Fahamu kwanini makada wa CCM wanaweweseka kuhusu Maalim Seif kuhamia ACT-Wazalendo badala ya CHADEMA

Ccm inadhani kuiua chadema ndio kuua upinzani sasa wameongeza adui mwingine mwenye nguvu ACT itabidi wajipange upya zile siasa za figisu zinamwisho

Sent using Jamii Forums mobile app
Angalau wewe mtazamo wako una mwelekeo wa ukweli kuwa chama cha siasa kitakacho athirika ni CHADEMA. Kwa upande mmoja CHADEMA imepoteza nguvu ya kisiasa ya Lowassa, Tanzania Bara, na kwa upande mwingine CHADEMA imepoteza nguvu ya kisiasa ya Seif, Zanzibar.

Baada ya chaguzi za kitaifa zijazo, CHADEMA hakitakuwa chama kikuu cha upinzani tena. Ila matokeo yake CCM imejijenga zaidi kisiasa Tanzania Bara na Visiwani, ikizingatiwa jinsi Rais Magifuli alivyofanikiwa kuendesha siasa za kuwalenga wanyonge kwa vitendo badala ya siasa za majukwaani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akili kama yako hawana kina Mbowe na wafuasi wao waa mitandaini. Wao wanadhani kumlata rais ni kuunda serikali. Hawa jamaa siwaamini hata kidogo wataishia kuwa madikteta kama wakifanikiwa kumweka mtu magigoni.

Kwa jinsi sheria zetu zilivyo za kishenzi na udhaifu mkubwa wa kikatiba kwenye madaraka makubwa ya urais, ukipata urais hata ukiwa na wabunge wachache ni rahisi kulivunja bunge, kisha kutangaza uchaguzi upya. Wakati wa uchaguzi unatumia mamlaka yako ya urais kuvigeuza vyombo vya kimamlaka kama tume ya uchaguzi na vyombo vya dola kuhakikisha wagombea wa chama chako wanatangazwa washindi bila kujali matokeo ya box la kura.

Haya ndio mambo yanayotokea sana hasa hapa nchini kwenye box la kura. Madaraka ya urais ndio huamua matoke ya kura yaweje wangalau kwa 40%. Kubali kataa lakini habari ndio hiyo.
 
zaidi ya mada yako kuwa na mpangilio mzuri wa aya , hakuna kingine kinachomfurahisha msomaji kusoma mpaka mwisho. Awali ya yote:
1. umeshindwa kusema ukweli kuwa waliopoteza kwenye huo mchezo ni CHADEMA na CUF na waliopata ni CCM na ACT. hapa kila chama(CCM na ACT) kimepata kadiri inavyoona ni fursa

2.CCM muda wote ulikuwa ukihofia nguvu aliyonayo seif visiwani lakini sasa hiyo nguvu imegawanywa mara mbilil, hivyo CCM hawana cha kupoteza kwa sababu bado nguvu yake ipo palepale.

3. CHADEMA kitakosa ushawishi mikoa ya kusini na zanzibar ambapo ilikuwa ngome kuu ya CUF na Maalimu, na hivyo kuna hati hati CHADEMA kitakua chama cha ukanda wa kaskazini tu na hivyo kupoteza ushawishi kwa kuonekana chama cha kikabila.

4. Maalimu seif ni mjanja sana kacheza na akili ya Mbowe kwa haraka sana. Zito alishtumiwa na CHADEMA kama msaliti na hivyo maalim seif kuhamia ACT ambaye ni mshirika wa UKAWA kutaifanya CHADEMA iikubali ACT ya zito na kusahau yote na hivyo mbowe kula matapishi yake.

5. Condition ambayo zitto atawapa wakitaka ajiunge na ukawa ni yeye kuwa mwenyekiti wa ukawa au mpeperusha bendera ya ukawa uchaguzi wa 2020. je chadema itakubali ? Lissu atakubali? mpasuko mpya unazaliwa tena mkubwa.

6. yote kwa yote , CCM hatuna cha kupoteza katika hili.
7. Maalimu ni pandikizi la CCM kama alivyo Lipumba... Hakuna bifu ila ni unono kwa CCM
 
Waungwana na wazalendo wa Tanzania mliopo JF nawasalimu,

Sasa ni Dhahiri kuwa Maalim Seif Sharrif Hamad amehama CUF na kuhamia ACT-Wazalendo. Kuanzia jana, kumekuwa na kuweweseka mno kwa makada wa CCM mitandaoni 'wakijikaza kisabuni' kwa kusema kuwa Maalim Seif ameikacha CHADEMA na kujiunga na ACT-Wazalendo iliyo chini ya Zitto Zuberi Kabwe Ruyagwa.

Mwaka 2015, CUF iliyokuwa ikiongozwa na Maalim Seif na Lipumba (kabla Lipumba hajajiweka mbali nao wakati wa uchaguzi) ilishirikiana na CHADEMA na vyama vingine vya NCCR-Mageuzi na NLD katika mwamvuli wa UKAWA. Makada wa CCM walipiga propaganda kuwa huo ulikuwa ni mwanzo wa CUF ya Maalim Seif kumezwa na CHADEMA ya Mbowe.

Ndiyo maana, ulipoibuka mgogoro mkubwa ndani ya CUF kufuatia Prof. Lipumba kurudi madarakani kama Mwenyekiti wake, makada wa CCM walikuwa wakimuunga mkono na kumpigia chapuo Prof. Lipumba. Ilikuwa ni njia ya 'kulipa kisasi kisiasa' kwakuwa tu Maalim Seif alishirikiana na CHADEMA hata kuwapa Mgombea Mwenza mwaka 2015 (Juma Duni Haji).

Propaganda ya kuwa CUF iliyokuwa ikiitwa ya Maalim kudhibitiwa na kumezwa na CHADEMA iling'ang'aniwa na hata kutangazwa vilivyo. Wakati huo, makada wengi wa CCM mitandaoni ikiwemo humu walikuwa upande wa CUF-ya-Lipumba. Maalim Seif alisemwa kuwa amedhibitiwa, anaendeshwa na kuamuliwa na CHADEMA ya Mbowe.

Hatimaye, jana Maalim Seif amejiunga na ACT-Wazalendo badala ya CHADEMA. Maalim Seif (yawezekana alikuwa akizifuatilia propaganda dhidi yake kwa umakini mkubwa) amefanikiwa kuruka kigingi cha propaganda hizo. Watungaji na wasambazaji wa propaganda hizo wamebaki wakiduwaa na kugosagosa wasijue la kufanya au kusema. Wanaweweseka!

Maalim Seif, kisiasa, anajitosheleza. Historia yake tangu akiwa masomoni inambeba ndani ya chama chochote kiwacho. Hakuna chama chochote cha siasa hapa Tanzania ambacho kinaweza kummeza Maalim Seif na kumfanya kuwa ni mwanasiasa wa 'kawaida' hasa kwenye siasa za Zanzibar. Ndiyo maana kuhama kwake kunafuatwa na kuhama kwa mamia ya wafuasi wake.

Kuhamia kwakeACT-Wazalendo badala ya CHADEMA ni pigo kwa makada wasio makini wa CCM. Ndiyo maana hawaachi kujipa Imani na kujikaza kisabuni kwa kubadili chenga hiyo kama kuikacha CHADEMA. Maalim ni mwanasiasa nguli na mbobezi. Anaweza 'kushaini' popote atakapojiunga. Kama kushirikiana kisiasa, alipo hapatakuwa ni kikwazo kwake.
Maalimu Seif ndio atakayeikomboa Zanzibar chini ya Utawala wa Mkoloni Mweusi SISIEMU,Wanzanzibar muendelee kumpa ushirikiano,CCM inamuogopa Maalim kwa sababu wanajua Maalim anataka kuikomboa Znz,Maalim anataka ZNZ huru!! Muungano unawaumiza wazanzibar.
 
Angalau wewe mtazamo wako una mwelekeo wa ukweli kuwa chama cha siasa kitakacho athirika ni CHADEMA. Kwa upande mmoja CHADEMA imepoteza nguvu ya kisiasa ya Lowassa, Tanzania Bara, na kwa upande mwingine CHADEMA imepoteza nguvu ya kisiasa ya Seif, Zanzibar.

