Fahamu kiwango cha fedha ambacho ukisafiri nacho lazima utoe taarifa TRA

Mamlaka wa Mapato Tanzania (TRA) ambayo ndiyo yenye dhamana ya kusimamia masuala mbalimbali yahusuyo fedha imetangaza kuwa, kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu, mtu yeyote akisafirisha fedha taslimu dola za kimarekani 10,000 ambazo ni sawa Tsh 22.5 milioni ni lazima awe amejaza fomu yenye maelezo kuhusu fedha hizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, George I. Mnyitafu imeeleza kuwa TRA imepata mamlaka hayo kutokana na Sheria ya Kudhibiti Fedha Haramu, Sura 423 na Kanuni yake inayohusu utoaji wa taarifa ya kiasi cha fedha taslimu na Hati za Malipo zinazosafirishwa kuingia au kutoka nchini.

Sheria hiyo imeipa Mamlaka ya Mapato Tanzania mamlaka ya kusimamia utoaji wa taarifa kuhusu fedha zinazosafirishwa kuingia au kutoka nchini.

Taarifa hiyo ya TRA inahusu usafirishaji wa fedha taslimu au hati za malipo (Bearer Negotiable Instruments) zinazofikia au kuzidi dola za kimarekani 10,000 (elfu kumi) au fedha nyingine yoyote yenye thamani sawa na hiyo iwapo fedha au hati hizo zitasafirishwa kwa njia
zifuatazo;

(a) mtu yeyote anayesafiri akiwa nazo au katika mizigo anayoambatana nayo au katika chombo cha usafiri;
(b) katika makontena ya kubebea mizigo, na
(c) kwa njia ya vifurushi.

TRA imeutaarifu umma kuwa, kuanzia tarehe 01 Oktoba 2017, msafirishaji yeyote wa fedha taslimu au hati za malipo zinazofikia kiwango kilichotajwa na kanuni hizi atalazimika kutoa taarifa kwa kujaza fomu zitakazopatikana kwa maafisa forodha mipakani.

Mamlaka hiyo imesisitiza kuwa, kutotoa taarifa au kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu usafirishaji huo fedha au hati za malipo ni kosa kisheria.

Kuwatoa hofu wananchi kuhusu sheria hii, TRA imeeleza kwamba, utaratibu huu haukusudii kuzuia usafirishaji wa fedha taslimu na hati
za malipo kuingia au kutoka nchini.

Kwa taarifa au ufafanuzi zaidi tafadhali wasiliana na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa namba za simu za bure: 0800 750075 au 0800 780078, au Barua pepe: huduma@tra.go.tz
Hiki nikichaka kingine cha kutengeneza waporaji kwa bongo.
 
Nani kakueleza hili? Ukiingia na zaidi ndiyo ya hizo ndiyo unatakiwa kudeclare kwamba ninaingia na fedha za kiasi ya dola elfu kumi au zaidi au hundi hii wame copy na kupaste.
Uzuri wa Wamarekani karibu kila kitu chao kiko online. Mpaka form ya kujaza ipo online hii hapa PDF

Form inaeleza wazi ni kwa mtu anayetaka kuingia au kutoka Marekani.

https://www.fincen.gov/sites/default/files/shared/fin105_cmir.pdf

Habari yenyewe hii hapa Currency and Monetary Instruments - Amount that can be brought into or leave the U.S.
 
Bakini hapo hapo. Tanzania maendeleo mtayasikia tu
Kwanza tumechelewa Marekani ndio maisha yao. Sijawahi ishi nje ya Tanzania hata kwa saa ishirini na nne tu lakini nimepata masimulizi kutoka kwa Watanzania wanaoishi huko.Flaviana Matata aliwahi kusimulia kupatwa na mkasa wa kukutwa akisafiri akiwa na dollar kadhaa ambazo ni ndogo kuliko walizotaja TRA, zilizuiwa na kutakiwa kujaza fomu ya kuzidai.
Fuatilia mahojiano yake kama sikosei katika kipindi cha mkasi EATV vipo yu tobe
 
