na fahari Kasie popo, mkesha club usiku, mla ujana, aliyeshindikana na familia ndo kabisaaa habari ya kubembeleza haipo kwangu. Nimekumbuka tuu leo habari yake, wakati huo anaenda Dubai was year 2012.
IVO, 100

Regards,

Kasie.
 
Bt m naona kama unajihakiki tu bt we ndo imekuuma mpaka kuandika hapa....kiukweli imekuuma ila unajifariji kwa maneno na kutafuta suport ya watu umu wakufariji kwa yalokutokea

hahahaha hata mie naona hivyo aissee jamani!!!
Alijuaje kuwa kaeka rohoni suala lile?? Je alimtamkia??
Yeye ndo imemuuma bhana asiwe anafikiria lililo ndani ya moyo wa mwenzie!!
 
Umeniongezea uelewa mwingine .... Nilijua fahari huwa ni jinsi moja (same sex) kumbe wanaweza kuwa tofauti!?
 
hahahaha hata mie naona hivyo aissee jamani!!!
Alijuaje kuwa kaeka rohoni suala lile?? Je alimtamkia??
Yeye ndo imemuuma bhana asiwe anafikiria lililo ndani ya moyo wa mwenzie!!

Umeona maisha hayaendi bila unafiki...watu hawataki hata kuwa wakweli kwa hisia zao na nafsi zao....kila mtu anataka onekana ye ndo alimpotezea mwenzie...ye ndo imemuuma hapo
 
haahahahhaha Kasinde mi wanifurahishaga tu post zako..... yan ukiamua umeamua... IVO.... hahhahahhahaha

yule mlopendana akakupeleka dunia nyingne kaishia wap tena jaman, hahahhahaa
 
Last edited by a moderator:
Wanaume wanapenda sanaaaaaa kubembelezwa! Acha kabisa! Mda mwingine hakutafuti tuuuuu ili akupime utafanyaje! Au anakupumzisha tu bench hamna mawasiliano ili tu urudi crawling to his feet! Nyoooooooo! Hapo ndo ule usemi USIACHE MBACHA KWA MSALA UPITAO una kazi muhimu. Akianza drama mimi na Ze Zomby aaaah tunasahaulishana machungu. Ila kama huna walau mazombi ma 2 au 3 lazima ukamlmbe makalio! Usiku haukuchi unless huo usiku uko kwnye viti virefu na Zomby!
scary-smiley-screaming-emoticon.gif
Moyoni unamwambia yule looser
kissmyass.gif
 
Back
Top Bottom