Fahamu Kuhusu Biashara ya Clearing and Forwarding Agent

Fahamu Kuhusu Biashara ya Clearing and Forwarding Agent

Ruaha Freight Ltd ni kampuni iliyo na leseni ya TRA, kutoa mizigo bandarini, viwanja vya ndege na mipakani (borders), yaani freight clearing and forwarding. Karibuni mtuletee kazi za kugomboa (clearing) mizigo ( magari, containers & loose cargo) tunazifanya kwa ufanisi, uaminifu mkubwa na kwa bei nafuu.


Ada zetu za uwakala ( agency fee) ni kama ifuatavyo;
1. Tunagomboa gari kwa tshs.200,000 tu.
2. Container la futi 20 kwa tshs. 250,000 na futi 40 kwa shs.300,000 tu.
3. Loose cargo ni tshs.100,000 mpaka tshs.300,000 inategemea na ujazo (Cubic Measurement)
4. Airport cargo tsh. 100,000 mpaka tsh. 250,000, nategemea uzito na thamani ya mzigo.
Wasiliana nasi kwa anuani ifuatayo;



Ruaha Freight Ltd,

Derm Plaza 11th Floor, Bagamoyo Road,

Makumbusho, Kijtonyama,

P.O.Box 62442,
Dar es Salaam- Tanzania.
Email: ruahafreight2017@gmail.com
Tel: +255222128447

Mob: +255718 866 651 (call or whatsapp).
 
Kuna mwamba namjua ametoboa kwa kupitia biashara hiyo hiyo now yupo njema vibaya sana

Uzuri anatokea familia yenye hela, baba yake alimpatia mkopo wa million 60 mwamba alifanikiwa kurudisha hela za mzee ndani ya miaka minne

Sa iv ana mawe hatari.

Na alifungua kampuni yake back in 2008 now kampuni kubwa na ina jina kwenye hiyo sekta.
Kwa mtu aliyeanza 2008 lazma awe na hela sahizi. Fursa ilikuwa wazi kabla kina GSM na HSC kuingilia mfumo. Sasa imagine 80% ya wafanyabiashara wanao import mizigo wanatolea GSM na jamaa walipambana sana ku kill competition toka walivyoingia.

Kampuni ambazo zime sustain kwenye game ni zile kongwe na zilizo base kwenye Exportation kuliko imports. Nyingine zilishaanguka.

Alipokuja Magu 2015 ndio kabisa biashara zikayumba na alipoanzisha TASAC ndio kaenda kutibua mipango.
 
Kwa mtu aliyeanza 2008 lazma awe na hela sahizi. Fursa ilikuwa wazi kabla kina GSM na HSC kuingilia mfumo. Sasa imagine 80% ya wafanyabiashara wanao import mizigo wanatolea GSM na jamaa walipambana sana ku kill competition toka walivyoingia.

Kampuni ambazo zime sustain kwenye game ni zile kongwe na zilizo base kwenye Exportation kuliko imports. Nyingine zilishaanguka.

Alipokuja Magu 2015 ndio kabisa biashara zikayumba na alipoanzisha TASAC ndio kaenda kutibua mipango.
Dah! Si mchezo ila jamaa niche yake ilikuwa ni magari kwa sana sijajua kama ameathirika sana
 
Dah! Si mchezo ila jamaa niche yake ilikuwa ni magari kwa sana sijajua kama ameathirika sana
Kwa magari sio mbaya maana wabongo wengi wanapenda magari. Ila ukiifanya kama dalali ndio unapata hela. Unawaagizia watu na kufanya clearance
 
Kama unaweza hata kuwa na Shipping address nje ya nchi itakuwa rahisi zaidi kama ambavyo makampuni mengine yanafanya
Boss

Naomba kufahamu zaidi hapa, je ninaweza kuwa na shipping address nje hata kama sipo huko physically?

Ningependa tujadili zaidi. Asante
 
Habari za wakti huu;

Leo nimeona nilete mjadala kidogo kuhusu Biashara ya Clearing and Forwaring Agency.Kabla ya kuingia kwenye mjadala niweke wazi kwamba mm sifanyi shughuli za C&F.Hivyo basi maoni na mtazamo wangu upo zaidi kibiashara na kiujumla na ninaamni kwamba wengine watajifunza na wale ambao wako kwenye industry wataongezea yale ambayo yanakosekana.