Hili si geni katika mataifa yaliyoendelea yanayosimamia uchumi wao vizuri. Kuna kipindi nilikuwa naenda taifa la Mashariki ya mbali Korea Kusini kwa flight ya kampuni ya ndege ya Qatar Airways ambapo kampuni ilituandalia utaratibu Wa kulala Doha, Qatar maana ndege iliondoka Dar saa 11 jioni na kufika Doha saa 4 usiku ndege ya kuunganisha kwenda ilikuwa ni siku iliyofuata Saa mbili asubuhi. Kwa hiyo Qatar Airway walituandalia in transit visa pamoja booking ya hotel. Nilikuwa na pesa za kutosha zaidi ya sola 20,000 wakati kucheki out Ahamad Into Airport sikupata shida. Kimbembe kilikuja wakati wa kucheck in kwa ajili yakuondoka airport. Maana jamaa walitaka nyaraka ya kuonyesha hizo fedha nimeingia nazo kumbe kwa haraka haraka wakati najaza fomu za uhamiaji Pale Doha sikujaza fomu inayoonyesha nimeingia na fedha kiasi gani na natarajia kutumia kiasi gani.
Kwa hiyo wao waliamini kuwa hizo pesa nimeingia bila kuwa nazo ila ninatoka nazo. Kwa kutaka kunisaidia wakaniomba kama kuna nyaraka toka JNIA -Dar ambayo inayoonyesha kuwa nimetoka na pesa hizo Dar. Ukweli jamaa walinishikilia zaidi ya SAA wakaniruhusu yaani bado kama nusu SAA tu ndege iruke mana jina langu lilikuwa likiitwa kwenye vipaza. Jamaa walikomaa sana maana walitaka washikilia kiasi kinachozidi USD 10,000. Nami nilikuwa radhi niachwe na ndege kuliko kuacha pesa zangu. Alikuja jamaa moja nadhani alikuwa na madaraka makubwa pale akawa ananihoji maswali mengi japo alikuwa anatumia mkalimani maana alikuwa hajui kingereza. Moja ya maswali walioniuliza ni kwamba kuna mtu ninayefahamiana naye halo Doha. Je nilifikia hotel gani? Mbali na hotelini nilipopumzika je nilikwenda maeneo gani? Je una uhakika hakuna aliyekuja kukutembelea hapo hotelini? Na maswali mengine mengi. Yaani wale watu walipiga simu mpaka kwenye hotel niliyofikia.
Tokea siku hiyo huwa nikiwa nasafiri kama nikiwa na kiasi kikubwa cha pesa lazima niwasumbue pale JNIA wanipatie form zile form zipo ila Mara nimewahi kuzikosa hata ninapozikosa huwa nawashikizi waniandikie hata Declaration tu kisha wanigongee mhuri.
 
Uzuri wa Wamarekani karibu kila kitu chao kiko online. Mpaka form ya kujaza ipo online hii hapa PDF

Form inaeleza wazi ni kwa mtu anayetaka kuingia au kutoka Marekani.

https://www.fincen.gov/sites/default/files/shared/fin105_cmir.pdf

Habari yenyewe hii hapa Currency and Monetary Instruments - Amount that can be brought into or leave the U.S.
Nisikilize wakati unaondoka unaweza sema tu nina kiasi fulani cha pesa na sehemu nyingi za kuondokea hizo form hazipo,wakati wa kuingia zimetapaka kila kwenye point of entry na ni lazima ujaze kwasababu usipojaza wakikuelekeza uende kwenye red line na huja declare utaishia ndani kwani ni kosa. Nimeelewa kwamba unatakiwa kujaza pia unapotoka.
 
Unaji contradict.

Marekani ni nchi ya sheria zilizo clear,angalau kuhusu hili, ama unatakiwa ku declare unapotoka zikizidi kiasi fulani, ama hutakiwi.

Swali letuni, unatakiwa au hutakiwi?

Hii habari ya "wakati unaondoka unaweza sema tu nina kiasi fulani cha pesa na sehemu nyingi za kuondokea hizo form hazipo,wakati wa kuingia zimetapaka kila kwenye point of entry" haiongelei sheria ya nchi inasemaje.

Halafu "nina kiasi fulani cha pesa" kiasi gani? Inawezekana unasema na unaachiwa kwa sababu una chini ya $10,000. Na ukiwa na zaidi ya $10,000 ni lazima ujaze form.

Utasemaje point ya form hazipo kwa sababu huzioni wakati mimi nime google hapa nimekuwekea link ambayo mtu yeyote popote duniani akiwa na computer na printer ana print?

Unasema formhazipokwa sababu huzionikwenye counter wakati watu wanatafuta kufanya kazi kwenye paperless office?

Hapa tunaongelea sheria ya nchi inasemaje. Ukitakakusafiri kwenda nje ya Marekani na zaidi ya $10,000, kisheria unatakiwa au hutakiwi ku declare hizo hela?

Ukianza kuongelea habari ya uzoefu binafsi, inawezekana mtu wa Customs akakuachia upitishe cocaine,hilo halimaanishi sheria za nchi zinaruhusu hilo.
 
Lengo zuri kwa inchi ila kwa wahujumu uchumi ni pigo kwao.

Tatizo hao wafanyakazi tra na mabenk ndiyo wanatuhumiwa kushirikana na majambazi kwenye kutoa taarifa za siri za wateja wao,
Pia kiasi hicho ni kidogo sana imagine nataka kununua gari 30 mil. Je itakuwaje ?
 
Fahamu kiwango cha fedha ambacho ukisafiri nacho lazima utoe taarifa TRA
Mamlaka wa Mapato Tanzania (TRA) ambayo ndiyo yenye dhamana ya kusimamia masuala mbalimbali yahusuyo fedha imetangaza kuwa, kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu, mtu yeyote akisafirisha fedha taslimu dola za kimarekani 10,000 ambazo ni sawa Tsh 22.5 milioni ni lazima awe amejaza fomu yenye maelezo kuhusu fedha hizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, George I. Mnyitafu imeeleza kuwa TRA imepata mamlaka hayo kutokana na Sheria ya Kudhibiti Fedha Haramu, Sura 423 na Kanuni yake inayohusu utoaji wa taarifa ya kiasi cha fedha taslimu na Hati za Malipo zinazosafirishwa kuingia au kutoka nchini.

Sheria hiyo imeipa Mamlaka ya Mapato Tanzania mamlaka ya kusimamia utoaji wa taarifa kuhusu fedha zinazosafirishwa kuingia au kutoka nchini.

Taarifa hiyo ya TRA inahusu usafirishaji wa fedha taslimu au hati za malipo (Bearer Negotiable Instruments) zinazofikia au kuzidi dola za kimarekani 10,000 (elfu kumi) au fedha nyingine yoyote yenye thamani sawa na hiyo iwapo fedha au hati hizo zitasafirishwa kwa njia
zifuatazo;

(a) mtu yeyote anayesafiri akiwa nazo au katika mizigo anayoambatana nayo au katika chombo cha usafiri;
(b) katika makontena ya kubebea mizigo, na
(c) kwa njia ya vifurushi.

TRA imeutaarifu umma kuwa, kuanzia tarehe 01 Oktoba 2017, msafirishaji yeyote wa fedha taslimu au hati za malipo zinazofikia kiwango kilichotajwa na kanuni hizi atalazimika kutoa taarifa kwa kujaza fomu zitakazopatikana kwa maafisa forodha mipakani.

Mamlaka hiyo imesisitiza kuwa, kutotoa taarifa au kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu usafirishaji huo fedha au hati za malipo ni kosa kisheria.

Kuwatoa hofu wananchi kuhusu sheria hii, TRA imeeleza kwamba, utaratibu huu haukusudii kuzuia usafirishaji wa fedha taslimu na hati
za malipo kuingia au kutoka nchini.

Kwa taarifa au ufafanuzi zaidi tafadhali wasiliana na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa namba za simu za bure: 0800 750075 au 0800 780078, au Barua pepe: huduma@tra.go.tz
Kazi VP ndugu John ,lini tena mnatangaza ??
[emoji53] [emoji53] [emoji53]
 
Kibaya zaidi unaweza ukazitolea maelezo na bado wasiridhike nayo na hili waridhike nayo itakubidi uwape rushwa.

Hili ni gap lingine kwa wapigaji waliojificha kwenye hizo taasisi
 
na
Unaji contradict.

Marekani ni nchi ya sheria zilizo clear,angalau kuhusu hili, ama unatakiwa ku declare unapotoka zikizidi kiasi fulani, ama hutakiwi.

Swali letuni, unatakiwa au hutakiwi?

Hii habari ya "wakati unaondoka unaweza sema tu nina kiasi fulani cha pesa na sehemu nyingi za kuondokea hizo form hazipo,wakati wa kuingia zimetapaka kila kwenye point of entry" haiongelei sheria ya nchi inasemaje.

Halafu "nina kiasi fulani cha pesa" kiasi gani? Inawezekana unasema na unaachiwa kwa sababu una chini ya $10,000. Na ukiwa na zaidi ya $10,000 ni lazima ujaze form.

Utasemaje point ya form hazipo kwa sababu huzioni wakati mimi nime google hapa nimekuwekea link ambayo mtu yeyote popote duniani akiwa na computer na printer ana print?

Unasema formhazipokwa sababu huzionikwenye counter wakati watu wanatafuta kufanya kazi kwenye paperless office?

Hapa tunaongelea sheria ya nchi inasemaje. Ukitakakusafiri kwenda nje ya Marekani na zaidi ya $10,000, kisheria unatakiwa au hutakiwi ku declare hizo hela?

Ukianza kuongelea habari ya uzoefu binafsi, inawezekana mtu wa Customs akakuachia upitishe cocaine,hilo halimaanishi sheria za nchi zinaruhusu hilo.
Naona unatafuta ligi endelea. Nimekuambia umeeleweka,Nimetoka na Fedha mara kibao zaidi ya hiyo elfu kumi na nimedeclare kwa kutamka tu na zimepita mpaka kwenye mashine na zimeonekana na sijapata tatizo wala nini na nikaingia nazo hadi Bongo.Unapoingia ndiyo kipembembe.Nimeshaona mwanafamilia amefungwa miezi 18 tena yeye aliingia nayo toka Bongo na ilikuwa ni fedha ya kulipia ada na hakudeclare na wakampa mvua.Na nakueleza bongo wamekopi na italeta usumbufu na haitakuwa salama. Wasiojulikana wataongezeka.
 
Jamaa Wa mipakani wakijua una na fedha lazima wakuchongeshee mchezo upore, hili serikali wamelifikiria kweli
Tatizo wewe ni NGUMBARU na hutaki kujifunza. Huu ni utaratibu wa kawaida duniani. Tanzania tumechelewa sana kuuanzisha
 
Uzuri wenzetu hata ukiwa na kiasi gani hakuna longolongo
Baada ya declaration unaendelea na safari yako,sijui umezipataje suala hilo hakuna
 
Nimekuelewa. Hapa itakuwa dili. Wazee wa point of entry JNIA hawachelewi kukupiga picha kisha watume kwa whatsapp kwa majambazi wa bodaboda, wakutight kwenye foleni TAZARA. Waje wakupore mchana kweupe
 
Yeah..na hili ndio tatizo kubwa..kuuzana kupo,inahitaji umakini sana hasa Kwa nchi zetu hizi..
 
Kuna watu kutungwa kwa mimba zao hizikutakiwa kukua kabla hazijaharibika lakini naona hilo Mungu aliliachia ili tumkumbuke kupitia matatizo watakayotusababishia watu hao na kujifunza.
 
Back
Top Bottom