Facts 13 kuhusu Lowassa na Uchaguzi 2015

Facts 13 kuhusu Lowassa na Uchaguzi 2015

Asee natafuta chance kama yako nakosa, hebu ni PM tuonane uniunganishe na mimi tuwe wote kwenye game.
Nina vijana.

1. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye wapenzi na mashabiki wengi kwa sasa....
...

Mytake: kwa hizi facts zote, ni wazi Lowassa kwa sasa tunakuitaji kuliko kipindi chochote kile katika historia ya Nchi hii...
 
1. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye wapenzi na mashabiki wengi kwa sasa.... (Wewe na ukoo wako tu)

2. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye wasifu na historia kubwa na iliyotukuka katika utendaji wake ndani ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali kwa ujumla.. (Kwa kufukuzwa uwaziri kwa ajiri ya ufisadi)

3. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee ambaye mpaka sasa kashawishiwa na makundi mengi sana ya kijamii, eg. Wakulima, wafanyabiashara, bodaboda, wafugaji, Mamalishe, wachimbaji wadogo wa madini, wanafunzi, wachungaji n.k (Umepayuka)

4. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye ushawishi na nguvu ndani ya Chama Cha Mapinduzi na jamii kwa ujumla (rejea tafiti na takwimu mbalimbali) Hiyo hainiusu wacha wafu wazike wafu wao

5. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee aliyeonyesha uzalendo wake kwa kupigania Nchi yake katika vita vya Kagera 1978/1979. Kwa Nchi nyingi duniani kupigana vita ni sifa muhimu na ziada kwa mtu anayewania uongozi. Kushiriki kupigana vita huchukuliwa kuwa ni kiwango cha juu kabisa cha uzalendo... (Uongo mtupu kawadanganye wadogo wako ambao walikuwa hawajazaliwa)

6. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye maono yaliyowazi katika kuwakomboa wananchi kwa kuonyesha vipaumbele vya Taifa eg. Elimu, Elimu, Elimu, Afya, Kilimo, Kuondoa umasikini, kukuza uchumi n.k Kumbe ndiye aliyeua elimu yetu kwa shule za kanumba bila walimu na madarasa wala mahabara?

7. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee aliye maarufu na ambaye wananchi wana matumaini naye kwa sasa. Hii inatokana na utendaji kazi wake na uwezo wake mkubwa wa kusimamia jambo eg. Shule za kata, mradi wa maji ziwa Victoria, Chuo cha UDOM, maamuzi ya City Water, viwanja vya Mnazi Mmoja na plot No. 125~157 Mikocheni n.k (Mazalio ya Kanumba au yebo yebo kama wewe)

8. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye maamuzi magumu na sahihi kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla...(Kwa kuwaimbia wananchi akiwa kiongozi bila aibu kweli ni maamzi magumu na kuahidi mvua toka Malayasia au Indonesia vile?)

9. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee atakayeweza kusimamia, kurudisha na kuleta nidhamu kwa viongozi na watendaji wa serikali na mashirika ya Umma... (Nidhamu ya kuiba ukiwa madarakani na kujitajirisha?)

10. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye nguvu wa ushawishi wa hoja kwa wananchi na katika vikao mbalimbali vya maamuzi (rejea kikao cha maamuzi kuhusu matumizi ya maji Ziwa Victoria nchini Misri, rejea kikao cha kupitisha maamuzi ya ujenzi wa UDOM n.k)....

11. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee aliyejiandaa kisaikolojia kuingia Ikulu (rejea uchambuzi wa Prof. Kitila Mkumbo).... (Ikulu anaiota tangu hata enzi za Mwalimu kufikia kutoa machozi)

12. Lowassa ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye sifa za ziada kama...
i. Mchapakazi kwa bidii
ii. Msikivu
iii. Mbunifu
iv. Muadilifu
v. Mpenda watu/wananchi
vi. Mvumilivu & Mstahimivu

13. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye dhamira na nia ya dhati kuondoa umasikini uliokithiri (Absolute Poverty).... Arushe hela zetu ili tutyajirike

Mytake: kwa hizi facts zote, ni wazi Lowassa kwa sasa tunakuitaji kuliko kipindi chochote kile katika historia ya Nchi hii...