Baada ya chaguzi za kitaifa zijazo, CHADEMA hakitakuwa chama kikuu cha upinzani tena. Ila matokeo yake CCM imejijenga zaidi kisiasa Tanzania Bara na Visiwani, ikizingatiwa jinsi Rais Magifuli alivyofanikiwa kuendesha siasa za kuwalenga wanyonge kwa vitendo badala ya siasa za majukwaani.

Sent using Jamii Forums mobile app

Acha upotoshaji, cdm hawajawahi kuwa na kiti cha ubunge wala udiwani huko ZnZ. Cdm hawana cha kuathirika kwani sehemu walizoshinda ni bara tena sehemu kubwa wamehujumiwa. Nguvu ya Seif iko ZnZ na sio huku bara. Ni kweli ACT inaweza kuwa chama kikuu cha upinzani kwa sababu ya viti vingi vya uwakilishi bungeni toka ZnZ, lakini kuwa chama kikuu cha upinzani na hali ya sifa zaidi lakini sio nguvu hasa ya cheo hicho. Halafu usituone sisi ni watoto, Lowassa hajawahi kuwa na nguvu yoyote ya kisiasa ambayo hasa aliileta cdm. Kura alizopata Lowassa cdm, hata asingegombea yeye bado cdm ingezipata hata zaidi.

Ccm hajajijenga zaidi kisiasa, bali matumizi mabaya ya madaraka kupitia mwenyekiti wa ccm ambaye ni rais, kutumia nafasi yake kuua ushindani wa kisiasa na kuweka matumizi makubwa ya vyombo vya dola, ikiwepo kutokuheshimu box la kura. Mtu mjinga tu ndio anaweza kusema ccm imeimarika kwa kuangalia matokeo ya kura au yatakayopatikana kupitia box la kura katika mazingira haya ya awamu ya tano, ambapo tunaona wazi kwa macho yetu hujuma za wazi ili ccm watangazwe washindi, hali inayopelekea wapiga kura wengi kutokujitokeza kupiga kura.

Huu upotoshaji unaofanywa kwa makusudi kuonyesha eti cdm imeathirika kwa Seif kujiunga ACT na kwamba ACT na ccm ndio wamefaidika huku cdm ikipoteza ni propaganda mfu ili kupanga matokeo yaendane na propaganda hiyo. Ukweli ni kuwa cdm ni tishio la kweli la ccm hapa Tanzania, hivyo lazima zitumike njia nzuri na hasa hasa mbovu ili kuiua cdm. Ukweli uko wazi, cdm inaweza kuchukua utawala wa nchi hii bila kupata hata kura moja huko ZnZ.
 
Unajua China ina miaka 1000 chini ya Authoritarian GVT hawajui hata democracy inafananaje,

Sent using Jamii Forums mobile app

Na hili ndilo tatizo Tanzania ikianza kuhesabu moja (1), mpaka tufikie huko kwa miaka 1000!
Ni kizazi cha ngapi hicho tokea sasa?

Sio hivyo tu, kwa vile tumekwishaonja onja chembechembe za mtindo wa Demokrasia, kutuweka katika mfumo wa China ni lazima pawepo (lag time), kutokana na mivurugano mikubwa itakayotokana hadi wote tuwekwe sawa kwa shurti kuufuata mtindo huo wakati huu.

Bado, usisahau mazingira tuliyomo sasa. Dunia nzima imebadilika, sivyo ilivyokuwa wakati waChina wanajifungia makwao wasijihusishe na mengine yatokeayo duniani. Dunia sasa hivi ni kijiji. Kuiondoa Tanzania isionekane katika kijiji hicho sio kazi rahisi.

Watafanya makosa makubwa wakishupaza shingo zao na kutufanya 'tusalimu amri - total submission.' Itawalazimu wafanye kazi kubwa sana!
 
Ni ndoto za alinacha na mchana kweupe kuamini Maalim Seif kuhamia ACT Mzalendo kutaitikisa CCM. Badala yake kuhama huko kunavunja nguvu ya Upinzani Tanzania Bara na Zanzibar.

Mifano iko mingi kutetea hoja yangu ila moja kubwa ni kuhama kwa Lowassa CCM kulivyoshindwa kuvunja nguvu ya CCM, Tanzania Bara. Ila kuhama kwa Seif CUF, kumevunja nguvu ya CUF Tanzania Visiwani.

La msingi ni kuangalia jinsi muungano wa Zitto na Seif utavyobadili mitazamo yao kisera na kiitikadi.

