Fahamu kwanini Wasomi wengi hukosa ajira

Samedi Amba

JF-Expert Member
Nov 13, 2018
227
178
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana wengi wa kitanzani na hili limeshuhudiwa zaidi katika majaribio mbalimbali ya nafasi za kazi ambapo vijana wengi hujitokeza kuomba ajira.

Ikumbukwe adha hii ya ajira sio tu kwa vijana wadogo bali kwa watu wenye umri zaidi ya vijana ambao wengi wao ni walioacha kazi zao za awali au kuzipoteza kutokana na mambo mbalimbali yatokeayo kwenye mazingira ya kazi zilizopita.

Tanzania ni moja kati ya nchi yenye tatizo la upungufu mkubwa wa ajira na ndio maana Raisi wa awamu ya tano Mh Dr John Pombe Magufuli akaamua kuja na kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda ili kutengeneza nafasi nyingi za ajira haswaa kwa vijana wa kitanzania.

Lakini bado tatizo hili limezidi kuwa kubwa sana kwa kuwa wahitimu wanaomaliza vyuo kuongezeka kila mwaka na kukutana na wengine ambao sio wahitimu wa vyuo vikuu na wahitimu waliomaliza masomo yao miaka iliyopita bado wako mtaani,kwa mfano wahitimu wa shahada ya ualimu wako mtaani tangu mwaka 2014 mpaka leo hawajaajiriwa na bado serikali haina mpango huo hasa kwa masomo ya sanaa ambao idadi yao ni kubwa sana.
?

Sababu 8 zinazopelekea wahitimu wengi hukosa ajira?

1⃣UFINYU WA NAFASI ZA AJIRA SERIKALINI.
Hakika hapa kila msomi atakuwa anaelewa nataka kuzungumzia nini,lakini ni wazi na dhahiri kuwa serkali bado inatoa nafasi chache sana za ajira kulinganisha na wanaomaliza katika taaluma mbalimbamli ambao wanahitajika na serikali,siamini kama walimu wa sanaa katika shule zetu nchini wameajaa na wametosha kwani hata maeneo ya mjini kwa sasa kuna shule ambazo mwalimu mmoja anahudumia idadi kubwa sana ya wanafunzi kwa darasa moja,kwani kitaalamu mwalimu mmoja ni vizuri akahudumia wanafunzi wasiozidi 50 kwa darasa moja ila bado haipo hivyo,kwa hiyo ni vizuri kama serikali zetu zingeangalia upya utaratibu wa utoaji upya wa ajira.

2⃣UBOVU WA MITAALA YA ELIMU ITOLEWAYO.
Hakika acha niliseme hili na kila mtu asome na asikie,mitaala yetu ya elimu bado ni changamoto katika soko la ajira kwani haimpi mwanafunzi mbinu za kujikwamua kiuchumi bali zinamuandaa mwanafunzi kuja kuwa mtumishi mwadilifu kwa bosi wake,mitaala bado haijabadilika kulingana na wakati uliopo sasa wa DUNIA YA SAYANSI YA MAWASILIANO,ambapo kutengeneza pesa hakuhitaji mtu kuwa na shamba kubwa sana au kumiliki mifugo mingi sana kama kigezo cha utajiri kwani biashara za mitandao zimekuwa chachu kubwa sana ya mabadiliko ya uchumi,hivyo mitaala yetu ni bora ingeangaliwa upya kulingana na nyakati mpya za sasa.

3⃣MFUMO WA KUFAHAMIANA BADO UNASUMBUA WENGI.
Hii nayo ni changamoto katika soko la ajira kwani watu wengi husumbuka sana kupata ajira kama ni mtoto wa mvuja jasho kutoka Kata ya kaloleni,Njoro au Kahe na huna yoyote anaemfahamu kumshika mkono hakika atasota,kwani ni mara kadhaa nimeshuhudia waajiri wakisema ni ngumu kumuajiri usiemjua na kumuacha unaemjua,kuna wakati nilifanya jaribio mahala fulani lakini sikupata nafasi kwa kuwa aliyekuwa anaajiri alisema alikua anafata protokali za kufanya jaribio hilo hivyo atakaowaajiri anawajua,niliumia sana kwa kuwa nilikuwa nimewazidi kila kitu ila mbaya ni kwamba nilikuwa sina ninaemfahamu kunisaidia kuipata ajira ile.