Biashara ya C& F ni bishara ambayo ina uhusiano na TRA ambako pia hujulikana kama mawakala wa Forodha.Lakini pia inahusisha ufanyaji kazi kwa karibu na Shipping Agencies,na kampuni za usafirishaji mizigo pamoja na waendesha Custom bonded warehouses na inland containers depots.Hivyo basi ili kazi yako ya C&F iwe vizuri ni lazima uwe na uelewa wa shughuli za hizo zilizotaja.

Kibali cha kufanya shughuli za wakala wa Forodha hutolewa na Mamlaka ya Mapato TRA kwa kuzingatia masharti ni vigezo mbalimbali ikiwemo kuwa na utaalamu wa masual ya Forodha ambapo Mafunzo yake yanapatikana katika chuo cha USIMAMIZI wa KODI cha TRA.Ni kozi ya Muda Mfupi(Less than a year).Lakini pia kuna masharti mengine ambayo unaweza kuyapata kwa kuwasiliana na ofisi ya TRA iliyo karibu na wewe,ikiwamo Bond Guarantee etc.

Je unapataje Pesa Katik Biashara hii?
Katika biashara hii wewe unakuwa na kazi moja kubwa ambayo ni kuhakikisha mzigo wa mteja wako unavuka katika Mpaka wa forodha mpaka kukufikia na kuhakikisha kwamba masuala yote ya kodi na malipo mengine yote yanafanyika kikamilifu.Katika kutoa huduma hii utatoza Ada maalum kwa mteja wako kulingana na aina ya huduma na thamani ya mzigo. Hivyo basi kadiri unavoweza kutoa huduma bora na unapokuwa na uelewa wa taratibu na kanuni mbalimbali ndivyo inavykuwa rahisi kwa wewe kutoa huduma bora zaidi na kutengeneza faida zaidi.

Unawezaje kufanikiwa katika Biashara hii?
Kufanikiwa katika biashara hii kunahitaji ubunifu wa hali ya Juu.Kwanza unahitaji kujenga mahusiano mazuri na kampuni za usafirishaji,Kampuni zinazoagiza mizigo kwa kiawango kikubwa(Cargo Consolidators na pia kujenga mtandao mzuri wa masoko na Biashara.

Unahitaji pia kufahamu aina ya biadhaa ambazo wateja huagiza mara kwa mara na nmna bora ya kuwawezesha kupata mzigo yao kwa haraka na kwa gharama nafuu

Je Biashara hii unaweza kuanza kwa mtaji kiasi gani?
Kwa kutegemea eneo ulipo na soko ulilolenga gharama za kuanzisha Biashara hii zinaweza kuhusisha gharama ya Pango,Computers,Leseni na Vibali,Bond Guarantee costs kwa ajili ya TRA,Gharama za Mafunzo kama huna Mafunzo yanayohusu hilo eneo pamoja na gharama za matangazo na Masoko.

Je ni Maboresho gani naweza kufanya katika Biashara hii?
Katika bisahra hii unaweza kujiongeza kwa kuongeza huduma za dropshiping and product sourcing kwa biadhaa zinazotoka nje ya nchi.Mfano unaweza wasaidia watu kuagizi bidhaa kutoka UCHINA,Japan,Uturuki,Uingereza na kwingine na kwa kutumia mtandao wako na uzoefu ukawawezesha kuagiz mzigo kwa kuwasiliana na wewe moja kwa moja badili ya kuwasiliana na watu tofauti tofauti.Kama unaweza hata kuwa na Shipping address nje ya nchi itakuwa rahisi zaidi kama ambavyo makampuni mengine yanafanya.Cha muhim ni kujaribu kufanya namna ili uwe na bidhaa fulani ambayo unaweza kuiagiza na kuipromote kwa uhakika huku ukifahamu gharama zake mpaka ifike kwa mnunuzi wa Mwisho


Karibuni tujadili zaidi kuhusu Biashara hii ya Clearing nd Forwarding Agent na kwa wale ambao wana utaalamu na biashara hii wanaweza kuja kuleta maboresho na kuboresha mjadala kwa maslahi ya wengine.

Kwa mawasiliano zaidi na huduma za ushauri wa biashara tafadhali wasiliana nasi kwa email:masokotz@yahoo.com au PM

Karibuni kwa mjadala
Bond around mil 40
 
Back
Top Bottom