Fahamu kwanini makada wa CCM wanaweweseka kuhusu Maalim Seif kuhamia ACT-Wazalendo badala ya CHADEMA

Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,554
2,000
Waungwana na wazalendo wa Tanzania mliopo JF nawasalimu,

Sasa ni Dhahiri kuwa Maalim Seif Sharrif Hamad amehama CUF na kuhamia ACT-Wazalendo. Kuanzia jana, kumekuwa na kuweweseka mno kwa makada wa CCM mitandaoni 'wakijikaza kisabuni' kwa kusema kuwa Maalim Seif ameikacha CHADEMA na kujiunga na ACT-Wazalendo iliyo chini ya Zitto Zuberi Kabwe Ruyagwa.

Mwaka 2015, CUF iliyokuwa ikiongozwa na Maalim Seif na Lipumba (kabla Lipumba hajajiweka mbali nao wakati wa uchaguzi) ilishirikiana na CHADEMA na vyama vingine vya NCCR-Mageuzi na NLD katika mwamvuli wa UKAWA. Makada wa CCM walipiga propaganda kuwa huo ulikuwa ni mwanzo wa CUF ya Maalim Seif kumezwa na CHADEMA ya Mbowe.

Ndiyo maana, ulipoibuka mgogoro mkubwa ndani ya CUF kufuatia Prof. Lipumba kurudi madarakani kama Mwenyekiti wake, makada wa CCM walikuwa wakimuunga mkono na kumpigia chapuo Prof. Lipumba. Ilikuwa ni njia ya 'kulipa kisasi kisiasa' kwakuwa tu Maalim Seif alishirikiana na CHADEMA hata kuwapa Mgombea Mwenza mwaka 2015 (Juma Duni Haji).

Propaganda ya kuwa CUF iliyokuwa ikiitwa ya Maalim kudhibitiwa na kumezwa na CHADEMA iling'ang'aniwa na hata kutangazwa vilivyo. Wakati huo, makada wengi wa CCM mitandaoni ikiwemo humu walikuwa upande wa CUF-ya-Lipumba. Maalim Seif alisemwa kuwa amedhibitiwa, anaendeshwa na kuamuliwa na CHADEMA ya Mbowe.

Hatimaye, jana Maalim Seif amejiunga na ACT-Wazalendo badala ya CHADEMA. Maalim Seif (yawezekana alikuwa akizifuatilia propaganda dhidi yake kwa umakini mkubwa) amefanikiwa kuruka kigingi cha propaganda hizo. Watungaji na wasambazaji wa propaganda hizo wamebaki wakiduwaa na kugosagosa wasijue la kufanya au kusema. Wanaweweseka!

Maalim Seif, kisiasa, anajitosheleza. Historia yake tangu akiwa masomoni inambeba ndani ya chama chochote kiwacho. Hakuna chama chochote cha siasa hapa Tanzania ambacho kinaweza kummeza Maalim Seif na kumfanya kuwa ni mwanasiasa wa 'kawaida' hasa kwenye siasa za Zanzibar. Ndiyo maana kuhama kwake kunafuatwa na kuhama kwa mamia ya wafuasi wake.

Kuhamia kwakeACT-Wazalendo badala ya CHADEMA ni pigo kwa makada wasio makini wa CCM. Ndiyo maana hawaachi kujipa Imani na kujikaza kisabuni kwa kubadili chenga hiyo kama kuikacha CHADEMA. Maalim ni mwanasiasa nguli na mbobezi. Anaweza 'kushaini' popote atakapojiunga. Kama kushirikiana kisiasa, alipo hapatakuwa ni kikwazo kwake.
 
bababikko

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
2,393

Hii in kama alivyopiga goli la kwanza Sadio Mane dhidi ya Bayern Munich

Sent using Jamii Forums mobile app
 
900 Inapendeza zaidi

JF-Expert Member
Nov 19, 2017
3,135

Pigo lingine kwa ccm,upinzani hauwezi kufa Tz,ccm iachane na mawazo ya china
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
38,278
2,000
Uenda Makada wa Chadema wanateseka ziadi ya makada wa CCM..! Kazi kwenu kugombania Ruzuku na kugombania kambi rasmi ya upinzani Bungeni CCM wala hawana presha na ACT

Ww lazima utakuwa ni mzee ndio maana unakuja na propaganda zilizoasisiwa na wazee ndani ya ccm. Tutajie siku waligombea ruzuku au kugombea kambi ya upinzani bungeni. Peleka siasa za kizee mbali.
 