Ila lililohitokeza ni kwamba baadhi ya Watanzania, imegundulika, hawajiungi na vyama vya siasa kwa sababu ya Sera na Itakadi ya chama husika bali kwa sababu ya kiongozi fulani.

Katika mantiki hiyo, maswali ya kujiuliza, Je, Zitto ana wafuasi wa kumpa Seif nguvu Zanzibar? Na je, wafuasi wa Seif Tanzania bara watamwongezea Zitto nguvu kisiasa au watabaki CUF ya Prof Lipumba?

Wakati ndio mwamuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nakubaliana na ww kabisa kuwa Seif kuhamia ACT hakuwezi kuitikisa ccm, ukweli ni kuwa ccm haishindani kama chama cha siasa. Nguvu ya ccm haipo kisiasa bali ni mwingiliano wa ccm na vyombo vya dola. Iwapo ccm itasimama na kushindana na vyama vingine bila kubebwa na vyombo vya dola, ni nadra ccm kupata kura zaidi ya 50%.

Unasema kuhama kwa Lowassa ndani ya ccm hukujavunja nguvu ya ccm. Ukweli ni Lowassa hakuwa na nguvu yoyote, zaidi ya kucheza siasa za ndani ya ccm inayotegemea nguvu ya dola. Ukitaka kujua kuwa Lowassa hakuwa na nguvu yoyote, ukiacha hayo mahubiri ya kura zinazosemwa alizoleta cdm, ni tawi lipi alifungua ndani ya cdm? Yeye na wanaccm wenzake wote hawawezi kufanya siasa nje ya vyombo vya dola.
 
CCM hajawahi kuhofia chama cha upinzani chochote maana yeye ana vyombo vya kumfanya ashinde hata akishindwa

Na hili halina mjadala, si hapa JF wala huko kwenye vyama vya upinzani kwenyewe.

Ndiyo maana halijadiliwi kwa mapana yake jinsi ya kuliondoa tatizo hili; au sio tatizo?

Kwa hiyo kila mtu anasubiri uchaguzi ufike, CCM ishinde, nasi tubaki tukilalamika kuhujumiwa!
 
Zanzibar ni Maalim Seif tutake tusitake. Ni habari njema ametua upinzani na siyo ccm inabidi atembeze sindano iwaingie wabaya wetu
 
Nakubaliana na ww kabisa kuwa Seif kuhamia ACT hakuwezi kuitikisa ccm, ukweli ni kuwa ccm haishindani kama chama cha siasa. Nguvu ya ccm haipo kisiasa bali ni mwingiliano wa ccm na vyombo vya dola. Iwapo ccm itasimama na kushindana na vyama vingine bila kubebwa na vyombo vya dola, ni nadra ccm kupata kura zaidi ya 50%.

Unasema kuhama kwa Lowassa ndani ya ccm hukujavunja nguvu ya ccm. Ukweli ni Lowassa hakuwa na nguvu yoyote, zaidi ya kucheza siasa za ndani ya ccm inayotegemea nguvu ya dola. Ukitaka kujua kuwa Lowassa hakuwa na nguvu yoyote, ukiacha hayo mahubiri ya kura zinazosemwa alizoleta cdm, ni tawi lipi alifungua ndani ya cdm? Yeye na wanaccm wenzake wote hawawezi kufanya siasa nje ya vyombo vya dola.

Wasema Ukweli ni Lowassa hakuwa na nguvu yoyote, zaidi ya kucheza siasa za ndani ya ccm inayotegemea nguvu ya dola, uchambuzi wangu ni kama ifuatavyo:

1) Sijaona chama kingine cha siasa chenye Itikadi na Sera zinazolenga kuleta mabadiliko ya kweli Kijamii, Kisiasa, Kiuchumi na Kiteknolojia kama CCM.

2) Kinachojitokeza nchini ni ushabiki wa umaarufu wa mwanasiasa fulani. Km leo hii Lissu akirudi nchini, akaanzisha chama chake, atapata kundi la wafuasi hata kama hawajui agenda yake ni nini.