LOWASA

Kwa mapenzi mema na nchi yetu na mwana (CCM) napenda niwape mfano hai wa Bwana Lowasa asivyo muadilifu na asivyopenda kuwajibika kichama CCM na kiserikali. Tanzania nzima mtakumbuka kuwa huyu mheshimiwa Edward Lowasa alikuwa ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Urais mwaka 1995 na akaenguliwa kwa hoja nzito ya kutokuwa muadilifu na marehemu Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere, kwa ukweli (wala sio tuhuma) kuwa alikuwa amejilimbikizia mali nyingi kwa kipindi kifupi ndani ya CCM na Serikali.Muda mfupi alikuwa ni mtumishi wa CCM, muda mfupi kama Mkurugenzi wa kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha.
Mfano hai wenyewe uko hivi; tufuatane kwa kuusoma tafadhali:-
Mara baada ya kurudi Butiama, 1995, baada ya kuenguliwa kugombea nafasi ya urais, siku moja mapema asubuhi Bwana Lowasa alinipigia simu na kusema yafuatayo:
"Bwana Kasori, naomba uende kumwambia Baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, aende Monduli kusaidia kusafisha jina langu ili nisikose ubunge kutokana na yale aliyonisema Dodoma'. Nilishikilia mkono wa simu (TTCL) kwa zaidi ya nusu saa tukiwa tunazungumza na hatimaye mimi nilipata ujasiri wa kumwambia Bwana Lowasa kuwa siwezi kwenda kusema maneno hayo kwa Baba wa taifa na kwamba akitaka aje Butiama na nitamruhusu waongee ana kwa ana. Nikanyamaza na hatimaye yeye akawa wa kwanza kukata simu. Hiyo ikawa itifaki njema kwangu!
Kesho yake tena asubuhi nilipokea simu, safari hii akawa ni mheshimiwa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa. Kwa maneno yake alisema "Bwana Kasori,jana ulizungumza na Edward Lowasa; naomba ufikishe ombi lake kwa Baba wa taifa tafadhali".
Kutokana na heshima ya Mheshimiwa Mzee Kawawa, nilikubali na nikaenda na kabla ya hapo nilimuomba Mzee Kawawa akae karibu na simu ili nimpe jibu muda si mrefu.
Nilimueleza Baba wa Taifa kuwa "Mheshimiwa Edward Lowasa kupitia kwa Mhe. Mzee Rashidi Mfaume Kawawa anaomba usaidie kusafisha jina lake kule jimboni kwake Monduli ili asikose ubunge kutokana na yale uliyomsema katika Kamati Kuu ya CCM Dodoma". Jibu la Baba wa Taifa alilonipa ni kuwa "Nenda umwambie Mzee Rashidi Mfaume Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa"!
Watanzania wote, leo March19, 2008, nawaomba radhi kuwa jibu hilo kwa uzito wa maneno hayo kuwa "Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa" kweli kwa kuzingatia heshima kati ya wazee hao wawili; "Kawawa sikumwambia hivyo"! Badala yake nilimdanganya (nawaomba radhi tena watanzania) jibu nililompa Mzee Kawawa ni kuwa juma lililokuwa linafuata tungekuwa Dar es Salaam na kwamba aje Msasani aongee na Baba wa Taifa. Mhe. Kawawa alikubali.
Nikarudi kwa Baba wa taifa kusema uongo (naomba radhi tena) kuwa "Mzee Kawawa ameomba mzungumze tatizo la Lowasa tutakapofika Dar es Salaam". Baba wa taifa alikubali na akaagiza nimuombe Mhe. mzee Kawawa kuwa Lowasa na Guninita na wapambe wengine wa Lowasa wote wafike Msasani.
Siku ya siku ikafika. Tukawepo Msasani na Mhe.mzee Kawawa akaja. Lowasa hakuwepo! Sababu anazijua mwenyewe.(muulizeni maana nasema ukweli). Mkutano ulipoanza mzungumzaji wa kwanza nikawa mimi, kueleza lengo la mkutano. Mzungumzaji wa pili alikuwa Baba wa Taifa na swali la kwanza ni kuuliza Lowasa yuko wapi?.