FPT

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
952
1,000
zaidi ya mada yako kuwa na mpangilio mzuri wa aya , hakuna kingine kinachomfurahisha msomaji kusoma mpaka mwisho. Awali ya yote:
1. umeshindwa kusema ukweli kuwa waliopoteza kwenye huo mchezo ni CHADEMA na CUF na waliopata ni CCM na ACT. hapa kila chama(CCM na ACT) kimepata kadiri inavyoona ni fursa

2.CCM muda wote ulikuwa ukihofia nguvu aliyonayo seif visiwani lakini sasa hiyo nguvu imegawanywa mara mbilil, hivyo CCM hawana cha kupoteza kwa sababu bado nguvu yake ipo palepale.

3. CHADEMA kitakosa ushawishi mikoa ya kusini na zanzibar ambapo ilikuwa ngome kuu ya CUF na Maalimu, na hivyo kuna hati hati CHADEMA kitakua chama cha ukanda wa kaskazini tu na hivyo kupoteza ushawishi kwa kuonekana chama cha kikabila.

4. Maalimu seif ni mjanja sana kacheza na akili ya Mbowe kwa haraka sana. Zito alishtumiwa na CHADEMA kama msaliti na hivyo maalim seif kuhamia ACT ambaye ni mshirika wa UKAWA kutaifanya CHADEMA iikubali ACT ya zito na kusahau yote na hivyo mbowe kula matapishi yake.

5. Condition ambayo zitto atawapa wakitaka ajiunge na ukawa ni yeye kuwa mwenyekiti wa ukawa au mpeperusha bendera ya ukawa uchaguzi wa 2020. je chadema itakubali ? Lissu atakubali? mpasuko mpya unazaliwa tena mkubwa.

6. yote kwa yote , CCM hatuna cha kupoteza katika hili.
 
Nnyindojihadini

JF-Expert Member
Nov 12, 2018
643
500
Maalimu Seif Sharif kuhamia ACT sababu ni hizi: Kamshindwa Prof Lipumba moja, muondo wa,ACT ni wa dola la Kiiran kuna cheo cha kiongozi mkuu/Ayattolah. Maalim Seif ana sifa zilizopitiliza za kuwa Ayatollah wa ACT, mbili. Nawashauri ACT wampe hiki cheo cha mkuu/Ayetollah wa chama ili awe taswira ya chama chao.

Mwisho muosha huoshwa,kama alivyo muosha James Mapalala kipindi cha nyuma naye kipindi hichi kapata kiboko yake wa kumuosha kwa jina la Prof Lipumba.
 
mitigator

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
4,959
2,000
zaidi ya mada yako kuwa na mpangilio mzuri wa aya , hakuna kingine kinachomfurahisha msomaji kusoma mpaka mwisho. Awali ya yote:
1. umeshindwa kusema ukweli kuwa waliopoteza kwenye huo mchezo ni CHADEMA na CUF na waliopata ni CCM na ACT. hapa kila chama(CCM na ACT) kimepata kadiri inavyoona ni fursa

2.CCM muda wote ulikuwa ukihofia nguvu aliyonayo seif visiwani lakini sasa hiyo nguvu imegawanywa mara mbilil, hivyo CCM hawana cha kupoteza kwa sababu bado nguvu yake ipo palepale.

3. CHADEMA kitakosa ushawishi mikoa ya kusini na zanzibar ambapo ilikuwa ngome kuu ya CUF na Maalimu, na hivyo kuna hati hati CHADEMA kitakua chama cha ukanda wa kaskazini tu na hivyo kupoteza ushawishi kwa kuonekana chama cha kikabila.

4. Maalimu seif ni mjanja sana kacheza na akili ya Mbowe kwa haraka sana. Zito alishtumiwa na CHADEMA kama msaliti na hivyo maalim seif kuhamia ACT ambaye ni mshirika wa UKAWA kutaifanya CHADEMA iikubali ACT ya zito na kusahau yote na hivyo mbowe kula matapishi yake.

