Fahamu kwanini makada wa CCM wanaweweseka kuhusu Maalim Seif kuhamia ACT-Wazalendo badala ya CHADEMA

Uenda Makada wa Chadema wanateseka ziadi ya makada wa CCM..! Kazi kwenu kugombania Ruzuku na kugombania kambi rasmi ya upinzani Bungeni CCM wala hawana presha na ACT
Obviously hujui siasa za upinzani wala hujui usemalo usemalo. Katika siasa kuna kupanda na kushuka na kamwe hakuna rafiki wa kuduma wala adui wa kudumu, kuna maslahi ya kudumu tu.
 
zaidi ya mada yako kuwa na mpangilio mzuri wa aya , hakuna kingine kinachomfurahisha msomaji kusoma mpaka mwisho. Awali ya yote:
1. umeshindwa kusema ukweli kuwa waliopoteza kwenye huo mchezo ni CHADEMA na CUF na waliopata ni CCM na ACT. hapa kila chama(CCM na ACT) kimepata kadiri inavyoona ni fursa

2.CCM muda wote ulikuwa ukihofia nguvu aliyonayo seif visiwani lakini sasa hiyo nguvu imegawanywa mara mbilil, hivyo CCM hawana cha kupoteza kwa sababu bado nguvu yake ipo palepale.

3. CHADEMA kitakosa ushawishi mikoa ya kusini na zanzibar ambapo ilikuwa ngome kuu ya CUF na Maalimu, na hivyo kuna hati hati CHADEMA kitakua chama cha ukanda wa kaskazini tu na hivyo kupoteza ushawishi kwa kuonekana chama cha kikabila.

4. Maalimu seif ni mjanja sana kacheza na akili ya Mbowe kwa haraka sana. Zito alishtumiwa na CHADEMA kama msaliti na hivyo maalim seif kuhamia ACT ambaye ni mshirika wa UKAWA kutaifanya CHADEMA iikubali ACT ya zito na kusahau yote na hivyo mbowe kula matapishi yake.

5. Condition ambayo zitto atawapa wakitaka ajiunge na ukawa ni yeye kuwa mwenyekiti wa ukawa au mpeperusha bendera ya ukawa uchaguzi wa 2020. je chadema itakubali ? Lissu atakubali? mpasuko mpya unazaliwa tena mkubwa.

6. yote kwa yote , CCM hatuna cha kupoteza katika hili.

Hiyo Point ya pili mnajidanganya nafsi zenu au wewe ulioandika hujui chochote kuhusu watu wanaoumuunga mkono Maalim Seif. Usijidanganye ukasema wamegawanyika na wala usijipe moyo wewe na hao vijana wenzako mulio ingia kwenye siasa majuzi.
hao wote waliopewa vyeo na Lipumba na lipumba mwenyewe hawana watu zanzibar. Huyo katibu mkuu wa Lipumba alikataliwa na wafuasi wa jimbo lake pemba mwaka 2015. najua wewe huyajui hayo kwasababu huna unalolijua ya Kule zanzibar.
CCM imefeli Kwa Maalim na itaendelea kufeli kwake labda hiyo siku ambayo atakuwa Maalim hayupo tena Duniani.
Kama kawa CCm zanzibar 2020 watashindwa tena kwa Kura. CCm haijawahi kutakiwa na walio wengi Zanzibar tangu 1995
 
Kongole kwako mkuu, umeandika waraka maridhawa kabisa.
Maalim Seif ni Taasisi, alipokuwa ndani ya CUF, aliidefine CUF. na sasa amehama na roho ya CUF kwenda ACT. CUF - Lipumba ni mzoga wa CUF, hakuna kitu hapo. inawezekana Lipumba anafurahi kwamba kafaulu kumtoa Maalim. Alivyo mbumbumbu wa kisiasa, huenda anafurahi, kama zuzu.
Kwa vyovyote mabwana zake wa CCM waliomtuma, wamefurahi sana, lakini baada ya kuhamia ACT, wametaharuki.

Hawana hakika kama hiki walichofanya kimewasaidia au kinawaletea matatizo makubwa zaidi.

Kwa upinzani hii ni habari njema. Huu mchanyato mpya wa Zitto-Maalim +CHADEMA utakuwa mziki wa aina yake kwa 2020. Maalim Seif wa ACT atakuwa na mchango mkubwa zaidi bara kuliko Maalim Seif wa CUF. Kumbuka Zitto wa sasa ni yule aliyebatizwa, siyo yule wa enzi za Kikwete. na zile takataka zilizokuwa ACT, akina Kitila, Anna Mughwira na yule katibu mkuu nimesahau jina lake, CCM walitusaidia kuzisafisha. na Magufuli akambatiza Zitto. kwa hiyo sasa ni poa.