4⃣MAWAZO FINYU YA WASOMI WENGI.
Katika kipindi amabacho wasomi wengi kuonekana kuwa hawana jipya ni hichi,kwani kuna wakati huwezi kutofautisha wazo la msomi na asie msomi,kuna wakati ukaona ni bora kukaa na asie msomi atakusaidia mawazo ya maisha kuko kukaa na wasomi wanaowaza mambo yasiyojenga,mfano unakuta msomi wa chuo anawazahuwezi kufanikiwa bila kujiunga freemason, mpaka unashangaa hii ni nini lakini hakuna cha ajabu kwa kuwa mawzo yetu wasomi kuna wakati bado ni mgando sana,lazima tufahamu huwezi kufanikiwa bila kutaabika na kuhangaika pasipo kukata tamaa,kwani kufanikiwa sio tambarare kama unavyodhania.

5⃣MAWAZO FINYU YA WAAJIRI.
Hili pia limekuwa tatizo kubwa kwa waajiri wengi,Lazima ieleweke kwamba Tanzania sio nchi inayotumia lugha ya kingereza hivyo ni swala la kawaida kumuona msomi akimaliza shahada na klugha ya kingereza kwake ikawa sio nzuri sana,hasa kwa wale waliotoka shule za kata kama mimi na wewe na nyinginezo ambazo mpaka mwalimu aongee kiswahili ndo aeleweke bila hivyo darasa zima watafeli na mwalimu atafukuzwa,kuna wakati una ujuzi mkubwa sana la ari ya kujituma ila lugha sio nzuri sana na utakosa ajira kwa kuwa muajiri amemsikia mwingine akiongea kingereza kizuri zaidi yako na kuvutiwa na lugha na wala sio utendaji.

Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Dar es salaam Profesa Rwekaza Mukandala alisema kwamba"BAADHI YA WAAJIRI WANACHANGANYA KATI YA UJUZI NA LAFUDHI"hivyo kubabaika na wanaotoka nje ya nchi wakidhani ni bora kwa kuwa huongea lugha ya kingereza kwa lafudhi safi na kwa ufasaha sana, hivyo wahitimu wa ndani kunyimwa ajira kwa sababu zisizo na mashiko yoyote.

6⃣KUCHAGUA KAZI KWA WASOMI WENGI.
Ni dahahiri wasomi wengi huwa na mawazo makubwa wawapo masomoni lakini mambo huwa tofauti wamalizapo masomo yao kwani mtaani mambo ni tofauti sana na waliyokuwa wanayawaza wakiwa vyuoni,wasomi wengi huwaza kuwa mameneja au wakurugenzi na kadhalika lakini mambo huwa sio hivyo kwani ni wachache sana ambao mambo huenda kama walivyopanga,hivyo wakikuta mambo sio hawataki kufanya kazi nyingine yoyote wakisubiri kuwa mameneja na nyadhifa nyingine nzuri walizoziota awali.

8⃣KUBWETEKA
Kuna wasomi mpaka leo wanasubiria kazi zitolewe na serikali na waajiriwe,lakini bado hakuna uhakika wa kazi hizo,hivyo kuendelea kuongeza idadi ya rundo la wasomi wasio na ajira mtaani,vijana lazima wajiongeze kufanya mambo mbalimbali hata kama hukusmea hicho usibweteke kijaribu huenda ndio kitakachokupa ajira ya kudumu na kukuondoa kwenye baa la ukosefu wa ajira.Kwa mfano wapo wengi ambao ni wafanyakazi wa kampuni mbalimbali hawakusomea lakini wanafanya tena kwa mafanikio makubwa,cha msingi ni kujituma na kuwa na ari ya kujifunza kwani Dunia imebadilika sio lazima uwe mwalimu kwa kuwa umesomea ualimu unaweza ukawa hata Mshauri wa maswala ya ukimwi au mjasiriamali na ukafanikiwa.

Mwisho nipende kuwashukuru wote mtaopitia makala yangu hii,ni vyema tukaenda nawakati na tukumbuke hii ni dunia nyingine sio ilee ya miaka ile lakini bado tuna nafasi ya kujifunza na kuchukua maamuzi mapya ya kujenga maisha yet na tuache kulalamika na kuilamu serikali kila siku tushachelewa haitatusaidia chochote bali tujipambanue kwa mapana zaidi.Nakumbuka kuna wakati nilikuwa boda boda na sikukata tamaa nilipambna japo nilipata changamoto kubwa ila unajifunza kupitia pale ili siku ukifanikiwa uheshimu mafanikio yako na wengine wanufaika

Na Peter Mapigano,

Original source: Epvate international consultancy
 
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana wengi wa kitanzani na hili limeshuhudiwa zaidi katika majaribio mbalimbali ya nafasi za kazi ambapo vijana wengi hujitokeza kuomba ajira,.Ikumbukwe adha hii ya ajira sio tu kwa vijana wadogo bali kwa watu wenye umri zaidi ya vijana ambao wengi wao ni walioacha kazi zao za awali au kuzipoteza kutokana na mambo mbalimbali yatokeayo kwenye mazingira ya kazi zilizopita.

