Binadamu kufanya makosa ni kawaida, na pale nilikosea. Hata hivyo, nilijitahidi sana kufanya naye kazi vizuri. Nimekaa naye kipindi cha mwaka mmoja. Unapopewa madaraka inabidi kwanza ujifunze, kwa hiyo nilijitahidi sana kuhakikisha kwamba katibu mkuu huyu, ambaye mimi mwenyewe nilimtafuta, aweze ku-cope na ile ofisi. Lakini kukawa kuna matatizo ya
Kwanza huwezi kumfananisha huyo na akina Thecla Mchauru, Kate Kamba, Dk Msimu ambao kiwango cha elimu yao kidogo ilikuwa zaidi. Hata Halima Mamuya elimu yake iko juu zaidi ya huyu. Huyu alibebeshwa mzigo ambao hakustahili, tulifanya makosa. Tulimbebesha mzito mkubwa wa kiutendaji. Pengine kisiasa kazi nyingine angeweza kuzifanya, lakini kiutendaji
Kuna kazi za utendaji zina miiko yake ambayo kiwango cha elimu yake ilikuwa kidogo kina matatizo.
Raia Mwema: Sawa kulikuwa na makosa, lakini wewe ulimpataje pataje hadi akaukwaa ukatibu mkuu wa UWT? Mama Sophia Simba: Huyu alikuwa mjumbe wa Baraza Kuu la UWT, ndicho kitu kimoja ambacho kilinifanya nimteue. Nimekuwa naye kwenye baraza tokea mwaka 2003. Mimi nimemjua Husna wakati nikigombea ujumbe wa Baraza Kuu. Kwa hiyo, nilipokwenda Arusha yeye ndiye aliyenisaidia kutafuta kura, siyo campaigner, lakini ndiyo nilianza kumfahamu.
Lakini nikamfahamu pia ndani ya vikao. Kwa hiyo nilimjua kwa hivyo. Na kwa bahati mbaya sana, sikujaribu kuomba ushauri kwa mtu yeyote kutaka kujua habari zake zaidi. Ndiyo maana nasema nakiri makosa. Hakuna mtu aliyenishawishi kuhusu yeye.