Mwaka huu mzuri sana kwa upinzani. juzijuzi tu kuna JIPU moja ambalo wapinzani walikuwa wanajiuliza wanalipasuaje, sasa limehama kama lilivyo likaingia CCM. sasa wao watajua namna ya kulipasua. wapinzani swwaaafiiii! Asante Mungu. Baada ya makasheshe yote, Tundu Lissu kupigwa risasi, kina Mbowe kusota rumande siyo mara moja wala mara mbili bali mara kadhaa, akina Lijualikali kunyanyaswa sana, kina Halima Mdee mara rumande mara kuhojiwa bungeni, hatimaye Mungu anatuelekeza Neema tele! Ashukuriwe Mungu.
Katibu uliemsahau ni Samson mwigamba. Na jipu lilobakia chadema ni sumae na kumpata katibu Mkuu, huyu wa sasa hafai, ni muoga wa polisi sana.
 
zaidi ya mada yako kuwa na mpangilio mzuri wa aya , hakuna kingine kinachomfurahisha msomaji kusoma mpaka mwisho. Awali ya yote:
1. umeshindwa kusema ukweli kuwa waliopoteza kwenye huo mchezo ni CHADEMA na CUF na waliopata ni CCM na ACT. hapa kila chama(CCM na ACT) kimepata kadiri inavyoona ni fursa

2.CCM muda wote ulikuwa ukihofia nguvu aliyonayo seif visiwani lakini sasa hiyo nguvu imegawanywa mara mbilil, hivyo CCM hawana cha kupoteza kwa sababu bado nguvu yake ipo palepale.

3. CHADEMA kitakosa ushawishi mikoa ya kusini na zanzibar ambapo ilikuwa ngome kuu ya CUF na Maalimu, na hivyo kuna hati hati CHADEMA kitakua chama cha ukanda wa kaskazini tu na hivyo kupoteza ushawishi kwa kuonekana chama cha kikabila.

4. Maalimu seif ni mjanja sana kacheza na akili ya Mbowe kwa haraka sana. Zito alishtumiwa na CHADEMA kama msaliti na hivyo maalim seif kuhamia ACT ambaye ni mshirika wa UKAWA kutaifanya CHADEMA iikubali ACT ya zito na kusahau yote na hivyo mbowe kula matapishi yake.

5. Condition ambayo zitto atawapa wakitaka ajiunge na ukawa ni yeye kuwa mwenyekiti wa ukawa au mpeperusha bendera ya ukawa uchaguzi wa 2020. je chadema itakubali ? Lissu atakubali? mpasuko mpya unazaliwa tena mkubwa.

6. yote kwa yote , CCM hatuna cha kupoteza katika hili.
Kijani kwa kujifariji hamjambo .
 
mkuu petero kwanza tuanzie hapa,
Si CCM tu wanaohaha ni hata CHADEMA

full stop
Kivipi CHADEMA wahahe wakati waliomba mgogoro uishe ili UKAWA ikusanye nguvu mpya. kumbuka zito hakuwepo kwenye UKAWA aliona madhara yake japo Magu aliwalipa kwa kuwapa ukuu wa mkoa Moshi, japo haibebeki. Sasa ACT ndani ya UKAWA. ANAYE HAHA hapa ni ccm japo wanajipanga kuongeza mamluk huko aliko SEIf
 
Ushauri kwa Vyama vya Upinzani
Hakuna Serikali yoyote nzur kama huna Wabunge wa kutosha.... Muunganiko wa Chadema na ACT kama new Ukawa kwa 2020 wakijikita kwenye Kutafuta idadi ya wabunge ambao watasababisha akidi isitime bila wao kuwemo litakua jambo la msing zaid kwao kuliko kutafuta Urais
 
Uenda Makada wa Chadema wanateseka ziadi ya makada wa CCM..! Kazi kwenu kugombania Ruzuku na kugombania kambi rasmi ya upinzani Bungeni CCM wala hawana presha na ACT
Mission ilikuwa kuufuta upinzani kwa kuanzia CUF badala yake wamemmaliza Sakaya na Lipumba.
Upinzani ndo kwanza umechochewa kwa petrol.
Mark my word.
 
Kongole kwako mkuu, umeandika waraka maridhawa kabisa.
Maalim Seif ni Taasisi, alipokuwa ndani ya CUF, aliidefine CUF. na sasa amehama na roho ya CUF kwenda ACT. CUF - Lipumba ni mzoga wa CUF, hakuna kitu hapo. inawezekana Lipumba anafurahi kwamba kafaulu kumtoa Maalim. Alivyo mbumbumbu wa kisiasa, huenda anafurahi, kama zuzu.
Kwa vyovyote mabwana zake wa CCM waliomtuma, wamefurahi sana, lakini baada ya kuhamia ACT, wametaharuki.