Tanzania ni moja kati ya nchi yenye tatizo la upungufu mkubwa wa ajira na ndio maana Raisi wa awamu ya tano Mh Dr John Pombe Magufuli akaamua kuja na kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda ili kutengeneza nafasi nyingi za ajira haswaa kwa vijana wa kitanzania.
Lakini bado tatizo hili limezidi kuwa kubwa sana kwa kuwa wahitimu wanaomaliza vyuo kuongezeka kila mwaka na kukutana na wengine ambao sio wahitimu wa vyuo vikuu na wahitimu waliomaliza masomo yao miaka iliyopita bado wako mtaani,kwa mfano wahitimu wa shahada ya ualimu wako mtaani tangu mwaka 2014 mpaka leo hawajaajiriwa na bado serikali haina mpango huo hasa kwa masomo ya sanaa ambao idadi yao ni kubwa sana.
?

*Sababu 8 zinazopelekea wahitimu wengi hukosa ajira* ?

1⃣UFINYU WA NAFASI ZA AJIRA SERIKALINI.
Hakika hapa kila msomi atakuwa anaelewa nataka kuzungumzia nini,lakini ni wazi na dhahiri kuwa serkali bado inatoa nafasi chache sana za ajira kulinganisha na wanaomaliza katika taaluma mbalimbamli ambao wanahitajika na serikali,siamini kama walimu wa sanaa katika shule zetu nchini wameajaa na wametosha kwani hata maeneo ya mjini kwa sasa kuna shule ambazo mwalimu mmoja anahudumia idadi kubwa sana ya wanafunzi kwa darasa moja,kwani kitaalamu mwalimu mmoja ni vizuri akahudumia wanafunzi wasiozidi 50 kwa darasa moja ila bado haipo hivyo,kwa hiyo ni vizuri kama serikali zetu zingeangalia upya utaratibu wa utoaji upya wa ajira.

2⃣UBOVU WA MITAALA YA ELIMU ITOLEWAYO.
Hakika acha niliseme hili na kila mtu asome na asikie,mitaala yetu ya elimu bado ni changamoto katika soko la ajira kwani haimpi mwanafunzi mbinu za kujikwamua kiuchumi bali zinamuandaa mwanafunzi kuja kuwa mtumishi mwadilifu kwa bosi wake,mitaala bado haijabadilika kulingana na wakati uliopo sasa wa DUNIA YA SAYANSI YA MAWASILIANO,ambapo kutengeneza pesa hakuhitaji mtu kuwa na shamba kubwa sana au kumiliki mifugo mingi sana kama kigezo cha utajiri kwani biashara za mitandao zimekuwa chachu kubwa sana ya mabadiliko ya uchumi,hivyo mitaala yetu ni bora ingeangaliwa upya kulingana na nyakati mpya za sasa.

3⃣MFUMO WA KUFAHAMIANA BADO UNASUMBUA WENGI.
Hii nayo ni changamoto katika soko la ajira kwani watu wengi husumbuka sana kupata ajira kama ni mtoto wa mvuja jasho kutoka Kata ya kaloleni,Njoro au Kahe na huna yoyote anaemfahamu kumshika mkono hakika atasota,kwani ni mara kadhaa nimeshuhudia waajiri wakisema ni ngumu kumuajiri usiemjua na kumuacha unaemjua,kuna wakati nilifanya jaribio mahala fulani lakini sikupata nafasi kwa kuwa aliyekuwa anaajiri alisema alikua anafata protokali za kufanya jaribio hilo hivyo atakaowaajiri anawajua,niliumia sana kwa kuwa nilikuwa nimewazidi kila kitu ila mbaya ni kwamba nilikuwa sina ninaemfahamu kunisaidia kuipata ajira ile.

