Fahamu kuhusu Kilimo cha Strawberries

Fahamu kuhusu Kilimo cha Strawberries

Mikoa inayositawisha vizuri strawberry ni Iringa na Morogoro,lakini unaweza kufanya utafit hata hapo ulipo,maana inastawi vizuri kwenye maeneo ya mwinuko,1500m
Soko kubwa sana lipo Kenya,lakini hata hapa Tanzania bado strawberry inalipa,ni miezi 2 tu tangu uanze kuandaa utakuwa umeanza kuvuna,siwadanganyi,unaweza kujifunza zaidi kuihusu

Mkuu unafanya au unazungumza kwa story za mtaani?


Niko Arusha na Nalima Strawberry kusema kuwa kwa mwez mmoja unakuwa unavuna si kweli zao hili linahitaji mtu mvumilivu na wa kulijulia hasa kwenye matunzo yake...


Ziko aina nyingi za zao hili lakin kwa hapa kwetu ambalo linafanya vizuri ni Chandler...
 
strawberry zinaliwa?

IMG_4508.JPG
 
Bei ya strawberry inategemea na soko,ila bei ya kufikia kwa soko la dar na arusha,kilo ni elf 30-50

Hii 30-50 ni pesa ya Zimbabwe au Tanzania?



Kama ni Tanzania sijawah kuuza zaid ya 20,000/=
 
Kuna maeneo kule kwetu haya matunda yanaota msituni na hayana mwenyewe. Yuko mchungaji mmoja pale Uwanji Makete alikuwa akiotesha bustanini kwake. Ngoja nitafute simu yake nimuulize kama angali na ile bustani.
Umeniwahi tu mkuu, mi mwenyewe nilitaka niseme hivyo kwamba haya matunda kwa kule kwetu tunayaona kama matunda pori. Tena kwa kule kwetu yapo kama rangi kama tatu hivi. Mimi mwenyewe kwa kuwa ni matunda niyapendayo nilikuwa nawaza kwenda kuyaotesha kwa majaribio.
 
Umeniwahi tu mkuu, mi mwenyewe nilitaka niseme hivyo kwamba haya matunda kwa kule kwetu tunayaona kama matunda pori. Tena kwa kule kwetu yapo kama rangi kama tatu hivi. Mimi mwenyewe kwa kuwa ni matunda niyapendayo nilikuwa nawaza kwenda kuyaotesha kwa majaribio.
Nimekula sana haya matunda iringa kule yanajiotea tuuu
 
Back
Top Bottom