Hawana hakika kama hiki walichofanya kimewasaidia au kinawaletea matatizo makubwa zaidi.

Kwa upinzani hii ni habari njema. Huu mchanyato mpya wa Zitto-Maalim +CHADEMA utakuwa mziki wa aina yake kwa 2020. Maalim Seif wa ACT atakuwa na mchango mkubwa zaidi bara kuliko Maalim Seif wa CUF. Kumbuka Zitto wa sasa ni yule aliyebatizwa, siyo yule wa enzi za Kikwete. na zile takataka zilizokuwa ACT, akina Kitila, Anna Mughwira na yule katibu mkuu nimesahau jina lake, CCM walitusaidia kuzisafisha. na Magufuli akambatiza Zitto. kwa hiyo sasa ni poa.

Mwaka huu mzuri sana kwa upinzani. juzijuzi tu kuna JIPU moja ambalo wapinzani walikuwa wanajiuliza wanalipasuaje, sasa limehama kama lilivyo likaingia CCM. sasa wao watajua namna ya kulipasua. wapinzani swwaaafiiii! Asante Mungu. Baada ya makasheshe yote, Tundu Lissu kupigwa risasi, kina Mbowe kusota rumande siyo mara moja wala mara mbili bali mara kadhaa, akina Lijualikali kunyanyaswa sana, kina Halima Mdee mara rumande mara kuhojiwa bungeni, hatimaye Mungu anatuelekeza Neema tele! Ashukuriwe Mungu.

vipi mkuu kuhusu hawa wabunge na sheria hii ya vyama vya siasa . nasikia ukihama chama lazima uwe umekaa mwaka mmoja ndiyo urudi ulingoni . sasa uchaguzi ni mwakani . wabunge waliopo wa cuf ,inabidi watoke bungeni au waendelee kama watakuwa wanamuunga profesa . .... sipati picha itakuwaje!
 
zaidi ya mada yako kuwa na mpangilio mzuri wa aya , hakuna kingine kinachomfurahisha msomaji kusoma mpaka mwisho. Awali ya yote:
1. umeshindwa kusema ukweli kuwa waliopoteza kwenye huo mchezo ni CHADEMA na CUF na waliopata ni CCM na ACT. hapa kila chama(CCM na ACT) kimepata kadiri inavyoona ni fursa

2.CCM muda wote ulikuwa ukihofia nguvu aliyonayo seif visiwani lakini sasa hiyo nguvu imegawanywa mara mbilil, hivyo CCM hawana cha kupoteza kwa sababu bado nguvu yake ipo palepale.

3. CHADEMA kitakosa ushawishi mikoa ya kusini na zanzibar ambapo ilikuwa ngome kuu ya CUF na Maalimu, na hivyo kuna hati hati CHADEMA kitakua chama cha ukanda wa kaskazini tu na hivyo kupoteza ushawishi kwa kuonekana chama cha kikabila.

4. Maalimu seif ni mjanja sana kacheza na akili ya Mbowe kwa haraka sana. Zito alishtumiwa na CHADEMA kama msaliti na hivyo maalim seif kuhamia ACT ambaye ni mshirika wa UKAWA kutaifanya CHADEMA iikubali ACT ya zito na kusahau yote na hivyo mbowe kula matapishi yake.

5. Condition ambayo zitto atawapa wakitaka ajiunge na ukawa ni yeye kuwa mwenyekiti wa ukawa au mpeperusha bendera ya ukawa uchaguzi wa 2020. je chadema itakubali ? Lissu atakubali? mpasuko mpya unazaliwa tena mkubwa.

6. yote kwa yote , CCM hatuna cha kupoteza katika hili.
Ciciem hamnazo kabisa subiruni uchaguz ufike mtajambia mbali kama mwanamke mwenye matako makubwa hasa hao mbwa wenu wanaokamata watu hovyo na kubambikiza kes wakikaa mita 100.
 
ACT-itaimarika mara dufu wakati huohuo chadema itadhoofika sana!
1.maalimu kahamia act na sio chadema
2. Lowasa kahamia ccm, chadema imepoteza mtu mzoefu na mkomavu ktk siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waungwana na wazalendo wa Tanzania mliopo JF nawasalimu,

Sasa ni Dhahiri kuwa Maalim Seif Sharrif Hamad amehama CUF na kuhamia ACT-Wazalendo. Kuanzia jana, kumekuwa na kuweweseka mno kwa makada wa CCM mitandaoni 'wakijikaza kisabuni' kwa kusema kuwa Maalim Seif ameikacha CHADEMA na kujiunga na ACT-Wazalendo iliyo chini ya Zitto Zuberi Kabwe Ruyagwa.

Mwaka 2015, CUF iliyokuwa ikiongozwa na Maalim Seif na Lipumba (kabla Lipumba hajajiweka mbali nao wakati wa uchaguzi) ilishirikiana na CHADEMA na vyama vingine vya NCCR-Mageuzi na NLD katika mwamvuli wa UKAWA. Makada wa CCM walipiga propaganda kuwa huo ulikuwa ni mwanzo wa CUF ya Maalim Seif kumezwa na CHADEMA ya Mbowe.

Ndiyo maana, ulipoibuka mgogoro mkubwa ndani ya CUF kufuatia Prof. Lipumba kurudi madarakani kama Mwenyekiti wake, makada wa CCM walikuwa wakimuunga mkono na kumpigia chapuo Prof. Lipumba. Ilikuwa ni njia ya 'kulipa kisasi kisiasa' kwakuwa tu Maalim Seif alishirikiana na CHADEMA hata kuwapa Mgombea Mwenza mwaka 2015 (Juma Duni Haji).

Propaganda ya kuwa CUF iliyokuwa ikiitwa ya Maalim kudhibitiwa na kumezwa na CHADEMA iling'ang'aniwa na hata kutangazwa vilivyo. Wakati huo, makada wengi wa CCM mitandaoni ikiwemo humu walikuwa upande wa CUF-ya-Lipumba. Maalim Seif alisemwa kuwa amedhibitiwa, anaendeshwa na kuamuliwa na CHADEMA ya Mbowe.

Hatimaye, jana Maalim Seif amejiunga na ACT-Wazalendo badala ya CHADEMA. Maalim Seif (yawezekana alikuwa akizifuatilia propaganda dhidi yake kwa umakini mkubwa) amefanikiwa kuruka kigingi cha propaganda hizo. Watungaji na wasambazaji wa propaganda hizo wamebaki wakiduwaa na kugosagosa wasijue la kufanya au kusema. Wanaweweseka!

Maalim Seif, kisiasa, anajitosheleza. Historia yake tangu akiwa masomoni inambeba ndani ya chama chochote kiwacho. Hakuna chama chochote cha siasa hapa Tanzania ambacho kinaweza kummeza Maalim Seif na kumfanya kuwa ni mwanasiasa wa 'kawaida' hasa kwenye siasa za Zanzibar. Ndiyo maana kuhama kwake kunafuatwa na kuhama kwa mamia ya wafuasi wake.

Kuhamia kwakeACT-Wazalendo badala ya CHADEMA ni pigo kwa makada wasio makini wa CCM. Ndiyo maana hawaachi kujipa Imani na kujikaza kisabuni kwa kubadili chenga hiyo kama kuikacha CHADEMA. Maalim ni mwanasiasa nguli na mbobezi. Anaweza 'kushaini' popote atakapojiunga. Kama kushirikiana kisiasa, alipo hapatakuwa ni kikwazo kwake.
Very well said learned brother. I absolutely countenance this. The truth hurts. But when it strikes, the truth is inescapable!
 
Zito akae mguu sawa kuondoka ACT au kufukuzwa.

Akumbuke historia ya Maalim.
Kila alipoingia, kichwa cha kiongozi kinaanguka kwa hila za Maalim.

Historia inatukumbusha, Aboud Jumbe Mwinyi ndani ya CCM,alisalitiwa na Maalim.

James Mapalala je, kuondolewa CUF na kufa kisiasa kazi ya Maalim.

Hamad Rashid Je, naye kutimuliwa kwake CUF kazi ya Maalim.

Lipumba chupuchupu.

Maalim ni Master of Controversies, Zito anza kuzihesabu siku.
 
Sawa Mkuu
 
vipi mkuu kuhusu hawa wabunge na sheria hii ya vyama vya siasa . nasikia ukihama chama lazima uwe umekaa mwaka mmoja ndiyo urudi ulingoni . sasa uchaguzi ni mwakani . wabunge waliopo wa cuf ,inabidi watoke bungeni au waendelee kama watakuwa wanamuunga profesa . .... sipati picha itakuwaje!
Hivi hiyo sheria Magufuli alishamwaga wino eeh? lakini mkuu, sasa hivi ni mwezi March, mwakani march ni mwaka mmoja tayari na uchaguzi ni October. kwa hiyo nadhani hiyo si tatizo. au?
 
Back
Top Bottom