Fahamu kiwango cha fedha ambacho ukisafiri nacho lazima utoe taarifa TRA

Fahamu kiwango cha fedha ambacho ukisafiri nacho lazima utoe taarifa TRA

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,009
Reaction score
61,260
Fahamu kiwango cha fedha ambacho ukisafiri nacho lazima utoe taarifa TRA
Mamlaka wa Mapato Tanzania (TRA) ambayo ndiyo yenye dhamana ya kusimamia masuala mbalimbali yahusuyo fedha imetangaza kuwa, kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu, mtu yeyote akisafirisha fedha taslimu dola za kimarekani 10,000 ambazo ni sawa Tsh 22.5 milioni ni lazima awe amejaza fomu yenye maelezo kuhusu fedha hizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, George I. Mnyitafu imeeleza kuwa TRA imepata mamlaka hayo kutokana na Sheria ya Kudhibiti Fedha Haramu, Sura 423 na Kanuni yake inayohusu utoaji wa taarifa ya kiasi cha fedha taslimu na Hati za Malipo zinazosafirishwa kuingia au kutoka nchini.

Sheria hiyo imeipa Mamlaka ya Mapato Tanzania mamlaka ya kusimamia utoaji wa taarifa kuhusu fedha zinazosafirishwa kuingia au kutoka nchini.

Taarifa hiyo ya TRA inahusu usafirishaji wa fedha taslimu au hati za malipo (Bearer Negotiable Instruments) zinazofikia au kuzidi dola za kimarekani 10,000 (elfu kumi) au fedha nyingine yoyote yenye thamani sawa na hiyo iwapo fedha au hati hizo zitasafirishwa kwa njia
zifuatazo;

(a) mtu yeyote anayesafiri akiwa nazo au katika mizigo anayoambatana nayo au katika chombo cha usafiri;
(b) katika makontena ya kubebea mizigo, na
(c) kwa njia ya vifurushi.

TRA imeutaarifu umma kuwa, kuanzia tarehe 01 Oktoba 2017, msafirishaji yeyote wa fedha taslimu au hati za malipo zinazofikia kiwango kilichotajwa na kanuni hizi atalazimika kutoa taarifa kwa kujaza fomu zitakazopatikana kwa maafisa forodha mipakani.

Mamlaka hiyo imesisitiza kuwa, kutotoa taarifa au kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu usafirishaji huo fedha au hati za malipo ni kosa kisheria.

Kuwatoa hofu wananchi kuhusu sheria hii, TRA imeeleza kwamba, utaratibu huu haukusudii kuzuia usafirishaji wa fedha taslimu na hati
za malipo kuingia au kutoka nchini.

Kwa taarifa au ufafanuzi zaidi tafadhali wasiliana na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa namba za simu za bure: 0800 750075 au 0800 780078, au Barua pepe: huduma@tra.go.tz
 
Pesa kidogo sana hizo alafu utoe taarifa TRA?upuuzi kabsa!
Ni kawaida sana.

Marekani ni nchi tajiri sana, lakini hutakiwi kutoka Marekani na fedha zaidi ya USD 10,000 bila kutoa taarifa.

Ukitoka na fedha zaidi bila taarifa unachukuliwa kamaunatorosha fedha na wanaweza kuzitaifisha.

Hukatazwi kuondoka na fedha zaidi,unachotakiwa ni kutoa taarifa, fedha za nani, unatoka nazo kwa sababu gani, zinaenda wapi etc.

Ili kuzuia money laundering and capital flight.

Ni kitu standard.
 
Hela ni zangu TRA Zinawahusu nini?

Katika kuzitafta hawakumkwekea mazingira Safi ya kuzipata kiurahisi nimeaso alafu kamishna wa TRA analeta fyoko fyoko

Uzoefu wangu. Mtu huwa aambiwi amount ya kutoka nayo nje ya nchi yake, bali bu declare kias wakati wa kuingia nchi YEYOTE, wasilete upuuzi, hizo ndo shule? Hayo ndo madawa? Hizo ndo mshahara? Wasilete upuuzi
 
Ni jambo la kawaida. Hata juzi hapa nikiwa kwenye mizunguko yangu kupitia Ethiopia, tulitangaziwa kuwa kama una pesa inayozidi dUSD 3,000 lazima ujaze fomu. Hata kama unaunga safari kwa maana ya transit passenger
 
Hela ni zangu TRA Zinawahusu nini?

Katika kuzitafta hawakumkwekea mazingira Safi ya kuzipata kiurahisi nimeaso alafu kamishna wa TRA analeta fyoko fyoko

Uzoefu wangu. Mtu huwa aambiwi amount ya kutoka nayo nje ya nchi yake, bali bu declare kias wakati wa kuingia nchi YEYOTE, wasilete upuuzi, hizo ndo shule? Hayo ndo madawa? Hizo ndo mshahara? Wasilete upuuzi
Uzoefu wako mdogo.

USA unatakiwa ku declare kiasi unachotoka nacho kama kimezidi USD 10,000.

Kuna mMexico mmoja alijipigiza USA kazi za kuosha vyombo miaka kibao, akadunduliza na ku save $60,000. Akapiga mahesabu hizi zinanitosha kwenda kuanzia maisha kwetu Mexico.

Ile anataka kuondoka USA wakamdaka ana hela zaidi ya $10,000 ambazo haja zi delare.

Wakazichukua na kumfungulia kesi ya kutorosha fedha za nchi kinyume na sheria.

Hili si jambo jipya, lilitakiwa kuwepo siku nyingi sana kuzuia capital flight na money laundering, tatizo sheria za Tanzania huku bara na Zanzibar zingeweza kuleta mtafaruku wa kikatiba kwa kuwa fedha si suala la muungano, kilaMzanzibari anayetakakuja bara au mtu wa bara anayekwenda Zanzibar angetakiwa afanye declaration ya hela wakati anasafiri nchini mwake mwenyewe. Hili ndilo lililochelewesha. Sijui wame li reconcile vipi hili.
 
Kwa watu waliosafiri ughaibuni hili ni jambo la kawaida,lakini bavicha watasema tunafukuza wawekezaji,sijui ni muwekezaji gani anatembea na furushi la pesa
Hivi ulishawahi kushika dollar wewe? Yaani dollar 10,000 ni bahasha ile ya barua ndogo ukipanga dollar 100, hazijai! Yaani kila kitu mnashabikia! Wapumbavu sana
 
Hela ni zangu TRA Zinawahusu nini?

Katika kuzitafta hawakumkwekea mazingira Safi ya kuzipata kiurahisi nimeaso alafu kamishna wa TRA analeta fyoko fyoko

Uzoefu wangu. Mtu huwa aambiwi amount ya kutoka nayo nje ya nchi yake, bali bu declare kias wakati wa kuingia nchi YEYOTE, wasilete upuuzi, hizo ndo shule? Hayo ndo madawa? Hizo ndo mshahara? Wasilete upuuzi
Hiyo ndio sheria kama huamini zaa mtoto kisha muue harafu uone sheria itakavyo kufanya
Lazima tuheshimu sheria haijailishi kitu Fulani sababu ni chako au umetafuta mwenyewe basi ufanye utakavyo
 
Kuna hatari ya watu kuanza kuviziana baada ya kukusanya mauzo, Mara paaap..!!!! Unashangaa unasimamishwa na kuambiwa "sisi ni maafisa mamlaka .......tunahitaji kukagua vitu ulivyobeba"
 
Ni kawaida sana.

Marekani ni nchi tajiri sana, lakini hutakiwi kutoka Marekani na fedha zaidi ya USD 10,000 bila kutoa taarifa.

Ukitoka na fedha zaidi bila taarifa unachukuliwa kamaunatorosha fedha na wanaweza kuzitaifisha.

Hukatazwi kuondoka na fedha zaidi,unachotakiwa ni kutoa taarifa, fedha za nani, unatoka nazo kwa sababu gani, zinaenda wapi etc.

Ili kuzuia money laundering and capital flight.

Ni kitu standard.
Nani kakueleza hili? Ukiingia na zaidi ndiyo ya hizo ndiyo unatakiwa kudeclare kwamba ninaingia na fedha za kiasi ya dola elfu kumi au zaidi au hundi hii wame copy na kupaste.
 
Back
Top Bottom