Fahamu matajiri watano (5) wenye hela ndefu duniani

Travis Walker

JF-Expert Member
Apr 10, 2017
323
332
1. Bwana Elon Musk, Elon ni tajiri wa kwanza dunia nzima. Huyu jamaa ana utajiri wa dola billioni 203 za kimarekani. Mafanikio ya Elon yalianza kuonekana alipoanzisha mfumo wa kufanya malipo online kupitia bank, Visa au Mastercard. Mfumo huo unatambulika kama Paypal ikiwa na maana “Mlipe Rafiki”.

Baada ya hapo aliuza mradi huo wa Paypal kwa fedha nyingi sana, na kuanzisha kampuni inayojulikana kama Space X. Kampuni inajihulisha na utengenezaji wa Rocket. Mnamo mwaka 2016 alianzisha tena kampuni mbili moja inayojulikana kama Boring na nyingine inajulika kwa nina la Neuralink. Kampuni ya boring inajihulisha na miundo mbinu ya ujezi wa barabara cha chini. Kampuni ya Neuralink inajihulisha na utengeneza wa chip ambazo zitawasiliana na ubongo wa binaadamu kwa lengo la kutibu maradhi ya akili yaani mental disorder.

Kwa mafanikio hayo bwana Elon Musk amekuwa tajiri wa kwanza wa dunia kwa mujibu wa jarida la investopedia mwaka 2021.

2. Bwana Jeff Benzos ni tajiri wa pili duniani kote. Mafanikio yake yalianza kuonekana alipoanzisha mfumo wa kuuza vitabu kupitia Internet, na baadae kuukuza mfumo na kuweza kuuza kila kitu. Mfumo huo unafahamika kama Amazon. Ni kampuni maarufu kwa sasa inayoongoza katika solo la uuzaji wa reja reja online. Baada ya hapo pia aliunda kampuni nyengine inayoitwa Blue origin inayoshughulika na utengenezaji wa vifaa mbali mbali kwa ajili ya usafiri wa anga za sayari. Jeff ana utajiri wa dola billioni 183 mpaka kufikia mwaka 2021. Mafanikio hayo yamefanya Jeff kuibuka tajiri wa pili duniani kote.

3. Inafahamika ya kwamba Bw. Bill Gates aliweza kukamata nafasi ya kwanza ya utajiri kwa muda wa maiaka 20. Lakini kwa miaka ya sasa imekuwa tofauti sana. Mpaka kufikia mwaka 2021 bwana Bill Gate ameibuka kuwa tajiri wa tatu duniani kote. Mafanikio yake yalianza kuonekana alipounda kampuni maarufu inayojulikana kwa umaarufu, ambayo ni Microsoft. Kampuni hii inaji gulisha rasmi kwa ajili ya kutengeneza Opreting system za compyuta. Pia Microsoft imetengeneza simu janja zinazojukana kama Nokia lumia. Lakini pia microsoft imetengeneza game console ambazo zinazofahamika kama Xbox. Bill gate ana utajiri wa dola billioni 133 za kimarekani.

4. Bernard Arnault
ni tajiri wa nne duniani. Yeye anajulikana kwa kutengeneza kampuni ya LVMH. Kampuni hii inajihulisha na utengenezaji wa vitu vya anasa kwa ajili ya matajiri. Imejizoleya umaaurufu mkubwa na bwana Bernard Arnault kuibuka tajiri wa nne.
Bernard Arnault kufikia mwaka 2012 ana utajiri wa dola billioni 113 za kimarekani.

5. Bwana Mark zuckerberg
ni tajiri wa tano duni. Mafanikio yake yalianza kuonekana alipoanzisha mtandao wa kijamii mnamo mwaka 2002. Mtandao huu maarufu inayojulikana kwa nina la Facebook. Baadae bwana Mark aliamua kufungua kampuni kabisa kwa nina la Facebook. Hivyo akatanua wingo na kumiliki mifumo mengine kama vile WhatsApp na Instagram. Bwana mark mpaka kufikia mwaka 2021 ana utajiri wa dola billioni 95 za kimarekani na kumfanya kuibuka na utajiri wa tano duniani.

Wenzetu wameumiza birches kuibadilisha dunia na kuweza kuwa Matajiri. Huu ni mwaka 2021, je wewe una mpango agni wa kuleta mabadiliko Tanzania na kujivunia hela ndefu. Toa mchango wako.

Imeandikwa na imekusanya na @Travis Walker
 
Mark nimemtumia details kuonyesha Facebook na Instagram sio salama sana. Wamenijibu kirahisim sijui kwakuwa mimi ni Mwafrika.

Niliambatanisha accounts zaidi ya 5 nilizodukua nimeishia kuambiwa asante bila kupewa zawadi /mkwanja.

Hawa nitawaharibia.

 
Eti pale kwenye uwanja wa maoni kuhusu maboresho wamesema ni marufuku kudukua account ya Mark mmiliki wa Facebook
Kama unaweza idukue, jimilikishe
Mbona Mark alishatoa dau siku nyingi kuwa mtu yeyote duniani atakayeweza kudukua account yake basi atamlipa zawadi kubwa sana.
Na alishasema account yake haiwezi dukuliwa na hacker yeyote duniani hata iweje.

Jaribuni,mnaweza amka mabilionea.
 
Mtaji. Vile vitu haviendeshwi kwa siri. Unaweza kukuta unapigwa fine trillions 4 za Kitanzania.
Ili Facebook wapate pesa kuna muunganiko wa taasisi zaidi ya tatu. Benki, mitandao ya simu, serikali n.k
Sasa wewe wakikupiga fine ya trillions 4, unaweza walipa ? Mtakaa muongee yaishe
 
Mark nimemtumia details kuonyesha Facebook na Instagram sio salama sana. Wamenijibu kiurahisi tu sijui kwakuwa mimi ni Mwafrika.

Niliambatanisha accounts zaidi ya 5 nilizodukua nimeishia kuambiwa asante bila kupewa zawadi /mkwanja.

Hawa nitawaharibia.
Da! Hii dunia inawatu
 
Mkuu nikusahihishe kidogo jeff amerudi nafasi yake ya kwanza ellon musk amepoteza almost 14m usd juzi tu ila hakika elon hazuiliki kuishika namba moja na fb ilianza 2006 sio 2002 nilipokosea nisahihishwe na ndo lengo la jamii forums.
Amerudi tena no1 muda tu.
 
Mbona Mark alishatoa dau siku nyingi kuwa mtu yeyote duniani atakayeweza kudukua account yake basi atamlipa zawadi kubwa sana.
Na alishasema account yake haiwezi dukuliwa na hacker yeyote duniani hata iweje.

Jaribuni,mnaweza amka mabilionea.
Aah! Acha tupambane na hali zetu.. na sie tuwe kama Elon.
 
Back
Top Bottom