4⃣MAWAZO FINYU YA WASOMI WENGI.
Katika kipindi amabacho wasomi wengi kuonekana kuwa hawana jipya ni hichi,kwani kuna wakati huwezi kutofautisha wazo la msomi na asie msomi,kuna wakati ukaona ni bora kukaa na asie msomi atakusaidia mawazo ya maisha kuko kukaa na wasomi wanaowaza mambo yasiyojenga,mfano unakuta msomi wa chuo anawazahuwezi kufanikiwa bila kujiunga freemason, mpaka unashangaa hii ni nini lakini hakuna cha ajabu kwa kuwa mawzo yetu wasomi kuna wakati bado ni mgando sana,lazima tufahamu huwezi kufanikiwa bila kutaabika na kuhangaika pasipo kukata tamaa,kwani kufanikiwa sio tambarare kama unavyodhania.

5⃣MAWAZO FINYU YA WAAJIRI.
Hili pia limekuwa tatizo kubwa kwa waajiri wengi,Lazima ieleweke kwamba Tanzania sio nchi inayotumia lugha ya kingereza hivyo ni swala la kawaida kumuona msomi akimaliza shahada na klugha ya kingereza kwake ikawa sio nzuri sana,hasa kwa wale waliotoka shule za kata kama mimi na wewe na nyinginezo ambazo mpaka mwalimu aongee kiswahili ndo aeleweke bila hivyo darasa zima watafeli na mwalimu atafukuzwa,kuna wakati una ujuzi mkubwa sana la ari ya kujituma ila lugha sio nzuri sana na utakosa ajira kwa kuwa muajiri amemsikia mwingine akiongea kingereza kizuri zaidi yako na kuvutiwa na lugha na wala sio utendaji.
Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Dar es salaam Profesa Rwekaza Mukandala alisema kwamba"BAADHI YA WAAJIRI WANACHANGANYA KATI YA UJUZI NA LAFUDHI"hivyo kubabaika na wanaotoka nje ya nchi wakidhani ni bora kwa kuwa huongea lugha ya kingereza kwa lafudhi safi na kwa ufasaha sana, hivyo wahitimu wa ndani kunyimwa ajira kwa sababu zisizo na mashiko yoyote.

6⃣KUCHAGUA KAZI KWA WASOMI WENGI.
Ni dahahiri wasomi wengi huwa na mawazo makubwa wawapo masomoni lakini mambo huwa tofauti wamalizapo masomo yao kwani mtaani mambo ni tofauti sana na waliyokuwa wanayawaza wakiwa vyuoni,wasomi wengi huwaza kuwa mameneja au wakurugenzi na kadhalika lakini mambo huwa sio hivyo kwani ni wachache sana ambao mambo huenda kama walivyopanga,hivyo wakikuta mambo sio hawataki kufanya kazi nyingine yoyote wakisubiri kuwa mameneja na nyadhifa nyingine nzuri walizoziota awali.

8⃣KUBWETEKA
Kuna wasomi mpaka leo wanasubiria kazi zitolewe na serikali na waajiriwe,lakini bado hakuna uhakika wa kazi hizo,hivyo kuendelea kuongeza idadi ya rundo la wasomi wasio na ajira mtaani,vijana lazima wajiongeze kufanya mambo mbalimbali hata kama hukusmea hicho usibweteke kijaribu huenda ndio kitakachokupa ajira ya kudumu na kukuondoa kwenye baa la ukosefu wa ajira.Kwa mfano wapo wengi ambao ni wafanyakazi wa kampuni mbalimbali hawakusomea lakini wanafanya tena kwa mafanikio makubwa,cha msingi ni kujituma na kuwa na ari ya kujifunza kwani Dunia imebadilika sio lazima uwe mwalimu kwa kuwa umesomea ualimu unaweza ukawa hata Mshauri wa maswala ya ukimwi au mjasiriamali na ukafanikiwa.

Mwisho nipende kuwashukuru wote mtaopitia makala yangu hii,ni vyema tukaenda nawakati na tukumbuke hii ni dunia nyingine sio ilee ya miaka ile lakini bado tuna nafasi ya kujifunza na kuchukua maamuzi mapya ya kujenga maisha yet na tuache kulalamika na kuilamu serikali kila siku tushachelewa haitatusaidia chochote bali tujipambanue kwa mapana zaidi.Nakumbuka kuna wakati nilikuwa boda boda na sikukata tamaa nilipambna japo nilipata changamoto kubwa ila unajifunza kupitia pale ili siku ukifanikiwa uheshimu mafanikio yako na wengine wanufaika

Na Peter Mapigano,

Original source: Epvate international consultancy

Mbona hizi zote zinajulikana na wengi kabla hata hujatuandikia hapa?
 
*Kuchagua kazi kwa wasomi*
1. Hivi mnapoandika hili hua mnafikiria kisomi au ndio mawazo yale yale ya kufanikiwa mpaka uwe Freemason? Let say, mtu amegraduate BSc in Chemistry. Kazi imetangazwa inamtaka graduate wa BSc in Animal Science. Unataka huyo mwalimu wa Chemistry nae atume maombi ya kazi hio? Automatically, mwalimu hato apply kwasababu qualification yake ni tofauti. So, hapo tuseme amebagua kazi au lah
2. Mtu ni graduate wa BSc in Biology, kuna nafasi ya kaz position ya Emergency Response Manager unataka afanye application ili hali hajui hata responsibilities za hio kazi labda akariri kutoka kwenye job description. Hapa napo amebagua kazi?
3. Mtu ana degree ya Pharmacy, nafasi ya kazi inataka Pharmacist mwenye qualification ya diploma, huyu graduate aombe kazi hio pa1 ni kwamba ana career hio. Je, asipoomba amebagua kazi?
4. MNH wanataka Doctor of Dental Surgery, unataka graduate wa Law aombe kazi hio. Hawezi omba, amebagua kazi?
Au hua mnaongelea ubaguzi upi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Graduate siku hizi hawachagui kazi...Tatizo la ajira Tanzania linachangiwa na vitu vingi sana. Unaweza kuwalaumu wasomi bure kumbe Tatizo ni mfumo wetu wa kutengeneza ajira. Tanzania hatuweki mazingira ya kutengeneza ajira mpya.
Kozi nyingi haziendani na hali ya soko la ajira...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba niwakilishe mchango wa mawazo husika kama fuatavyo, kwa sasa wahitimu wengi inatakiwa tujikite sana kwenye TRAINING mbalimbali kutoka consultancy companies za field tofauti tofauti hii itawezesha uwe na sifa za ziada za kutofautisha na wahitimu wengi ntachambua kwa upande wa business Administration

Natolea mfano wew ni muhitimu wa business Administration nafasi imetangazwa ni cutomer service representative hapa ungekuwa umepata Training kutoka Soft trainers university kuhusu Customer relation management system and KYC know your customer Training nazani hapa unakuwa nasifa mbili za ziada kumshinda Muhitimu mwingine wa kawaida.

Umemaliza Human resource Management mfano hii course ukitembelea consultancy companies kuhusu mambo ya HR utapata kujifunza mambo kama ya Employment relation and Labour act, Code of good practice pia utajifunza Human resource Management systems hii ina maana utakuwa upo vizuri kushindana na wahitimu wengine wa hii course

Mfano umemaliza Accountancy tembelea consultancy companies zinahusu mambo ya finance hapa utaweza kujifunza mambo ngi kwa vitendo Ikiwemo Accounting packages kama Pitchtil, Quick books na Tally pia utaelekezwa na international standard procedure za Accounting kwa matendo hii itakuafanya uwe mtu wa kujiamini na kuweza kuwashinda wahitimu wengine

Hizo consultancy companies ili ujifunze hayo nilihainisha hapo juu na wakupe mpaka certification kuna gharama kidogo ila ni za kawaida ambapo kwa mtu mwenye nia uwezi kukosa yani hiyo itakufanya hata kwa mwaka unabdilisha kazi hata 5 kwakuwa waajiri wengi hawapendi sana kuanza na mtu from scratch wanapenda mtu amabaye ata add value course nyingi hasa za biashara zina hitaji kupata training nyingi za kujua kazi zinaendaje ambayo hayo yote utayapata ukitembelea izo consultancy companies hivyo utajikuta huwez kuchelewa kupata kazi tena itafika mda utawezakuchagua hii natka ile sitaki
 
mi nazani mtoa uzi umejitahidi kugusa points halisia lkn tusidanganyane hapa sababu kubwa ni moja tu '' MFUMO WA ELIMU'' huu mfumo wa sasa haujibu mahitaji yetu kwa kiasi kikubwa nafikiri tukirekebisha mfumo wetu wa elimu either kuanzia chini au hata hapa kati kati bac ajira nyingi zitatengenezwa
 
*Kuchagua kazi kwa wasomi*
1. Hivi mnapoandika hili hua mnafikiria kisomi au ndio mawazo yale yale ya kufanikiwa mpaka uwe Freemason? Let say, mtu amegraduate BSc in Chemistry. Kazi imetangazwa inamtaka graduate wa BSc in Animal Science. Unataka huyo mwalimu wa Chemistry nae atume maombi ya kazi hio? Automatically, mwalimu hato apply kwasababu qualification yake ni tofauti. So, hapo tuseme amebagua kazi au lah
2. Mtu ni graduate wa BSc in Biology, kuna nafasi ya kaz position ya Emergency Response Manager unataka afanye application ili hali hajui hata responsibilities za hio kazi labda akariri kutoka kwenye job description. Hapa napo amebagua kazi?
3. Mtu ana degree ya Pharmacy, nafasi ya kazi inataka Pharmacist mwenye qualification ya diploma, huyu graduate aombe kazi hio pa1 ni kwamba ana career hio. Je, asipoomba amebagua kazi?
4. MNH wanataka Doctor of Dental Surgery, unataka graduate wa Law aombe kazi hio. Hawezi omba, amebagua kazi?
Au hua mnaongelea ubaguzi upi?

Sent using Jamii Forums mobile app

Nafikiri Ana maana kwamba usijikweze

mfano kuna watu nilifanya nao interview kule kwenye SGR
wale waturuki wakasema nawaajiri kama technicians kwanza.
wenzangu kwakua wana degree lakin hawajui chochote practically
wakawa hawajakubaliana na hilo swala.
 
*Kuchagua kazi kwa wasomi*
1. Hivi mnapoandika hili hua mnafikiria kisomi au ndio mawazo yale yale ya kufanikiwa mpaka uwe Freemason? Let say, mtu amegraduate BSc in Chemistry. Kazi imetangazwa inamtaka graduate wa BSc in Animal Science. Unataka huyo mwalimu wa Chemistry nae atume maombi ya kazi hio? Automatically, mwalimu hato apply kwasababu qualification yake ni tofauti. So, hapo tuseme amebagua kazi au lah
2. Mtu ni graduate wa BSc in Biology, kuna nafasi ya kaz position ya Emergency Response Manager unataka afanye application ili hali hajui hata responsibilities za hio kazi labda akariri kutoka kwenye job description. Hapa napo amebagua kazi?
3. Mtu ana degree ya Pharmacy, nafasi ya kazi inataka Pharmacist mwenye qualification ya diploma, huyu graduate aombe kazi hio pa1 ni kwamba ana career hio. Je, asipoomba amebagua kazi?
4. MNH wanataka Doctor of Dental Surgery, unataka graduate wa Law aombe kazi hio. Hawezi omba, amebagua kazi?
Au hua mnaongelea ubaguzi upi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Time will tell

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makala imekaa kuwakosoa zaidi vijana kuliko mfumo uliowaletea hilo janga, yani mfano ugonjwa umezuka we unaanza kupambana na mgonjwa badala ya kupamabana na ugonjwa wenyewe.
 
Kuna baadhi ya point zako siziungi mkono Namba 4, 6, 8.
Tufike mahali tujitambue Haiwezekani mtu ni proffesional wa fani flani katumia muda mwingi kujifunza hio proffession halafu tukubaliane tu kwamba afanye kazi yoyote .
Shida kubwa ipo kwa Goverment

Hii inagusa sehemu nyingi sana kuanzia kwenye aina ya kozi watu wanazosoma, kwa sababu serikali ndiye anasimamia,

Inagusa kwenyeUendeshaji wa sekta binafsi Haiwezekani mfanyakazi wa Private analipwa kama anavyo amua Mwenye taasisi hapa namaanisha kuna kazi nyingi Ambazo watu wanashindwa kufanya kwa sababu ya maslai mabovu

Inagusa kwenye uwezeshwaji wa wana taaluma mbalimbali kwa sababu hawawezi kuajiriwa wote kwa hiyo inatakiwa wengine wajiongeze either kuanzisha taasisi mpya zenye ubunifu ziwe za serekali au za binafsi

NOTE: Ukifikiria tatizo la ajira fikiria Kitaifa sio kwa mtu mmoja mmoja ( mfano kuna mtu anaongelea maswala ya course za mda mfupi izo zitasaidia baadhi ya watu kupata, ila kundi kubwa litabaki halina ajira)
 
9. Kufuata shauri za Consaltant feki na Motivation speakers wanaonuka njaa.
 
Back
Top Bottom