3) Hakuna ubishi kuwa Maalim Seif si mwanasiasa ila mtu mwenye uchu wa madaraka. Alipoteuliwa kuwa Makamu wa Rais kwenye Serikali ya Muungano alitulia. Sasa anaingia ACT Mzalendo ateuliwe tena kugombea Urais wa Zanzibar. Hivyo kitendo cha kupewa kadi na 1 ya ACT Mzalendo ni kutukuza ukuu wake anaoutaka.

MTAENDELEA KUCHEZWA AKILI ZENU NA WANA SIASA UCHWARA (WANAFIKI NA WENYE UCHU WA MADARAKA)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii game plan imechezwa kwa ustadi wa hali ya juu na team lumumba..ili kuidhoofisha chadema.. ccm wanateseka kinafki....mzee..!!.wamepunguza pressure ya uchaguzi kwao..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasema Ukweli ni Lowassa hakuwa na nguvu yoyote, zaidi ya kucheza siasa za ndani ya ccm inayotegemea nguvu ya dola, uchambuzi wangu ni kama ifuatavyo:

1) Sijaona chama kingine cha siasa chenye Itikadi na Sera zinazolenga kuleta mabadiliko ya kweli Kijamii, Kisiasa, Kiuchumi na Kiteknolojia kama CCM.

2) Kinachojitokeza nchini ni ushabiki wa umaarufu wa mwanasiasa fulani. Km leo hii Lissu akirudi nchini, akaanzisha chama chake, atapata kundi la wafuasi hata kama hawajui agenda yake ni nini.

3) Hakuna ubishi kuwa Maalim Seif si mwanasiasa ila mtu mwenye uchu wa madaraka. Alipoteuliwa kuwa Makamu wa Rais kwenye Serikali ya Muungano alitulia. Sasa anaingia ACT Mzalendo ateuliwe tena kugombea Urais wa Zanzibar. Hivyo kitendo cha kupewa kadi na 1 ya ACT Mzalendo ni kutukuza ukuu wake anaoutaka.

MTAENDELEA KUCHEZWA AKILI ZENU NA WANA SIASA UCHWARA (WANAFIKI NA WENYE UCHU WA MADARAKA)

Sent using Jamii Forums mobile app

Bora kushinda home na mke wangu kuliko kusikilia siasa

***Subhanallah ***
 
Maalimu Seif ndio atakayeikomboa Zanzibar chini ya Utawala wa Mkoloni Mweusi SISIEMU,Wanzanzibar muendelee kumpa ushirikiano,CCM inamuogopa Maalim kwa sababu wanajua Maalim anataka kuikomboa Znz,Maalim anataka ZNZ huru!! Muungano unawaumiza wazanzibar.
I see...sikuwa najua Mkuu
 
Wasema Ukweli ni Lowassa hakuwa na nguvu yoyote, zaidi ya kucheza siasa za ndani ya ccm inayotegemea nguvu ya dola, uchambuzi wangu ni kama ifuatavyo:

1) Sijaona chama kingine cha siasa chenye Itikadi na Sera zinazolenga kuleta mabadiliko ya kweli Kijamii, Kisiasa, Kiuchumi na Kiteknolojia kama CCM.

2) Kinachojitokeza nchini ni ushabiki wa umaarufu wa mwanasiasa fulani. Km leo hii Lissu akirudi nchini, akaanzisha chama chake, atapata kundi la wafuasi hata kama hawajui agenda yake ni nini.

3) Hakuna ubishi kuwa Maalim Seif si mwanasiasa ila mtu mwenye uchu wa madaraka. Alipoteuliwa kuwa Makamu wa Rais kwenye Serikali ya Muungano alitulia. Sasa anaingia ACT Mzalendo ateuliwe tena kugombea Urais wa Zanzibar. Hivyo kitendo cha kupewa kadi na 1 ya ACT Mzalendo ni kutukuza ukuu wake anaoutaka.

MTAENDELEA KUCHEZWA AKILI ZENU NA WANA SIASA UCHWARA (WANAFIKI NA WENYE UCHU WA MADARAKA)

Sent using Jamii Forums mobile app

Narudia tena kwa msisitizo.