5. Condition ambayo zitto atawapa wakitaka ajiunge na ukawa ni yeye kuwa mwenyekiti wa ukawa au mpeperusha bendera ya ukawa uchaguzi wa 2020. je chadema itakubali ? Lissu atakubali? mpasuko mpya unazaliwa tena mkubwa.

6. yote kwa yote , CCM hatuna cha kupoteza katika hili.
We kenge ulitaka mwandishi afikiri na kuandika kama wew wa Lumumba!!
 
MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
15,706
2,000
Waungwana na wazalendo wa Tanzania mliopo JF nawasalimu,

Sasa ni Dhahiri kuwa Maalim Seif Sharrif Hamad amehama CUF na kuhamia ACT-Wazalendo. Kuanzia jana, kumekuwa na kuweweseka mno kwa makada wa CCM mitandaoni 'wakijikaza kisabuni' kwa kusema kuwa Maalim Seif ameikacha CHADEMA na kujiunga na ACT-Wazalendo iliyo chini ya Zitto Zuberi Kabwe Ruyagwa.

Mwaka 2015, CUF iliyokuwa ikiongozwa na Maalim Seif na Lipumba (kabla Lipumba hajajiweka mbali nao wakati wa uchaguzi) ilishirikiana na CHADEMA na vyama vingine vya NCCR-Mageuzi na NLD katika mwamvuli wa UKAWA. Makada wa CCM walipiga propaganda kuwa huo ulikuwa ni mwanzo wa CUF ya Maalim Seif kumezwa na CHADEMA ya Mbowe.

Ndiyo maana, ulipoibuka mgogoro mkubwa ndani ya CUF kufuatia Prof. Lipumba kurudi madarakani kama Mwenyekiti wake, makada wa CCM walikuwa wakimuunga mkono na kumpigia chapuo Prof. Lipumba. Ilikuwa ni njia ya 'kulipa kisasi kisiasa' kwakuwa tu Maalim Seif alishirikiana na CHADEMA hata kuwapa Mgombea Mwenza mwaka 2015 (Juma Duni Haji).

Propaganda ya kuwa CUF iliyokuwa ikiitwa ya Maalim kudhibitiwa na kumezwa na CHADEMA iling'ang'aniwa na hata kutangazwa vilivyo. Wakati huo, makada wengi wa CCM mitandaoni ikiwemo humu walikuwa upande wa CUF-ya-Lipumba. Maalim Seif alisemwa kuwa amedhibitiwa, anaendeshwa na kuamuliwa na CHADEMA ya Mbowe.

Hatimaye, jana Maalim Seif amejiunga na ACT-Wazalendo badala ya CHADEMA. Maalim Seif (yawezekana alikuwa akizifuatilia propaganda dhidi yake kwa umakini mkubwa) amefanikiwa kuruka kigingi cha propaganda hizo. Watungaji na wasambazaji wa propaganda hizo wamebaki wakiduwaa na kugosagosa wasijue la kufanya au kusema. Wanaweweseka!

Maalim Seif, kisiasa, anajitosheleza. Historia yake tangu akiwa masomoni inambeba ndani ya chama chochote kiwacho. Hakuna chama chochote cha siasa hapa Tanzania ambacho kinaweza kummeza Maalim Seif na kumfanya kuwa ni mwanasiasa wa 'kawaida' hasa kwenye siasa za Zanzibar. Ndiyo maana kuhama kwake kunafuatwa na kuhama kwa mamia ya wafuasi wake.

Kuhamia kwakeACT-Wazalendo badala ya CHADEMA ni pigo kwa makada wasio makini wa CCM. Ndiyo maana hawaachi kujipa Imani na kujikaza kisabuni kwa kubadili chenga hiyo kama kuikacha CHADEMA. Maalim ni mwanasiasa nguli na mbobezi. Anaweza 'kushaini' popote atakapojiunga. Kama kushirikiana kisiasa, alipo hapatakuwa ni kikwazo kwake.
unaposema chadema ya MBOWE unamaanisha?
 
Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
6,349
2,000
zaidi ya mada yako kuwa na mpangilio mzuri wa aya , hakuna kingine kinachomfurahisha msomaji kusoma mpaka mwisho. Awali ya yote:
1. umeshindwa kusema ukweli kuwa waliopoteza kwenye huo mchezo ni CHADEMA na CUF na waliopata ni CCM na ACT. hapa kila chama(CCM na ACT) kimepata kadiri inavyoona ni fursa

2.CCM muda wote ulikuwa ukihofia nguvu aliyonayo seif visiwani lakini sasa hiyo nguvu imegawanywa mara mbilil, hivyo CCM hawana cha kupoteza kwa sababu bado nguvu yake ipo palepale.

3. CHADEMA kitakosa ushawishi mikoa ya kusini na zanzibar ambapo ilikuwa ngome kuu ya CUF na Maalimu, na hivyo kuna hati hati CHADEMA kitakua chama cha ukanda wa kaskazini tu na hivyo kupoteza ushawishi kwa kuonekana chama cha kikabila.

4. Maalimu seif ni mjanja sana kacheza na akili ya Mbowe kwa haraka sana. Zito alishtumiwa na CHADEMA kama msaliti na hivyo maalim seif kuhamia ACT ambaye ni mshirika wa UKAWA kutaifanya CHADEMA iikubali ACT ya zito na kusahau yote na hivyo mbowe kula matapishi yake.

5. Condition ambayo zitto atawapa wakitaka ajiunge na ukawa ni yeye kuwa mwenyekiti wa ukawa au mpeperusha bendera ya ukawa uchaguzi wa 2020. je chadema itakubali ? Lissu atakubali? mpasuko mpya unazaliwa tena mkubwa.

6. yote kwa yote , CCM hatuna cha kupoteza katika hili.
Point No 3 ( of course ndio nilipoishia kusoma) unaweza kunitajia mbunge wa kusini pamoja na Zanzibar kwa kutokea Chadema? If the answer is No then kwanini unadhani sasa hivi hiyo nguvu unayoiongelea huko eti inaweza kupungua ilihali haijawahi kuwepo? Ungenambia CUF kwa Zanzibar ndio kwishiney walau ningekuelewa and hence aliye loose hapo ni CUF na wala sio Chadema. CUF kwa Zanzibar was Maalimu Seif na sasa ndio huyo yupo zake ACT, kama ofisi tu zilianza kubadirishwa rangi kabla hata hajaondoka rasmi then what next to CUF in Zanzibar? Kwa huku bara, wala sio siri, CUF ilinufaika mno kwa uwepo wa UKAWA, miaka yote Cuf hawajawahi kupata walau wabunge 4 wa kuchaguliwa, kwa mgogoro hu ambao kimsingi ulipandikizwa na ccm wenyewe through Lipumba ( niameacha neno prof makusudi) wote wenye akili zao timamu wanajua Lipumba anatumika so kwenye uchaguzi hata afanyaje hawezi hata kuingia kwenye top 3, nasema hawezi. Hata mbeleko ya chuma itumike still hataweza kukanyaga hiyo top 3, kitu pekee ambacho Chadema kinawagharimu kwasasa ni kutokuwepo kwa Dr. Slaa, that is all but the good thing kwa Dr. Slaa yupo nje ya nchi so hawezi kushiriki saana kampeni za mwaka 2020, hilo tu.
 
Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,114
2,000
Waungwana na wazalendo wa Tanzania mliopo JF nawasalimu,

Sasa ni Dhahiri kuwa Maalim Seif Sharrif Hamad amehama CUF na kuhamia ACT-Wazalendo. Kuanzia jana, kumekuwa na kuweweseka mno kwa makada wa CCM mitandaoni 'wakijikaza kisabuni' kwa kusema kuwa Maalim Seif ameikacha CHADEMA na kujiunga na ACT-Wazalendo iliyo chini ya Zitto Zuberi Kabwe Ruyagwa.

Mwaka 2015, CUF iliyokuwa ikiongozwa na Maalim Seif na Lipumba (kabla Lipumba hajajiweka mbali nao wakati wa uchaguzi) ilishirikiana na CHADEMA na vyama vingine vya NCCR-Mageuzi na NLD katika mwamvuli wa UKAWA. Makada wa CCM walipiga propaganda kuwa huo ulikuwa ni mwanzo wa CUF ya Maalim Seif kumezwa na CHADEMA ya Mbowe.