Bila kupoteza wakati Mwalimu alisema "Rashidi , huyu Kasori ananiambai eti niende Monduli nikasafishe jina la Mhe. Lowasa eti asikose ubunge kwamba nilimchafulia Dodoma katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM. Kutokana na ombi lako nilimtuma akuambie usiwe mjinga kama Lowasa. Kasori alikuambia eh?"
Oneni , huko nyuma tayari nilishasema uongo kwa kutosema maneno hayo kwa Mhe. mzee Kawawa. Kweli hilo kurudiwa na Baba wa Taifa kwa Mzee Kawawa mbele yangu lilisababisha kalamu yangu kuanguka, nikatetemeka na nikatokwa na jasho jingi mbele ya hao wazee!!! Bila kutegemea na kwa mshangao mkubwa Mhe. mzee Kawawa alikubali kwa kuitikia "NDIO ALINIAMBIA". Mwalimu akacheka sana!!!! Sababu sijui hadi leo kwa nini alicheka sana.
Kwa kuendelea, Mwalimu alimwambia Mzee Kawawa kuwa "Kasori ana umri mkubwa kuliko Lowasa. Kasori alipata taabu sana kufikisha kwangu ombi la Lowasa na aliniambia kuwa jana yake alikuwa amekataa ombi la Lowasa. Sasa nasema kuwa kwa umri wangu mimi mzee, Lowasa ni mtoto wangu tena mdogo sana. Kwa heshima mliyonayo kwangu na kwa chama cha Mapinduzi mtanishangaa sana mkisikia niko Monduli eti nipo kwenye majukwaa nasafisha jina Bwana Lowasa asikose ubunge.
Kweli Lowasa ni jasiri sana kusema maneno hayo. Hayo ningeambiwa na Kasori tu ningesita kumuamini. Lakini kwamba hata wewe Rashidi ulitumiwa kusema maneno hayo! Huyu Lowasa ni jasiri sana!!. Lakini kwa nini hajatuambia ukweli kuhusu mali hizo ambazo ni nyingi kuliko mimi ambaye nimekuwa Rais wenu kwa kipindi kirefu? Sasa Bwana Rashidi, nakuomba hivi, kamwambie mwenyekiti wa CCM Mhe. Mwinyi aitishe wajumbe wote wa Kamati Kuu, chagueni tarehe na mahali popote Tanzania, mimi nitakuja kumsafisha Bwana Lowasa na nitagharamia mkutano huo kwa hela zangu. Kamwe msitumie hela za chama wala serikali. Monduli sitokwenda,umesikia eh?"
Mkutano ukaisha hapo Msasani. Hadi uchaguzi 1995, unafanyika na kumalizika Baba wa Taifa hakwenda Monduli. Alichukia sana tabia za Lowasa na alimfahamu kama mtu muongo na mwenye kiburi. Hadi Baba wa Taifa anafariki,sikuwahi na hata niandikapo makala hii sijasikia wala kusoma popote ambapo Lowasa anakanusha alivyolombikiza mali akiwa mtumishi wa CCM na serikali kwa muda mfupi kiasi cha kumzidi Rais wa Kwanza !!!
Sasa anatuhumiwa na vyombo vya habari kununua sehemu ya Ranchi za Taifa kwa kuandika majina ya wanafamilia! Kama hilo nalo ni kweli, ningekuwa mimi nisingeota tena kugombea URAIS n.k Tanzania. Bora kuendelea na biashara kwa uwazi kuliko kupitia mgongo au wa serikali au wa chama ( CCM). Huo ndio ushauri wangu kama mwana CCM kwa Lowassa.
Angalia tunavyofanya "total transgression of CCM regulations and ethics." Kamati kuu 1995 ilimwona Mhe. Lowassa hana uadilifu. Mhe. Mkapa baada ya kuingia madarakani baada ya muda si mrefu sijui ni kwa kikao gain cha CCM na taasisi ipi ya serikali akamwona Lowassa ni safi na akamweka katika safu yake ya baraza la mawaziri.
Huyu bwana akaendelea na huo usafi hadi akaukwaa uwaziri mkuu 2005. Yote haya yanatia shaka kama kweli ndani ya CCM na Serikali tuna benki sahihi za takwimu za mienendo kitabia ya wanachama na watumishi wetu kama si kubebana kwa majina tu! Nilinunua gazeti la mzalendo nikampa Baba wa Taifa na aliposoma kuwa Lowassa ni Waziri alimaka AHH!!
Katika hili nabaki nimeduwaa hasa tunapopeana madaraka makubwa ya kuendesha nchi kimzaha tu. Tukumbuke kuwa kwa kila kitu na kwa dini yoyote Mungu huweka wazi mambo mahali na kwa muda atakao yeye.( Time and space) ya Mwalimu J.K Nyerere juu ya Lowassa tuliyapuuza. Sasa Mungu kayaanika! Basi tuone hizi tuhuma za RICHMOND n.k, Mikataba ya Madini, EPA zitakavyoshughulikiwa.