Ccm sio chama cha kisiasa tena kwa maana ya siasa, bali ni taasisi ya kidola inayoweza kupata madaraka kwa kutumia udhaifu wa katiba kupitia mamlaka ya rais. Ccm haina uwezo bali ndio iliyopo madarakani na inaweza kutumia kodi za wananchi kufanya lolote itakalo na wala sio kufanya watakavyo wao. Mfano mrahisi ni katiba mpya. Katiba mpya hasa ya rasimu ya Warioba ilibeba maslahi ya umma, lakini genge la ccm lilibadili maoni ya wananchi kwa manufaa ya hilo genge linalojiita ccm.

Utasema ccm ina sera, ukisikiliza sera zao ni eti ni kuleta maji, umeme, barabara nk. Hata mimi kwangu nimelipia kupata huduma ya maji, umeme nk, je niambie familia yangu hiyo ni sera? Kutokana na udhaifu wa katiba ccm inaweza kuendelea kukaa madarakani ikifanya majaribio ya sera zake bila kujali faida au hasara kwa taifa. Wangalau wakati wa Nyerere ccm ilikuwa na sera ya ujamaa na kujitegemea. Ila baada ya hapo nchi yetu haiendeshwi na sera bali utashi wa rais aliye madarakani.

Ccm pia ni taasisi ya kidola yenye uchu wa madaraka na uthibitisho wa dhahiri ni kilichotokea uchaguzi wa Znz 2015, tafauti ya hilo genge la ccm na Seif kwenye uchu kwa madaraka, ccm inakuja kwa jina la taasisi na Seif anatokea zaidi kama mtu.
 
I see...sikuwa najua Mkuu
Leo tulia tukufunde mngoni kama hukulijua hilo.

Sipendi kukubishia ulichokiandika lakini ukweli ccm hawaweweseji maana wana mtaji mkubwa sana Policcm. Kwao kuweweseka ni kufanya unafiki na nadhani watu wameshaingia kwenye mtego.
Maalim Seif ni tishio tangu zamani sioni kigeni atakachokileta ndani ya ACT.
 
Narudia tena kwa msisitizo.

Ccm sio chama cha kisiasa tena kwa maana ya siasa, bali ni taasisi ya kidola inayoweza kupata madaraka kwa kutumia udhaifu wa katiba kupitia mamlaka ya rais. Ccm haina uwezo bali ndio iliyopo madarakani na inaweza kutumia kodi za wananchi kufanya lolote itakalo na wala sio kufanya watakavyo wao. Mfano mrahisi ni katiba mpya. Katiba mpya hasa ya rasimu ya Warioba ilibeba maslahi ya umma, lakini genge la ccm lilibadili maoni ya wananchi kwa manufaa ya hilo genge linalojiita ccm.

Utasema ccm ina sera, ukisikiliza sera zao ni eti ni kuleta maji, umeme, barabara nk. Hata mimi kwangu nimelipia kupata huduma ya maji, umeme nk, je niambie familia yangu hiyo ni sera? Kutokana na udhaifu wa katiba ccm inaweza kuendelea kukaa madarakani ikifanya majaribio ya sera zake bila kujali faida au hasara kwa taifa. Wangalau wakati wa Nyerere ccm ilikuwa na sera ya ujamaa na kujitegemea. Ila baada ya hapo nchi yetu haiendeshwi na sera bali utashi wa rais aliye madarakani.

Ccm pia ni taasisi ya kidola yenye uchu wa madaraka na uthibitisho wa dhahiri ni kilichotokea uchaguzi wa Znz 2015, tafauti ya hilo genge la ccm na Seif kwenye uchu kwa madaraka, ccm inakuja kwa jina la taasisi na Seif anatokea zaidi kama mtu.
Kipi kigeni ambacho Maalim Seif atakileta ACT tofauri na miaka 20 huko nyuma?
Kama alishindwa huko nyuma pamoja na kuwepo ruhusa ya mikutano ya hadhara ndiyo ataweza sasa kwenye mikutano ya mitandaoni?

Mbona watu na umakini wenu mnaingia kirshisi kwenye mtego wa ccm kama watoto wadogo.
Mnajitokeza wengi kuwa wataalamu wa sayansi ya kisiasa???

Seif hajawahi kuwa force of reckoning kama Mrema 1995 na wote mashahidi ndiyo leo mtaweza wakati vyama vyenyewe vipo kimakundi?

Tusubiri 2020 novemba wabunge wakivaa suti nyeusi kama wamefiwa na kuziba midomo kwa tape.
 
Ww lazima utakuwa ni mzee ndio maana unakuja na propaganda zilizoasisiwa na wazee ndani ya ccm. Tutajie siku waligombea ruzuku au kugombea kambi ya upinzani bungeni. Peleka siasa za kizee mbali.
siyo mzee tu, malizia mzee meko
 
3. CHADEMA kitakosa ushawishi mikoa ya kusini na zanzibar ambapo ilikuwa ngome kuu ya CUF na Maalimu, na hivyo kuna hati hati CHADEMA kitakua chama cha ukanda wa kaskazini tu na hivyo kupoteza ushawishi kwa kuonekana chama cha kikabila.
Wabunge wote wa chadema na halmashauri zinazoongozwa na chadema ni za kaskazini au ni za kikabila?
 
Waungwana na wazalendo wa Tanzania mliopo JF nawasalimu,

Sasa ni Dhahiri kuwa Maalim Seif Sharrif Hamad amehama CUF na kuhamia ACT-Wazalendo. Kuanzia jana, kumekuwa na kuweweseka mno kwa makada wa CCM mitandaoni 'wakijikaza kisabuni' kwa kusema kuwa Maalim Seif ameikacha CHADEMA na kujiunga na ACT-Wazalendo iliyo chini ya Zitto Zuberi Kabwe Ruyagwa.

Mwaka 2015, CUF iliyokuwa ikiongozwa na Maalim Seif na Lipumba (kabla Lipumba hajajiweka mbali nao wakati wa uchaguzi) ilishirikiana na CHADEMA na vyama vingine vya NCCR-Mageuzi na NLD katika mwamvuli wa UKAWA. Makada wa CCM walipiga propaganda kuwa huo ulikuwa ni mwanzo wa CUF ya Maalim Seif kumezwa na CHADEMA ya Mbowe.

Ndiyo maana, ulipoibuka mgogoro mkubwa ndani ya CUF kufuatia Prof. Lipumba kurudi madarakani kama Mwenyekiti wake, makada wa CCM walikuwa wakimuunga mkono na kumpigia chapuo Prof. Lipumba. Ilikuwa ni njia ya 'kulipa kisasi kisiasa' kwakuwa tu Maalim Seif alishirikiana na CHADEMA hata kuwapa Mgombea Mwenza mwaka 2015 (Juma Duni Haji).

Propaganda ya kuwa CUF iliyokuwa ikiitwa ya Maalim kudhibitiwa na kumezwa na CHADEMA iling'ang'aniwa na hata kutangazwa vilivyo. Wakati huo, makada wengi wa CCM mitandaoni ikiwemo humu walikuwa upande wa CUF-ya-Lipumba. Maalim Seif alisemwa kuwa amedhibitiwa, anaendeshwa na kuamuliwa na CHADEMA ya Mbowe.

Hatimaye, jana Maalim Seif amejiunga na ACT-Wazalendo badala ya CHADEMA. Maalim Seif (yawezekana alikuwa akizifuatilia propaganda dhidi yake kwa umakini mkubwa) amefanikiwa kuruka kigingi cha propaganda hizo. Watungaji na wasambazaji wa propaganda hizo wamebaki wakiduwaa na kugosagosa wasijue la kufanya au kusema. Wanaweweseka!

Maalim Seif, kisiasa, anajitosheleza. Historia yake tangu akiwa masomoni inambeba ndani ya chama chochote kiwacho. Hakuna chama chochote cha siasa hapa Tanzania ambacho kinaweza kummeza Maalim Seif na kumfanya kuwa ni mwanasiasa wa 'kawaida' hasa kwenye siasa za Zanzibar. Ndiyo maana kuhama kwake kunafuatwa na kuhama kwa mamia ya wafuasi wake.

Kuhamia kwakeACT-Wazalendo badala ya CHADEMA ni pigo kwa makada wasio makini wa CCM. Ndiyo maana hawaachi kujipa Imani na kujikaza kisabuni kwa kubadili chenga hiyo kama kuikacha CHADEMA. Maalim ni mwanasiasa nguli na mbobezi. Anaweza 'kushaini' popote atakapojiunga. Kama kushirikiana kisiasa, alipo hapatakuwa ni kikwazo kwake.
Haaa uchizi huuu sasa uchambuzi gani huu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom