Fahamu umuhimu wa kuhonga katika mahusiano ya mapenzi

Fahamu umuhimu wa kuhonga katika mahusiano ya mapenzi

Vyuma vimekaza naona watu wanajaribu kujenga hoja ili kuona kama watalegezewa a.k.a kuhongwa.
All in all kuhonga hakukubaliki katika serikari ya ndonga langu
 
Habari wanajamiforum?

Leo nimeamua kuleta somo linalohusu umuhimu wa kuhonga ktk mapenzi.
Watu wengi hawaelewi umuhimu wa kuhonga kwenye mapenzi na kuanza kufikiria mambo mabaya naomba niwasilishe kama ifuatavyo:

1. KUHONGA HUBORESHA MAPENZI:

Fahamu kuwa unapomhonga mpenzi wako unamfanya ajihisi kama ni wapekee kwako, atajiona kama ni mmoja wapo kati ya watu wenye thamani kwako na huamini kama kweli upo karibu yake na unamjali.

Hali hii humfanya yeye kushindwa kutolipa mazuri kwako.
Wengi kabla ya kuomba papuchi hutanguliza hongo kwanza, si lazima iwe pesa hata hongo ya sifa za uongo na ukweli.

Kwa kuhonga kwako inamlazimu na yeye kulipa fadhila kwa kuonesha upendo wa dhati na utamfanya azidishe mapenzi kwako.


2. KUHONGA KUNAJENGA SANA KUMBUKUMBU KATIKA MAPENZI:

Fahamu kuwa unapomhonga mpenzi wako inakusaidia wewe kujijenga katika mawazo yake na endapo kama itatokea mkaachana nae basi pindi mpenzi wako atakapokuwa anaziona zawadi zako zitamfanya akukumbuke kwa mengi na atahisi kama kuachana na wewe kwake kuna tofauti na atajihisi kupoteza vingi toka kwako na kamwe kumbukumbu yako kwake haitofutika kila anapoona vitu ulivyomhonga.


Jitahidi sana unapohonga usihonge pesa tu, honga vitu vya kudumu maana huwa asset yako ya baadaye, pindi unapotokea mkwaruzano baina yenu.

Pesa huwa ni hongo inayovutia kwa muda mfupi na husaidia kupata kile unachokitaka kwa muda mfupi, ila jua atazitumia zitaisha utakuwa hujajenga misingi imara ya mapenzi.

Simaanishi kuwa usimpe mpenzi wako hela, hapana ila inabidi ufahamu kuwa pesa hutumika katika kukidhi mahitaji na sio katika kuboresha mapenzi.

Nyongeza:

Aisee jifunzeni kuhonga mpunguze stress za mapenzi.

Demiss (Cha mdeko )
Huwezi kuanza kutoa umuhimu wa kuhonga bila kueleza maana ya kuhonga.

Maana wengine tumeoa, tunapowapa wake zetu hela tunakuwa tunahonga?

Au kuhonga ni kwa wazinifu pekee?
 
Ni kweli...

Tatizo binadamu ni wabishi sana...

Alafu anayehongwa awe mwanamke anayejua kujiongeza...

Watu wanaweza hisi jamaa amelogwa na mwanamke, kumbe hapana anayepokea nae anajua kurudisha...


Cc: mahondaw
hapo hujahonga umekopesha
 
kuhonga ni kutokujiamini kama utaweza kupendwa.

Tuje kwanza kwenye maana ya kuhonga.

Kuhonga ni kutoa chochote kwa lengo la kupatiwa huduma nje na utaratibu. kwa muktadha wa mapenzi ni kumpa me/ke chochote iwe pesa au kitu cha thamni kupewa penzi.

Sioni kama kuna haja ya mwanamke/mwanamme kuhongwa ila anapaswa asukumwe na mapenzi yake kumpenda mtu....
[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Hahahhahahahahaha ntawaongozea na omo povu likoleee vizur ,Ila lazima tuwaambie ukweli.
Ndioo wanahonga lakini akija huku anaanzisha uzi wa kulalamika wanawake tunapenda pesaa

Haya leo nimewapa somooo
 
4.KUHESHIMIKA
Apa utaheshimika kuliko ata wazazi,mana we ndo unampa kiburi na jeuri ya kucheua na kubeua.huezi mkuta mdada au mkaka anamdharau anayemuhonga au kumtatulia mahitaji yake ya muhimu.......ukiomba mechi anytime unapewa na unapewa ushirikiano wa kiwango cha lami.tofauti na ukiwa na mkono mfupi mara unyimwe,mara ususiwe yaaan tafrani,majibu ya rejareja yenye kukunvujia heshima na utu wako hayakwepeki.
Hapa katika utoaji ataheshimiwa mtu ambaye ata hayuko siriaz,mpitaji tu na mhusika kuliko mwenye malengo ya dhati

Mjini heshima pesa,shikamoo makelele
Kunywa windock ya barid nakuja kulipa
 
kuhonga ni kutokujiamini kama utaweza kupendwa.

Tuje kwanza kwenye maana ya kuhonga.

Kuhonga ni kutoa chochote kwa lengo la kupatiwa huduma nje na utaratibu. kwa muktadha wa mapenzi ni kumpa me/ke chochote iwe pesa au kitu cha thamni kupewa penzi.

Sioni kama kuna haja ya mwanamke/mwanamme kuhongwa ila anapaswa asukumwe na mapenzi yake kumpenda mtu....
Sio kwa dunia ya saivii ndugu
 
Ni kweli...

Tatizo binadamu ni wabishi sana...

Alafu anayehongwa awe mwanamke anayejua kujiongeza...

Watu wanaweza hisi jamaa amelogwa na mwanamke, kumbe hapana anayepokea nae anajua kurudisha...


Cc: mahondaw
Watu wanaojitambua kama wewe ni wachache sana mkuu sema binadamu wabishi sana

Wanafikiria kuhonga kama ni kununua mwanamke au mwanaume .

Kuna jinsi ya kuhongaa ambayo haina athar za fikra mbaya
 
Back
Top Bottom