Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,500
- 5,537
Kulipa kodi ni sehemu ya uzalendo na ni wajibu wa kila mwananchi.
Kodi unayolipa ndio ambayo hupatia watu huduma na mahitaji mengine ya jamii na miundo mbinu.Usipolipa kodi unakua unajiibia wewe na kuiibia jamii na taifa lako.Hata hivyo kuna wakati hutokea ama kwa kujua au kwa kutokujua mtu analipa kodi pungufu au kuipunja serikali.Linatokea kwa kujua pale ambapo ama unaficha taarifa au unaghushi taarifa za kikodi ili kulipa kodi pungufu.jamo hili ni kosa kisheria na linaweza kuathiri biashara yako kwa namna mbaya ikiwamo kuotzwa faini na hata kufungwa.
Lakini pia kuna wakati inatokea mfanyabiashara anajikuta analipa kodi kupita kiasi yaani unalipa zaidi.
Masuala ya kodi ni tata sana na yanahitaji uelewa mkubwa wa falsafa ya kodi na wajibu na haki zako kama mlipa kodi.Elimu hii yakodi sio elimu rahisi kuelewa na kufuatilia lakini kama mjasiriamali ni muhimu sana ukaelewa masuala ya kodi yanayohusu biashara na huduma yako.Kuelewa masuala au sheria na kanuni hizo hata kama hulipi kodi kunaweza kukuwezesha kutambua wajibu an athari unazoweza kupata katika masuala ya kodi.Tabia ya kukwepa kodi ipo kwa wafanyabiashara wengine na wengine hushirikiana na watumishi wa mamlaka za kodi katika kuficha uhalifu wao.Kuna ina nyingi sana za kodi ambazo zinahusika katika biashara.Kuna kodi zinaitwa kodi za mauzo,kodi za zuio,ushuru na tozo za aina mbalimbali.kodi hizo zinakuwa sehemu ya gharama zako katika biashara.Ni muhimu sana ukaelewa ni kodi zipi zinahusika katika eneo lako la biashara kwani kuna baadhi ya kodi ambazo zinaweza kuhusika katika biashara ya aina fulani lakini zisihusike katika biashara nyingine.
Katika aina zote za kodi unazolipa serikali unapaswa kufahamu kwamba zipo baadhi ya kodi ambazo unaziingiza katika sehemu ya matumizi yako ya kibiashara hasa katika kampuni.Kwa mfano Ushuru wa aina zote na tozo za aina zote ni sehemu ya matumizi ya Kampuni yako.Kwa lugha nyingine unapoweka hesabu za matumizi ya kampuni kwa sababu za kikodi ni lazima ufikiri gharama za hizo tozo za ziada.Hata hivyo ni muhimu ukapata ushauri wa mtaalamu wa masuala ya kodi hasa iwapo gharama hizo zitaathiri kiwango cha kodi unachopaswa kulipa kwa zaidi ya asilimia 80%.
Vile vile kuna kodi ambazo zinaitwa kodi za zuio ambazo mara nyingi kampuni yako inakuwa tu kama wakala wa kulipa kodi kwa niaba ya mteja/mtoa huduma wako.Kodi hizi sio sehemu ya matumizi ya kampuni yako na zinapaswa kuwasilishwa serikali kila mwezi.Hata hivyo ipo kodi ya zuio ambayo ni maalum inayotozwa katika mauzo ambayo ina kodi ya ongezeko la thamani.Kodi hii ni tofauti na kodi nyingi kwa sababu ni kodi ambayo inatozwa kwa mlaji wa mwisho na wewe kama mmiliki wa kampuni sio mlaji wa mwisho,Unaposajiliwa kama mlipaji w kodi hii unakuwa unastahili kurejeshewa kodi ambayo wewe utalipa kwa wengine ambao wamesajiliwa kwa kodi hio.Inapotokea kiwango cha kodi ulichotozwa ni kikubwa kuliko ulichotoza basi unapaswa kufanyiwa Refund na ikiwa pungufu basi wewe utalipa.Hata hivyo zipo sheria za kodi ambazo zinaweka masharti ya namna namazingira ya kodi hii na u napaswa kuielewa pia vizuri hasa katika sekta ya uchumi uliyopo.
Unaofanya biashara yoyte jitahidi sana uelewe kwamba kila suala la kodi linalohusu biashara yako.Ni muhimu pia ukawa na mfumo wa kutunza kumbukumbu zako za kikodi. ili kunapotokea sintofhamu ya aina yoyote basi unakuwa na rekodi sahihi.
Mamlaka zao kodi kama zilivo mamlaka nyingine za kiserikali zina tatizo la RUSHWA.Vinara wengi wa rushwa hutumia ukosefu wa maarifa wa wafanyabiashara wadogo ama kuwaibia kwa njia ya RUSHWA na wakati mwingine kuwaingize katika kuvunja sheria za kikodi kwa makusudi.Kwa mfano.Afisa wa TRA anapokuwa kazini na kukushawishi kwamba badala ya kulipa kodi yako halali ya Shiling 10000 ulipe 5000 na yeye umpe 2000 basi jua utakuwa umelipa shiling 12000 ya kodi kwa hata afisa wa kodi hayuko juu ya sheria za kodi na kama sheria ya kodi inasema ulipe 10,000 utalipa 10000 kama sio leo ni kesho ila utailipa.
Washauri wa kodi na wahasibu ni watu muhimu sana katika masuala ya kodi.Hata hivyo ni muhimu sana uelewe masuala ya kodi ili uweze kutumia vizuri huduma zao kwani kuna wakati wanakuwa na tamaa na kutaka kuipitisha ile kodi inayoenda serikalini kwa kukuonesha njia haramu za kukwepa kodi.Hata hivyo wengi hutumia hofu yako na uelewa wako mdogo kukuonesha kwamba uko katika matatizo ili kukufanya ufuate miongozo yao.Ndio maana mara zote huwa nawashauri wote kwamba USIOGOPE KUTAFUTA MAARIFA KWANI MAARIFA HUKUONGEZEA KUJIAMINI..
Eneo lingine unalopaswa kujizatiti ni kutunza kumbukumbu zako za kodi.Kama unayo mashine ya EFD itumie vizuri.Siku hizi TRA wameruhusu watu kujikadiria kodi peke yako tumia fursa hio.Tunza rekodi za mapato yako,tunza rekodi za matumizi yako.Jilipe Mshahara.Kokotoa faida za kampuni yako kila mwaka ila ujue faida yako.Usiogope kuta ngaza hasara,usiogope kuchukua mikopo,usiogope kuwa na madeni kwani yote hayo unaweza kuyatumia katika taarifa yako ya fedha kuhakikisha kwamba masuala yako ya kodi yanakaa sawa.
Jitahidi sana matumizi yako ya kampuni yawe zaidi katika ASSETS na OPERATIONS.Matumizi yako binafsi tafuta namna ya kuyashield ili yawe na nafuu ya kodi.Hasa yale matumizi ambayo ni makubwa..
Nimechokoza mada karibu tujadili zaidi kuhusu uelewa wetu wa masuala ya kodi na namna bora ya kusimamia masuala yetu ya kodi.