Ndiyo maana, ulipoibuka mgogoro mkubwa ndani ya CUF kufuatia Prof. Lipumba kurudi madarakani kama Mwenyekiti wake, makada wa CCM walikuwa wakimuunga mkono na kumpigia chapuo Prof. Lipumba. Ilikuwa ni njia ya 'kulipa kisasi kisiasa' kwakuwa tu Maalim Seif alishirikiana na CHADEMA hata kuwapa Mgombea Mwenza mwaka 2015 (Juma Duni Haji).

Propaganda ya kuwa CUF iliyokuwa ikiitwa ya Maalim kudhibitiwa na kumezwa na CHADEMA iling'ang'aniwa na hata kutangazwa vilivyo. Wakati huo, makada wengi wa CCM mitandaoni ikiwemo humu walikuwa upande wa CUF-ya-Lipumba. Maalim Seif alisemwa kuwa amedhibitiwa, anaendeshwa na kuamuliwa na CHADEMA ya Mbowe.

Hatimaye, jana Maalim Seif amejiunga na ACT-Wazalendo badala ya CHADEMA. Maalim Seif (yawezekana alikuwa akizifuatilia propaganda dhidi yake kwa umakini mkubwa) amefanikiwa kuruka kigingi cha propaganda hizo. Watungaji na wasambazaji wa propaganda hizo wamebaki wakiduwaa na kugosagosa wasijue la kufanya au kusema. Wanaweweseka!

Maalim Seif, kisiasa, anajitosheleza. Historia yake tangu akiwa masomoni inambeba ndani ya chama chochote kiwacho. Hakuna chama chochote cha siasa hapa Tanzania ambacho kinaweza kummeza Maalim Seif na kumfanya kuwa ni mwanasiasa wa 'kawaida' hasa kwenye siasa za Zanzibar. Ndiyo maana kuhama kwake kunafuatwa na kuhama kwa mamia ya wafuasi wake.

Kuhamia kwakeACT-Wazalendo badala ya CHADEMA ni pigo kwa makada wasio makini wa CCM. Ndiyo maana hawaachi kujipa Imani na kujikaza kisabuni kwa kubadili chenga hiyo kama kuikacha CHADEMA. Maalim ni mwanasiasa nguli na mbobezi. Anaweza 'kushaini' popote atakapojiunga. Kama kushirikiana kisiasa, alipo hapatakuwa ni kikwazo kwake.
Kongole kwako mkuu, umeandika waraka maridhawa kabisa.
Maalim Seif ni Taasisi, alipokuwa ndani ya CUF, aliidefine CUF. na sasa amehama na roho ya CUF kwenda ACT. CUF - Lipumba ni mzoga wa CUF, hakuna kitu hapo. inawezekana Lipumba anafurahi kwamba kafaulu kumtoa Maalim. Alivyo mbumbumbu wa kisiasa, huenda anafurahi, kama zuzu.
Kwa vyovyote mabwana zake wa CCM waliomtuma, wamefurahi sana, lakini baada ya kuhamia ACT, wametaharuki.

Hawana hakika kama hiki walichofanya kimewasaidia au kinawaletea matatizo makubwa zaidi.

Kwa upinzani hii ni habari njema. Huu mchanyato mpya wa Zitto-Maalim +CHADEMA utakuwa mziki wa aina yake kwa 2020. Maalim Seif wa ACT atakuwa na mchango mkubwa zaidi bara kuliko Maalim Seif wa CUF. Kumbuka Zitto wa sasa ni yule aliyebatizwa, siyo yule wa enzi za Kikwete. na zile takataka zilizokuwa ACT, akina Kitila, Anna Mughwira na yule katibu mkuu nimesahau jina lake, CCM walitusaidia kuzisafisha. na Magufuli akambatiza Zitto. kwa hiyo sasa ni poa.

Mwaka huu mzuri sana kwa upinzani. juzijuzi tu kuna JIPU moja ambalo wapinzani walikuwa wanajiuliza wanalipasuaje, sasa limehama kama lilivyo likaingia CCM. sasa wao watajua namna ya kulipasua. wapinzani swwaaafiiii! Asante Mungu. Baada ya makasheshe yote, Tundu Lissu kupigwa risasi, kina Mbowe kusota rumande siyo mara moja wala mara mbili bali mara kadhaa, akina Lijualikali kunyanyaswa sana, kina Halima Mdee mara rumande mara kuhojiwa bungeni, hatimaye Mungu anatuelekeza Neema tele! Ashukuriwe Mungu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom