Mwaliko kwa Wadau kushiriki katika Shughuli za Kamati ya Maboresho ya Sera za Kodi (Task Force on Tax Reforms)

Nkerejiwa

Senior Member
Feb 25, 2014
146
214
Serikali kupitia wizara ya Fedha inaomba maoni yako kuhusu vile unatamani sheria za kodi kwa mwaka ujao wa fedha ziwe.

Kipi kiongezwe, kipi kiondolewe kodi, kipi kipewe unafuu wa kikodi etc. Toa maoni yako sasa. https://maoni.mof.go.tz/
IMG_4944.jpg
 
Sawa

Ushauri wangu ni mmoja tu

Kitengenezwe Kikokotoo cha Wafanyabiashara binafsi ( individuals) kitakachowawezesha kutambua Kodi wanayopaswa kulipa bila Hata kutumia Wahasibu/ tax consultants

Kama ambavyo Mfanyakazi anajua PAYE yake vile vile Wafanyabiashara wanaweza kujua kodi zao endapo watatengenezewa Mfumo au Software za Kujaza Taarifa zao wao wenyewe badala ya kujaziwa na Tax officers through Tax Returns

Kimsingi bado Kodi Halali anayopaswa kulipa mfanyabiashara wa Kawaida ni Fair ila kwa sababu hawajui inafikiwaje Ndio sababu wengine wanakwepa

Nitoe rai kwa Vijana Wetu waliobobea mwenye Sayansi ya software ambapo mtu ataandaa Taarifa zake za Biashara za kila siku na mwisho wa mwezi imtolee Kodi stahiki anayoicarry forward kuelekea mwisho wa mwaka.au malipo ya instalments

Mungu wa Mbinguni awabariki Sana
 
Ondoeni utitiri wa kodi kwenye mafuta, umeme,
Ina sikitisha, kodi zilizoko kwenye hizo budhaa.
Kama vipi, EWURA uunganishwe na REA, Pia LATRA iunganishwe na TANROADS. Na serikali ibebe jukumu la kuendesha hizo taasisi na sio kuchangiwa na wananchi
 
Serikali kupitia wizara ya Fedha inaomba maoni yako kuhusu vile unatamani sheria za kodi kwa mwaka ujao wa fedha ziwe.

Kipi kiongezwe, kipi kiondolewe kodi, kipi kipewe unafuu wa kikodi etc. Toa maoni yako sasa. View attachment 2895966
Naomba kuuliza swali lililo nnje ya mada.
Wewe ni Mwigulu, PS wake, ama msaidizi wake wa karibu au ni chawa tuu!!??

Akhsante sana.
 
Washushe Kodi Hadi 10% hakuna atakayekwepa Kodi. Na kama mfanyabiashara hajasajiliwa akatwe 10% kwenye mapato yake. Watoa huduma wote wakatwe withholding tax ya 5%
 
Serikali itosheke na VAT inayokusanya, tozo za miamala zimeishia kudumaza sekta husika. Uchumi wa nchi sio panya wa maabara wa kumfanyia majaribia na vitu vya kijinga.
 
Back
Top Bottom