Ni huyu Lowasa leo anasema kanyimwa "Natural Justice" hakuulizwa na kamati , kaonewa, kamati ya Mwakyembe inauonea wivu uwaziri mkuu wake na ni mahiri wa kuchukizwa mikataba mibovu na kudhalilika! Oh kweli?
Hivi Lowassa amewahi kusoma wasifu wa kila mmoja wa hao? Bila kupima uzito, busara na hekima ya maneno yake anasema ameachia ngazi kama alivyofanya Mhe.Alli Hassan Mwinyi, Peter Kisumo, Peter Siyovelwa n.k. Hivi CCM yetu hawa ndiyo viongozi tulio nao ngazi za juu? Wasio sema ukweli? Tukumbuke na kukiri kwa dhati wajibu wa wanachama wa CCM , katika katiba (ccm) inasema 15 (7) " kuwa tayari kujikosoa na kukosolewa…
Watanzania wenzangu haya anayosema Lowasa yanafanana na nukuu niliyoanza nayo? Fikiria nairudia tena "For those winding and crooked courses, are the goings of the serpent, which goes basely upon the belly and not upon the feet!
There is no vile that does cover a man with shame as to be found false and pertifidious" Niharakishe kusema hapa kuwa viumbe vyote ambavyo havikupenda kusema ukweli Mungu aliviadhibu kwa kuvifanya vitembelee matumbo yao milele nyoka wakiwemo! Lowasa, Mwanyika, Hosea na wenzake naomba kama nilivyoanza, tafadhali wasome hiyo nukuu mara kadhaa na waielewe na kuizingatia.
Watanzania wanawashangaa, wanadharau na kuchukizwa na viongozi wasiopenda kusema ukweli kwa maisha magumu waliyo nayo ambayo wao wanawazomea kwa dharau kuwa ni wavivu na wachovu wa kufikiri. Wanasahau kuwa hawa watu wa kawaida ndio wanaozalisha kile kinacholipa mishahara na marupurupu yao.
Kama viongozi wakuu wa CCM, katika hili daima kumbukeni wajibu wenu kwa mujibu wa katiba ya CCM, ibara ya 15 (4) kuwa wakati wote mkweli, mwaminifu na raia mwema wa Tanzania. Onekaneni hivyo kwa vitendo tafadhali. Utaratibu huu wa kusema uongo unadhoofisha amani na utulivu Tanzania.
Hayo niliyasema niko tayari kuyasema bungeni akiwepo Lowasa ikibidi. Hatuwezi kukubali nchi hii kuendelea kuwa na viongozi wa aina hii. WAWE WAKWELI, WASEME UKWELI TU. WANAPOKOSEA HARAKA NA KWA UKWELI NA UNYENYEKEVU WAOMBE RADHI KWENYE VYAMA VYAO, SERIKALINI NA KWA WANANCHI. NI UPUUZI WA HALI YA JUU KUJITETEA OVYO NA KUINGIZA UKABILA ( LOWASSA NA OLE NAIKO) HATA KWA MAKOSA YALIYO DHAHIRI.
Katika mahojiano na TVT Lowassa alikiri kuwa alishindwa kuvunja mkataba wa RICHMOND. Sababu alizitaja. Sawa. Waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa Serikali, kwa mujibu wa kanuni za kudumu za utumishi wa umma ( Toleo 1994), kifungu F33, makosa yake kiserikali ni haya yafuatayo; 33( xi) omission which is against public interest. 33(xiii) negligence occasioning loss to the employer ( yaani serikali na taifa kwa ujumla). 33( xiv) gross negligence in the performance of duty.
Kama mtendaji mkuu wa shughuli zote nzito za serikali bwana Lowassa hana namna ya kujitetea kwa makosa hayo yaliyodhahiri ambayo TANESCO imeendelea kudhoofishwa na RICHMOND kwa yeye kuogopa kutumia utaalam nje ya wale aliowaamini. Mbona tuna vyuo vikuu, je, aalivitumia kikamilifu? Mbona kwa maswala yasiyo na maslahi ya maana tumezoea sasa kukodi wataalam wa nje?
Kwanini hakujiridhisha katika maeneo yote hayo? Tatizo hili ni kubwa sana maana watanzania sasa wanatozwa viwango vikubwa sana kulipia umeme ikiwa ni pamoja na sehemu za uzalishaji zenye kutumia umeme achilia mbali malipo ya capacity charges? Nani anabisha kuwa kwa huu mkataba wa RICHMOND n.k Bwana Lowassa na Wenzake waliweka sahihi za kifo siyo kwa TANESCO tu bali pia cha kuvuruga maendeleo ya nchi yetu na kuendeleza umasikini?
Katika yote haya ambayo yamesemwa, Bwana Lowassa na wenzake wajue kuwa kama watanzania, we have a compelling moral case for complaining against him.
There is also a compelling case that is in Tanzania's self interest. Recently many trade agreements already have made the poorest countries worse off. Such agreement already have condemned to death thousands of our people . Corporations of whatever name do strip Tanzania of its natural resources leaving behind a trail of environmental devastation etc. This is done through very poor legal frameworks. Nimuhimu tukawa na viongozi waaminifu, waadilifu na wasema ukweli. Kwa haya yanayotendeka, something is fundamentally wrong with our government.
Kwa kila maamuzi tunayoyafanya mara zote tuzingatie ni kwa maslahi ya nani; yale ya Taifa ni kipaumbele cha kwanza. Tuzingatie matumizi mazuri ya rasilimali zetu daima. Duniani ziko serikali nyingi tu ambazo zimevunja mikataba mibovu. Kwa ziara nyingi ambazo viongozi wetu wanafanya na baada ya wanahabari kupigia kelele RICHMOND, kwanini Lowassa huko nje hakutaka kujifunza namna ya kuvunja mikataba mibovu?
Yaani umahiri wake uliishia mkataba wa maji Dar es salaam na kiwanja cha Mnazi Mmoja? Mikakati yetu ya maendeleo imekuwa haileti tija iliyokusudiwa moja ya sababu ikiwa a flawed vision of development. Successful countries have a broader vision of what development entails and a more comprehensive strategy for bringing it about.
It is very unfortunate that in the majority of developing countries Tanzania included the nation – state has been weakened thoroughly! Haya maamuzi yanayofanywa na viongozi kama Lowassa ndiyo matokeo ya kutojua namna ya kuthibiti na kutumia kwa uangalifu fursa za kitu kinaitwa UTANDAWAZI.
Government that attempt to control capital flows find themselves unable to do so, as individuals find ways of circumventing the regulations. A county may want to raise the minimum wage, but discovers it can't, because foreign companies operating there will decide to move to a county with lower wages.
Situmeona jinsi waziri Chiligati ( waziri wa kazi wa wakati huo) alivyohenyeshwa na wakubwa – wawekezaji kukataa kulipa kima cha chini hapa Tanzania? Wengine wamepunguza kazi ndugu zetu na sasa ni katika kundi la Machinga! Waziri mkuu wa wakati huo Lowassa alisaidiaje? KIMYA! Dhahiri kinachoonekana hapo ni sense of powerlessness. Kwa kukumbatia matajiri na wakubwa wa nje, kupitia utanzawazi, baadhi ya viongozi wetu kama inavyojidhihirisha kupitia RICHMOND n.k. find their ability to act eroded.
These days it is the order of the day for the electorate to see its government bending before foreigners wenye (mitaji). Day in day out democracy is being systematically undermined. When the electorate shouts through the media etc, no body listens! Wanataka sifa tu.
The electorate feels being thoroughly betrayed. Whether we like it or not, it is perceived, quite rightly, I think the way globalization is currently managed is not consistent with democratic principles. Little weight is given to the concerns and voices of ordinary people and the poor! Kwa kiburi cha wakubwa kutosikia, kutopenda kukosolewa Tanzania inaendelea kubaki masikini. Lowassa na wenzake wangekuwa makini na mahiri katika kusikiliza waandishi wa habari mapema RICHMOND n.k isingetufikisha tulipo sasa ambapo kila siku tunapoteza fedha nyingi.
Tusingekuwa na tume juu ya tume ambazo baadhi tunazibeza kwa kejeli hata kwa kutumia chama (CCM). CCM kweli tunasoma na kuzingatia kwa vitendo wajibu wa mwanachama wa CCM kifungu 15(3) na 15 (4) na 15(7) pamoja na ahadi za mwanachama wa CCM (3) na (4), na (8). Hivi CCM sasa ni mali na jina la mtu; kwamba hivyo mtu akikosolewa hamtaki kuona kakosa na mko tayari chama kife kwa ajili ya mtu mmoja au kundi dogo tu la watu? Nendeni Butiama mtupe majibu tafadhali. Uwezo, busara na nia vyote mnavyo. Ningekuwa Lowassa Butiama nisingeenda. Yeye kwenda huko ni kejeli kwa Baba wa Taifa.
BADO TUTAENDELEA KUWASEMA WENZAO KUHUSU MIKATABA YA HOVYO NA UKWAPUAJI WA RASILIMALI ZA NCHI HII. HOJA YA MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR BWANA IDD PANDU HASSAN- " Lowasa kutostahili kuitwa Waziri mkuu Mstaafu" ni muhimu ikazingatiwa sambamba na utata wa stahili za mafao. Haitoshi kuimba utawala wa sheria na kumbe inapofika kwa wakubwa tunakunja na kunyonga sheria zetu. Sheria ni Msumeno. Someni Pensions Ordinance cap 371 sambamba na kanuni za kudumu za utumishi wa umma toleo la (1994) kifungu F53 (d) na (e). Tusiwe na kigugumizi katika hili.Tujifunze yaliyojiri hapo jirani Kenya hivi majuzi.
Namalizia kwa kusema "Tuheshimu na kudumisha kitu UKWELI". Kwa viongozi, zingatieni na kwa unyenyekevu heshimuni viapo vyenumnapokabidhiwa madaraka. Baba wa Taifa daima katika mkoba wake alibeba Bibilia na Azimio La Arusha.
Nyinyi kwa kipindi hiki kigumu cha ufisadi na kukithiri kwa rushwa na mikataba mibovu; bebeni daima photo-copy za viapo vyenu pamoja na Bibilia au Koran pamoja na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mnazo dini zenu. Sikusikia yeyote akiapa kwa dini za asili kwa Rais au kwa Spika wa Bunge. Nawashukuru watanzania, Mhe. Spika na Waandishi wa habari ambao wamekemea maneno ya Lowasa na wenzake baada ya kikao cha Bunge.
Namshukuru sana Mhe. William H. Shelukindo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji na Biashara kwa kuwasilisha hoja ya kuundwa kwa kamati ya kuchunguza Richmond na shukran maalum nazitoa kwa Dr. Mwakyembe na wajumbe wote walioshughulikia suala la Richmond na kuwasilisha taarifa Bungeni kwa uadilifu mkubwa sana.
Mwisho nawashukuru Watanzania wote na nchi za nje walionipongeza na kunipa moyo kuhusu makala zangu za kukemea ukwepuaji rasilimali za nchi BoT yenye kichwa cha habari "Salaam kwa Mawaziri" Namshukuru Rais Kikwete. Namshukuru pia Mhariri gazeti la Rai namba 748 na 749. Halmashauri kuu ya CCM inayokutana Butiama naitakia mafanikio makubwa katika maazimio watakayofikia . Baada ya hapo muonekane mmedhamiria kutenda kwa kuleta maendeleo yenye kuzingatia uadilifu na uwajibikaji
Viongozi wabovu wawajibishwe tu.
Watanzania wengi leo bado wanamlilia Mwalimu J.K. Nyerere hasa kwa matatizo kama haya ya mikataba mibovu ya Madini, RICHMOND n.k. Wanasema sorry Mwalimu lived ahead of his time. Alituangazia kwa mengi, hakuna wa kututetea leo kwa matatizo yote haya.
Mungu Ibariki Tanzania. Mungu Ibariki Afrika
Samwel. H. Kasori
Katibu mstaafu wa J.K.Nyerere
0754 372141
 
Lowasa ndio mtarajiwa pekee anaetishia future ya wachafuzi wa nchi hii hasa wanaompinga
 
Lowasaa ni mkristo safi anayeamini katika kusamehe 7 mara 70..... Swala la afya siyo kweli Edward yuko fiti asilimia 100, na infact hilo ni swala ambalo mamlaka nayo analo Mungu.....

Bwana Ocampo Four
Ni kweli kabisa uyasemayo kwa asilimia mia, ila sote tunajua lazima tahadhari zichukuliwe Lowasa ni mgonjwa na kila mtu anafahamu. Naomba tufanye jambo moja tusubiri Mungu atatuonyesha picha kamili.
Namuombea afya njema Edward Ngoyai Lowasa
 
yani bado hujanishawishi eti lowassa awe kiongozi wa nchi kwa mtonyo gani wa maana alioufanya kwa nchi yetu pendwa :what:
labda utahitaji miaka elfu moja unishawishi na kumsafisha boss wako kwa kashfa zinazomkabili za ufisadi. then huyu jamaa sio presidential material haendani kabisa labda ajaribu uraisi mwingine lakin sio wa nchi mtakuwa mnachekesha sana...
 
We unaejiita mwananchi kweli unamfahamu sana lowasa.lakini kwanini basi umfahamu zaidi lowasa kuliko wengine? Kuna jambo mlikuwa mnashirikiana au ,la we nyumba ndogo ya edo.pole ali ku du sasa ,kakutema.tulia tafuta mwingine magomeni wamejaa au uende mombasa wako tele.
 
1. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye wapenzi na mashabiki wengi kwa sasa....

2. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye wasifu na historia kubwa na iliyotukuka katika utendaji wake ndani ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali kwa ujumla..

3. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee ambaye mpaka sasa kashawishiwa na makundi mengi sana ya kijamii, eg. Wakulima, wafanyabiashara, bodaboda, wafugaji, Mamalishe, wachimbaji wadogo wa madini, wanafunzi, wachungaji n.k

4. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye ushawishi na nguvu ndani ya Chama Cha Mapinduzi na jamii kwa ujumla (rejea tafiti na takwimu mbalimbali)

5. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee aliyeonyesha uzalendo wake kwa kupigania Nchi yake katika vita vya Kagera 1978/1979. Kwa Nchi nyingi duniani kupigana vita ni sifa muhimu na ziada kwa mtu anayewania uongozi. Kushiriki kupigana vita huchukuliwa kuwa ni kiwango cha juu kabisa cha uzalendo...

6. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye maono yaliyowazi katika kuwakomboa wananchi kwa kuonyesha vipaumbele vya Taifa eg. Elimu, Elimu, Elimu, Afya, Kilimo, Kuondoa umasikini, kukuza uchumi n.k

7. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee aliye maarufu na ambaye wananchi wana matumaini naye kwa sasa. Hii inatokana na utendaji kazi wake na uwezo wake mkubwa wa kusimamia jambo eg. Shule za kata, mradi wa maji ziwa Victoria, Chuo cha UDOM, maamuzi ya City Water, viwanja vya Mnazi Mmoja na plot No. 125~157 Mikocheni n.k

8. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye maamuzi magumu na sahihi kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla...

9. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee atakayeweza kusimamia, kurudisha na kuleta nidhamu kwa viongozi na watendaji wa serikali na mashirika ya Umma...

10. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye nguvu wa ushawishi wa hoja kwa wananchi na katika vikao mbalimbali vya maamuzi (rejea kikao cha maamuzi kuhusu matumizi ya maji Ziwa Victoria nchini Misri, rejea kikao cha kupitisha maamuzi ya ujenzi wa UDOM n.k)....

11. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee aliyejiandaa kisaikolojia kuingia Ikulu (rejea uchambuzi wa Prof. Kitila Mkumbo)....

12. Lowassa ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye sifa za ziada kama...
i. Mchapakazi kwa bidii
ii. Msikivu
iii. Mbunifu
iv. Muadilifu
v. Mpenda watu/wananchi
vi. Mvumilivu & Mstahimivu

13. Lowassa, ndiye mgombea mtarajiwa pekee mwenye dhamira na nia ya dhati kuondoa umasikini uliokithiri (Absolute Poverty)....

Mytake: kwa hizi facts zote, ni wazi Lowassa kwa sasa tunakuitaji kuliko kipindi chochote kile katika historia ya Nchi hii...

Utakuwa umetumwa wewe. Msimamisheni muone
 
Bwana Ocampo Four
Ni kweli kabisa uyasemayo kwa asilimia mia, ila sote tunajua lazima tahadhari zichukuliwe Lowasa ni mgonjwa na kila mtu anafahamu. Naomba tufanye jambo moja tusubiri Mungu atatuonyesha picha kamili.
Namuombea afya njema Edward Ngoyai Lowasa

Mkuu hmjamii ugonjwa wa Lowassa unakuzwa na magazeti yanayotumiwa na Membe e.g Raia Tanzania, Sauti Huru, na Tafakari....

Lowassa ameendelea kuwa mzima wa afya njema.... Hilo ndiyo jambo la kumshukuru Mungu...
 
14. Lowassa ndio mgombea pekee ambaye ni Mgonjwa

Mussolin5 viongozi karibu wote Tanzania ni wagonjwa wa magonjwa makubwa tena sana sana ila Lowasa amezidi sana na ndio maana amefikia hatua ya kuwa anageuka kama robot
 
Bwana Ocampo Four
Ni kweli kabisa uyasemayo kwa asilimia mia, ila sote tunajua lazima tahadhari zichukuliwe Lowasa ni mgonjwa na kila mtu anafahamu. Naomba tufanye jambo moja tusubiri Mungu atatuonyesha picha kamili.
Namuombea afya njema Edward Ngoyai Lowasa

hivi mgonjwa anaweza kukimbia lilomita 5 acha ushabiki wa kip...uzi
 
Mangula pia mnafiki kutwa vikao vya siri na Jack Gotham ndo maadili hayo? Mangula na nape mnatumika kulipa fadhila lakini nawaambieni wana CCM hatudanganyiki na jidanganyeni eti mmewahi kukata watu na chama hakijayumba nawaomba sana mjaribu haka kamchezo kenu ambacho mnakapangia mikakati ya gizani eti kuwasuprise wanaccm Naapa pigo mtakalo pata mtaandikwa kwenye vitabu vya historia ya ccm
hawawezi kumkata jina mkuu utaona
 
HIZO SIFA MBONA KAMA DESA/PAMPHLET LA NYAMBARI NYANGWINE?POINT MOJA IMENYUMBULIWA IKAZAA POINT3.UTOTO HUU,TUNAJUA UMEKULA HELA HUYU MTU AMEKUWA SERIKALINI MUDA WOTE Ana LIPI JIPYA ALISHINDWA KUFANYA AKIWA PM ANATAKA AFANYE SASA AKIWA RAIS WA JMT?
 
Kama kuna watu wanataka kuhaini taifa ni hii team lowassa.Kwa sababu ya posho zao,wanataka kutuzika shimoni.Leo tu imetoka habari mtoto wake kahausika kwenye ufisadi wa kutisha,afu mwezi oktoba awe kwenye first family,si TRA itakuwa family saccos.
 
Back
Top Bottom