Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,359
- 2,780
Najua watu wengi hawajui kama Tanzania Kuna Kiwanda cha kutengeneza simu janja (smartphone) โ umeshtuka sio โ๏ธ.
Nchini Tanzania mkoa wa pwani wilaya ya mkuranga kama siku utafanikiwa kutembea basi Kuna Kiwanda kinaitwa Raddy Fiber Manufacturing na Raddy Electronics ambapo kwa ndani utakutana na Kiwanda cha Raddy electronics ndo kinajihusisha na kutengeneza simu janja.
Ni simu za smartphone ambapo utaweza kukuta zinatengenezwa na Kiwanda hicho kliwahi kutembelewa na Waziri wa mawasiliano na Teknolojia ya Habari nchini Jerry William Silaa.
Kiwanda hicho kinatarajia kutoa ajira zaidi ya 5000 ambapo mkurugenzi mkuu wa Kiwanda hicho ni Mtanzania anaitwa Ramadhan Mlazi.