Fahamu kuhusu utofauti wa Meli, Boti, Jahazi, Mashua, Mtumbwi na Ngalawa

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
5,064
12,889
Vyombo vya majini (Watercraft) ni chombo chochote kinachotumika kufanya safari majini kutoka sehemu moja kwenda nyingine.Mfano wa hivyo vyombo ni Meli, Boti, Nyambizi (Submarine) na Sea Planes (Ndege zinazoweza kuelea).

Tuangalie utofauti wa vyombo hivi vya majini ambavyo vinafanya kazi kila siku.

1. Meli
Hiki ni chombo cha majini chenye uwezo mkubwa wa kubeba abiria na mizigo pia inaendeshwa na nguvu ya injini.

Ndani ya meli kunaweza kukawa na boti ya uokoaji au dharura. Hivyo boti ni ndogo kuliko meli.

images (2).jpeg

2. Boti
Hiki ni chombo cha majini ambacho ni kidogo kwa meli ukilinganisha ubebaji wa abiria,mizigo na urefu. Boti unaweza ukaendesha kwa nguvu ya kupiga kasia, upepo au injini.

images (6).jpeg

3. Jahazi
Hii imetengezwa kwa kutumia mbao na huwa na mlingoti ambao hufungwa tanga (shuka) kwa ajili ya kusaidia kutumia upepo wawapo safarini. Jahazi licha ya kutumia upepo baadhi hutumia na injini kuongeza nguvu au kurahisisha wakati wa kupaki. Jahazi hubeba mizigo mikubwa kulingana na ukubwa wake.

Dhow01.JPG

4. Mashua
Mashua ni jamii moja na jahazi tofauti yake ni kuwa mashua huwa ni ndogo,uwezo wake kubeba mizigo ni mdogo na hutumika sana kwenye uvuvi na utalii.Pia mashua hutumika nguvu ya upepo kujiendesha na kasia.

images (3).jpeg

5. Mtumbwi
Hii ni chombo kidogo cha majini ambacho hubeba watu na mzigo kidogo. Hutumia kasia kuendeshwa na huwa haitumii injini.

images (2).jpeg

6. Ngalawa

Hiki ni chombo kidogo cha majini ambacho hutumia mwiko wa kupigia kasia kujiendesha. Na hutumika kwenye uvuvi na utalii uwezo wake ni kubeba watu 1 mpaka 3.Pembeni huwa na sapoti ya mbawa ambazo husaidia kuipa stability.

Vyombo vingine vinavyofanya kazi kwenye maji.

7. Hovercraft
Hivi ni vyombo vyenye uwezo wa kufanya kazi nchi kavu na majini. Hutengenezwa kama cushioned air ambapo huwezesha kuelea kikiwa majini. Mfano ni kama boya ambazo zimejazwa hewa na zina injini nyuma.

Formel1_hovercraft.jpg

II. Personal Watercraft (Jet Ski)
Hii ni kama pikipiki ambazo hutumika kwenye michezo ya majini.

images.jpeg

III. Seaplanes
Hizi ni ndege ndogo ambazo licha ya kupaa angani huwa zimewekewa mfumo wa maboya sehemu ya chini hivyo ikiingia kwenye maji inaelea kama boti.

images (4).jpeg

IV. Submarine (Nyambizi)
Hizi ni meli kubwa ambazo hupita chini ya maji na nyingi hutumika kijeshi au katika utafiti.Huibuka juu ziwapo kwenye eneo la bahari ya nchi nyingine(Territory Water) au bandarini.

images (3).jpeg
 
Vyombo vya majini (Watercraft) ni chombo chochote kinachotumika kufanya safari majini kutoka sehemu moja kwenda nyingine.Mfano wa hivyo vyombo ni Meli, Boti, Nyambizi (Submarine) na Sea Planes (Ndege zinazoweza kuelea).

Tuangalie utofauti wa vyombo hivi vya majini ambavyo vinafanya kazi kila siku.

1. Meli
Hiki ni chombo cha majini chenye uwezo mkubwa wa kubeba abiria na mizigo pia inaendeshwa na nguvu ya injini.

Ndani ya meli kunaweza kukawa na boti ya uokoaji au dharura. Hivyo boti ni ndogo kuliko meli.

View attachment 1508336

2. Boti
Hiki ni chombo cha majini ambacho ni kidogo kwa meli ukilinganisha ubebaji wa abiria,mizigo na urefu. Boti unaweza ukaendesha kwa nguvu ya kupiga kasia, upepo au injini.

View attachment 1508349

3. Jahazi
Hii imetengezwa kwa kutumia mbao na huwa na mlingoti ambao hufungwa tanga (shuka) kwa ajili ya kusaidia kutumia upepo wawapo safarini. Jahazi licha ya kutumia upepo baadhi hutumia na injini kuongeza nguvu au kurahisisha wakati wa kupaki. Jahazi hubeba mizigo mikubwa kulingana na ukubwa wake.

View attachment 1508337

4. Mashua
Mashua ni jamii moja na jahazi tofauti yake ni kuwa mashua huwa ni ndogo,uwezo wake kubeba mizigo ni mdogo na hutumika sana kwenye uvuvi na utalii.Pia mashua hutumika nguvu ya upepo kujiendesha na kasia.

View attachment 1508375

5. Mtumbwi
Hii ni chombo kidogo cha majini ambacho hubeba watu na mzigo kidogo. Hutumia kasia kuendeshwa na huwa haitumii injini.

View attachment 1508368

6. Ngalawa
Hiki ni chombo kidogo cha majini ambacho hutumia mwiko wa kupigia kasia kujiendesha. Na hutumika kwenye uvuvi na utalii uwezo wake ni kubeba watu 1 mpaka 3.Pembeni huwa na sapoti ya mbawa ambazo husaidia kuipa stability.

Vyombo vingine vinavyofanya kazi kwenye maji.

7. Hovercraft
Hivi ni vyombo vyenye uwezo wa kufanya kazi nchi kavu na majini. Hutengenezwa kama cushioned air ambapo huwezesha kuelea kikiwa majini. Mfano ni kama boya ambazo zimejazwa hewa na zina injini nyuma.

View attachment 1508347

II. Personal Watercraft (Jet Ski)
Hii ni kama pikipiki ambazo hutumika kwenye michezo ya majini.

View attachment 1508367

III. Seaplanes
Hizi ni ndege ndogo ambazo licha ya kupaa angani huwa zimewekewa mfumo wa maboya sehemu ya chini hivyo ikiingia kwenye maji inaelea kama boti.

View attachment 1508332

IV. Submarine (Nyambizi)
Hizi ni meli kubwa ambazo hupita chini ya maji na nyingi hutumika kijeshi au katika utafiti.Huibuka juu ziwapo kwenye eneo la bahari ya nchi nyingine(Territory Water) au bandarini.

View attachment 1508329
Je Melikebu ni nini??
 
Tofauti ya ngalawa na mtumbwi haiko clear.Maana vyombe vyote vinatumia makasia ili kuongeza mwendo kasi
 
Back
Top Bottom