Fahamu Alama ya jicho lenye maana ya siri kubwa likihusishwa na Ushetani

Mau Mau

JF-Expert Member
Dec 30, 2012
673
478
Dhana ya uwepo wa kitu cha siri imeghubika nembo za kwenye sarafu na kufanywa kuwa ishara au alama inayoonekana.

Alama ya 'Jicho' - hili ni jicho ndani ya umbo la pembe tatu - ni moja ya alama inayohusishwa na masuala ya ushetani ambayo pia imeonekana kuwa na uhusiano wa karibu na Iluminati, kundi la watu matajiri linalosemekana kwamba hutafuta kumiliki mali za dunia kwa nguvu ya shetani.

Alama hii ya jicho inadhaniwa kuficha kitu fulani kwasababu yenyewe ipo sehemu fiche kiasi kwamba sio rahisi kwa mtu kuitambua kwa macho yake moja kwa moja.

Pia inajitokeza sio tu kwa makanisa kadhaa bali pia kwenye majengo yenye kujihusisha na imani za kishetani kote duniani na pia alama hiyo ya jicho ipo katika noti za dola za Marekani pamoja na chapa ya muhuri mkubwa wa Marekani.

Ukweli ni njia ya zamani isiyo ya kawaida ya kuashiria nchi. Na alama ya jicho inaashiria matamanio ya kuwa na sauti au nguvu.

Ukichanganya na lile umbo la piramidi, ni kama ishara ya kundi fulani la zamani.

Lakini kwanini watu hulinganisha alama hii na masuala ya ushetani?

Awali kabisa, alama hiyo ya jicho ilikuwa na Kikristo na matumizi ya kwanza kabisa ya alama hiyo yanahusishwa na michoro ya dini hasa ya kumwakilisha mungu.

Ilibuniwa kama ishara ya uangalizi wa huruma ya Mungu juu ya wanadamu.

Chanzo kingine cha alama hiyo ni kitabu cha zamani kabisa cha nembo ambacho kwa mara ya kwanza kabisa kilichapishwa mwaka 1593. Alama hiyo ya jicho iliwekwa kuashiria 'utakatifu' yaani 'mungu'.

Kujenga yaliopita

Hakuna anayejua chanzo cha ubunifu wa alama hii lakini wa kwanza kabisa kuhusika na ubunifu wake aliihusisha na imani za kidini.

Umbo la pembe tatu lilikuwa ni alama ya muda mrefu ya Utatu wa Kikiristo; yaani Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu; na kuna wakati Mungu aliashiriwa kuwa ndani ya umbo hilo la pembe tatu.

Miale ya mwanga ambayo mara nyingi hungaa ndani ya alama hiyo pia ni miongoni mwa alama za mwanzo kabisa za Kikiristo.

Lakini chanzo cha lile jicho ni nini? Mungu amekuwa akiashiriwa kwa njia nyingi hapo kabla, mfano mkono mmoja unaojitokeza kutoka mawinguni lakini sio kama jicho.
#Itaendelea
 

Attachments

  • 126824455_1030524587371972_4823706654010255899_n.jpg
    126824455_1030524587371972_4823706654010255899_n.jpg
    19.7 KB · Views: 16
Jicho la tatu

Triangle ikiwa na jicho katikati.

Jicho linaloona zaidi ya haya macho mawili,jicho la kiroho
 
Tuliite ni 'Jicho la Upaji'...

Chochote unakiona na kukibaini 'kiakili' huja kwa pembetatu na duara katika fikra ama neno.

Unaweza kubaini maarifa yote, ukweli wa sura na mienendo yeyote ya kijamii kwa alama hiyo.

Katika karne hii tutabaini ukweli wa hii alama na mambo mengi yanaboreka ama kuchukua sura mpya na yenye kheri zaidi kupitia hiyo alama -- uchumi, elimu, ilimu, tamaduni na stawi...

Kilimanjaro, Kibosho, kuna kanisa la kihistoria ambamo alama hii imetumika sambamba na tamko: 'Kaa ndani yangu, nikae ndani yako...' Hili ni fumbo la 'Ufahamu Kristu'... Tanzania tunayofunguo kwa mabadiliko makubwa ya kiuchumi na staaarabu ambayo dunia nzima itajifunza kutoka kwetu... Hiyo alama ndiyo ufunguo wenyewe na maarifa fulani yatakayokuja kuwa wazi miaka michache mbeleni...

Ni alama ya kheri; na jukwaa hili la 'Jamii Intelligence' litaweza kukamilishwa na ufunguo uliopo kwenye alama hiyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom